Utawala Bora na Uwajibikaji

Utawala Bora na Uwajibikaji

Chuwa jr

New Member
Joined
Oct 17, 2020
Posts
3
Reaction score
1
Habari wakuu!

Katika Nchi zilizoendelea na zinazoendelea suala la utawala bora na uwajibikaji ni kipaumbele cha kwanza ambacho kinawezesha nchi kuleta matokeo chanya mfano kwa hapa Tanzania suala la utawala bora na uwajibikaji bado halina nafasi kubwa hivyo hupelekea baadhi ya maeneo ya kiutawala kutoleta matokeo mazuri haswa.

Kwa upande wa watendaji wa serikali wengi wanafanya kazi kimazoea, kisiasa au kwa kujuana inakuwa ngumu msomi aliyesomea masuala ya kiutawala kusimamiwa na mwanasiasa ambaye yeye anafanya kazi kwaajili ya wananchi wake ili apate kura ikiwa ni tofauti na mwenendo wa kiutawala (utaalamu) na hupelekea baadhi ya miradi kukwama au kufanyika bila ya usimamizi yakinifu Ushauri wangu kwa serikali iteuwe viongozi wenye taaluma katika fani husika ili wawe na maono sawa ili kutoa matokeo chanya.
 
UTATUZI wa Yote hayo ni KATIBA MPYA KATIBA iliyopo inampa Mtu mmoja KUTEUA Watu Awatakao ndio maana hata Wahuni wanateuliwa ,Ndugu,Kabila lake,kada hata kama hawana VIGEZO WANATEULIWA
 
Tatizo la kwanza ni chama kimoja kubaki madarakani kwa muda mrefu ni hasara kwa Taifa. Maana yake wanachama ambao ndiyo waandamizi wa serikali hawatakuwa tayari kuyaweka wazi makosa waliyoyafanya na kuruhusu uwajibikaji.
 
Sahihi kabisa, CCM ndio tatizo kubwa hapa - matatizo mengine yamo ndani ya hilo furushi liitwalo CCM.

Katiba Mpya ni muhimu mno kwa sasa kuliko wakati mwegine wowote wa historia ya nchi yetu.
 
UTATUZI wa Yote hayo ni KATIBA MPYA KATIBA iliyopo inampa Mtu mmoja KUTEUA Watu Awatakao ndio maana hata Wahuni wanateuliwa ,Ndugu,Kabila lake,kada hata kama hawana VIGEZO WANATEULIWA
Yah!nikweli mkuu
 
Back
Top Bottom