Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Hakuna Taifa ambalo halina mfumo wa Utawala, kila Taifa Duniani lina mfumo wake wa Utawala. Hapa ndipo tunapopata aina mbili za utawala yaani Utawala Bora na Bora Utawala. Hii Bora Utawala ni aina ya utawala isiyofuata misingi ya Sheria na ikishamiri sana kwenye taifa lolote basi huenda ikasababisha vilio, dhulma, maumivu nk katika Taifa husika. Ogopa sana Taifa linaloendeshwa kwa misingi ya Bora Utawala.
Utawala bora ni matumizi ya mamlaka ya kisiasa, kiuchumi kijamii au vinginevyo katika kusimamia masuala ya nchi kwenye ngazi zote. Utawala bora ni matumizi ya mamlaka ambayo yanakuwa na uwazi, uwajibikaji, ushirikishwaji wa watu, ufanisi, tija, uadilifu usawa na unafuata utawala wa sheria.
Dhana ya Utawala Bora inabebwa na nguzo muhimu zifuatazo; Katiba ya kidemokrasia (yenye msingi wa maoni ya wananchi), Uhuru wa Mahakama, Uhuru wa vyombo vya habari, kulinda Haki za Binadamu, Mgawanyo wa Madaraka.
Kuna mifano mingi sana ya kuelezea jinsi viongozi wanavyopaswa kuishi kwenye misingi ya Utawala Bora. Fikiria mtu aliyeamini kama Paul Makonda na mpaka kupewa Ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam lakini kiburi kikamjaa na kuamua kukandamiza Utawala Bora na kuongoza kadri ya Utashi wake, Cheo ni dhamana na sasa hivi hana cheo chochote amebaki kulalamika kuwa anataka kupotezwa lakini kama kwenye utawala wake angebeba ile misingi mikuu ya utawala bora basi angekuwa sehemu salama kama viongozi wengine waliomaliza muda wao na wanaishi kwa amani na wananchi
Na ili kutekeleza dhana ya Utawala Bora mambo yafuatayo ni lazima yazingatiwe; matumizi mazuri ya rasilimali kwa faida ya Wananchi, Viongozi kujua na kutambua madaraka waliyonayo na mipaka yao, matumizi sahihi ya Dola, nguvu ya kila Muhimili (hakuna muhimili unaomeza mingine) kulingana na mipaka iliyowekwa na Katiba na Sheria.
Zifuatazo ni faida chache kati ya nyingi za kuwa na Utawala Bora;
Mataifa mengi hususan Afrika yamekuwa yanaangukia katika Bora Utawala na machache yanaangukia katika Utawala Bora. Hakuna namna maisha yatabadilika bila ya kila Taifa kuikubali na kuitumia dhana hii ya Utawala Bora kwasababu UTAWALA BORA ndiyo nyenzo muhimu sana ya kufanikisha ajenda kuu za Taifa lolote na za Dunia kwa ujumla ambazo ni Maendeleo Endelevu na ustawi wa wananchi kwa kulinda na kutetea Haki ili pamoja na mambo mengine kuifanya Dunia kuwa sehemu salama zaidi kwa Binadamu kuishi.

- Kuleta ustawi wa Wananchi
- Matumizi mazuri ya rasilimali
- Huduma bora za kijamii
- Kuheshimiwa kwa Haki za Binadamu
- Utatuzi wa migogoro kwa mujibu wa sheria.