SoC03 Utawala Bora ni Haki kwa Nchi Huru

SoC03 Utawala Bora ni Haki kwa Nchi Huru

Stories of Change - 2023 Competition

Joshua Deus

Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
50
Reaction score
21
UTAWALA BORA NI HAKI KWA NCHI HURU

Utawala Bora ni mchakato wa kupima ni kwa jinsi gani taasisi za umma, zimeshughulika na Mambo ya umma kwa ufanisi na kutambua haki za binadamu na maadili ya kutotumia mamlaka vibaya kwa watumishi wa umma na kutojihusisha na vitendo vya rushwa na kuwepo kwa uongozi wa kisheria.

FAIDA ZA KUWEPO KWA UTAWALA BORA
Kujenga Imani kati ya mtawaliwa na mtawala
Viongozi wengi wa umma wakipewa mamlaka na nafasi ya kuwatumikia wananchi wengi hutumia vyeo vyao vibaya wengine wakidhani wanao waongoza hawana akili na hawaelewi kinacho endelea hivo watu hubakia na manung'uniko juu ya uongozi unao waongoza

Kuwepo kwa Taasisi imara,
kunapokua na utawala Bora serikali watu watatendewa haki kwa sababu ya uwepo wa utawala Bora,na Taasisi imara zinazo tekeleza majukumu yake vyema hivyo kupungua,au kutokuwepo kwa malalamiko miongoni mwa watawaliwa au watendakazi.
Kuimarika kwa shughuli za kiuchumi,
Unarahisisha utendendaji wa kazi,Utawala Bora unatoa fursa kwa kila mtumishi kuzingatia matakwa kisheria na kikanuni katika utekelezaji wa majukumu yake,na kutengeneza mahusiano Bora miongoni mwa watenda kazi,hata wanaopewa huduma kutoka Taasisi mbali mbali kuopata kwa viwango bora.
Kunapokua na mazingira mazuri ya Amani inavutia uwekezaji wa biashara na shughuli za utalii hivyo inapelekea kukua uchumi wa nchi na pato la mtu mmoja mmoja.



1.1774256.jpg


(Picture Credit: Utumishi wa umma)

SABABU ZINAZOZUIA UTAWALA BORA
Rushwa; Hii Ni moja ya sababu kubwa inayo pelekea kuzuia Changamoto hii,viongozi wengi wa umma wanatumia mamlaka Yao kujitajirisha wenye na familia zao na kutokujali mahitaji ya wananchi wao, ndio maana hata leo Kuna kujua baadhi ya sekta na so huduma kwa usawa mfano sekta ya ajira na Afya wengi inawalizimu kutoa rushwa ili wafanikishe malengo Yao.

Umaskini na kutokua na usawa wa mgawanyo wa rasilimali
Umaskini ulio kithiri ni sababu kubwa inayo pelekea machafuko na kudhoofisha utawala bora,na serikali kushindwa kufikia maeneo yanayo zalisha kidogo kulingana na Yale yenye rasilimali nyingi hivyo kukwamisha mafanikio ya utawala Bora.

Migogoro ya kisiasa
Kuwepo kwa migogoro ya kisiasa inayotengenezwa na vyombo vya ulinzi kutumika kisiasa inapelekea uhasama na ugomvi baina ya chama tawala na vyama vya upinzani ambapo hupelekea chuki na kudidimizwa kwa haki upande usio na nguvu hivyo kubaki kwa malalamiko kwa kubinywa haki za wananchi wote.

ZIFUATAZO NI HATUA ZA KUHAMASISHA UTAWALA BORA
Kuanzisha sheria imara kupambana na rushwa
Serikali itumge sheria ambazo zitamfanya kiongozi wa umma asitamani kula rushwa Hii itahamasisha sehemu kubwa kuondokana na tatizo hili

Kuboresha uwajibikaji na uwazi,
Mara nyingi viongozi wa umma wamekua hawawajibiki na kukumbwa na urasimu mkubwa katika utekelezaji wa majukumu Yao wanapoa amua kufanya majukumu Yao kwa weledi na kwa uwazi hii itachochea kwa Kasi kubwa utawala Bora.

Kuupa nguvu ushirikiano wa kikanda,
Wahenga walisema umoja Ni nguvu utengano ni dhaifu,kupeana uzoefu wa kukabili Changamoto na kufanya Mambo kwa ufanisi Ina boresha utenda kazi lakini pia kuumarika kwa ulinzi na Amani katika mazingira hivyo inasaidia kuwepo kwa utawala bora.

Kupambana na umaskini na kuepuka kutokua na usawa katika mgawanyo wa rasilimali,

Serikali inapochagua kufanya maendeleo ifanye kwa usawa na sio kwa uoendeleo wa kikanda,kikabila hii inasaidia Sana kwa kiasi kikubwa kuumarika kwa utawala Bora.

Kuwawajibisha viongozi wa umma walio kwenda kinyume na taratibu za utumishi wa umma
Kumekua na viongozi wengi wanafanya makosa ya kuhujumu pesa za umma,lakini Hakuna hatua zozote wanazo chukuliwa ili wajutie kuvunja taratibu za utumishi hii inawapa hasira wananchi na kutokua na Imani na viongozi wao.

Viongozi wa serikali, wananchi na kila rika, na kundi katika jamii inapaswa kuhakikisha inapaza sauti ili kuhakikisha haki, usawa na uwajibikaji wa viongozi wa umma unakua katika viwango vya juu, hii itasaidia kuwa na taifa lenye amani, umoja na upendo na kuishi bila uhasama, tukiungana kwa pamoja na kuwa na kitu kimoja kama nchi itafanya kila mtu kufanya kwa majukumu yake kwa furaha pia wananchi watafurahia viongozi wao.

 
Upvote 3
Naomba Kura zenu wadau mnaopita kusoma chapisho hili,lakini maoni na ushauri wenu Ni wa muhimu Sana kwangu,karibuni na Asantee.
 
Aiseee jamaa kweli umeandika,hasa sekta ya ajira yaani hapa ni kujuana sana,Kama hauna connection,elimu yako inaonekana haina maana.
 
Back
Top Bottom