Athumani malumalu
New Member
- Mar 24, 2022
- 4
- 4
Katika mfumo bora wa uongozi na uendeshaji wa mamlaka utawala bora ni muhimu kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na huduma sawa na zenye tija.
Katika taifa letu wimbi la uongozi m bovu katika ngazi za chini za utawala limekuwa kubwa na hii pengine ni kutokana na serikali kutofuatilia mienendo na maadili ya viongozi wanao pewa dhamana kuiwakilisha serikali kwa wananchi wake.
Sehemu kubwa ya viongozi wanaohudumu maeneo hasa ya vijiji wanakosa maadili katika utendaji na kufanya wananchi hao kushindwa kuziona juhudi zinazo fanywa na serikali katika kuhakikisha kila mmoja anapata haki na usawa kama mwananchi.
Idadi kubwa ya wananchi wanaoishi vijijini ni wakulima na wafugaji ambao hawana elimu yakutosha juu ya sheria, na haki zao na kupitia hili viongozi wasio waadilifu wanatumia kuwanyanyasa kwakuwatoza faini kubwa zisizo halali katika makosa, vile vile uanzishaji wa faini binafsi kama vile faini ya meza, pesa ya mgambo na faini yauangalizi endapo utawekwa rumande
Tabia hizi za viongozi wasio waadilifu ni moja ya sababu kubwa na chochezi inayofanya wananchi wengi kupoteza imani na serikali yao na wengine hata kushindwa kushiriki katika mambo muhimu ya uendeshaji na maendeleo ya taifa letu.
Na pengine hii ni kwasababu ya kuelekeza nguvu kubwa katika ngazi za juu za utawala kama, wilaya, mikoa, miji na majiji na kusahau kutenga muda wakutosha wa ufatiliaji wa mienendo ya viongozi wa ngazi za chini kabisa kitu kinachopelekea kuongezeka kwa wimbi la rushwa, ukiukwaji wa haki za binadamu, matumizi mabaya ya mamlaka na upotevu wa rasimali za taifa.
Katika kufikia matarajio ya utawala bora lazima serikali ikubali kuweka misingi imara ya ufatiliaji wa karibu wa viongozi wanao hudumu vijijini kujiridhisha na kuhakikisha sheria na haki stahiki za wananchi zinafuatwa.
Vile vile ni bora serikali kuandaa semina maalum kabisa katika vijiji vinavyo gundundulika kuwa na wimbi kubwa la matatizo ya namna hii ili kuondoa dhana potofu inayotengenezwa na wananchi juu ya serikali yao
Vile vile ni vyema serikali kuweka utaratibu maalumu kwa wabunge kuwafikia wananchi wao kwa muda ili kupata taarifa sahihi za kero za kuziwasilisha serikalini kwa usahihi, kwani wabunge wengi wamekuwa wakionekana maeneo yao hasa nyakati za uchaguzi tu na kusababisha kushindwa kujua kero sahihi za wananchi katika maeneo baadhi ya majimbo hasa yale ya vijijini.
Vile vile utekelezaji hafifu wa miundo mbinu katika maeneo ya vijiji zalishi bado ni changamoto kubwa jambo linalopelekea wananchi wanaotegemea mazao ya shambani kuona kutelekezwa na serikali yao kwani kadhia hii imekuwa kichocheo kikubwa katika mfumko wa bei ya chakula hasa mazao ya shambani kutokana gharama kubwa za ufikishaji wa mzigo katika eneo husika(sokoni) . Kutokana na umuhimu huu ni vyema sana serikali kuchukuwa hatua za makusudi za ufuatiliaji wa sera ya utawa bora katika ngazi hizi za utawala ili kumhakikishia mtu ili kuliokoa taifa kutokana unyanyasaji, ujinga, maendeleo haba, rushwa na uoga katika kushiriki shughuli za maendeleo.

Upvote
1