Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoendelea duniani na iliyojaliwa rasilimali nyingi ambazo kama zikisimamiwa na kutumiwa vizuri zitakuza uchumi na kuleta maisha bora kwa wananchi. Ili ziweze kusimamiwa na kutumiwa vizuri na ili uchumi uweze kukua na kuleta maisha bora kwa wananchi, serikali na vyombo vyake haina budi kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia kanuni za utawala bora na uwajibikaji.
Kwenye ripoti ya mwaka huu ya utawala bora (The Chandler Good Government Index 2021), Tanzania imeshika nafasi ya 83 kati ya nchi 104 zilizofanyiwa utafiti duniani. Kwenye ripoti ya kupambana na rushwa (Corruption Perceptions Index 2020), Tanzania imeshika nafasi ya 94 kati ya nchi 180 zilizofanyiwa utafiti duniani. Kwenye ripoti ya utawala bora kwa nchi za Afrika (Ibrahim Index of African Governance Index Report 2020), Tanzania imeshika nafasi ya 19 kati ya nchi 54 zilizofanyiwa utafiti. Ripoti zote hizi zinaonyesha maeneo tuliyofanya vizuri na tunayotakiwa kuboresha.
Kwenye makala haya nimeainisha vichocheo kumi vya mabadiliko katika utawala bora na uwajibikaji ili Tanzania tunayoitaka iwezekane. Katika muktadha huu, utawala bora na uwajibikaji una maana ya utendaji wa shughuli za serikali unaozingatia 1) utawala wa sheria na wa haki, 2) kushiriki kwa wananchi na sekata binafsi katika shughuli za serikali, 3) mgawanyo na usimamizi mzuri wa rasilimali za taifa, 4) uwazi katika ngazi zote za utendaji wa serikali, 5) uchumi jumuishi, 6) uchaguzi huru na wa haki, 7) uvumilivu wa kisiasa na maoni mbadala, 8) uhuru wa maoni na 9) juhudi za kupambana na kuzuia rushwa.
Utawala wa sheria na wa haki
Katiba ya nchi, na katika muktadha wa makala haya Katiba bora, ndiyo sheria mama inayoweka misingi mizuri ya sera, sheria, kanuni, taasisi na mifumo imara ya uendeshaji wa serikali na vyombo vyake. Ili Katiba iwe bora na izae sheria na kanuni nzuri, dhana ya utawala wa sheria haina budi iendane na dhana ya utawala wa haki.
Kwa hiyo, kuna umuhimu wa kuwa si tu na Katiba Mpya, bali Katiba bora inayoweka misingi mizuri ya mgawanyo mzuri wa madaraka na mamlaka na uendeshaji wa shughuli za serikali na sera za taifa. Lengo lake ni kulinda na kudumisha haki na amani, utengamano wa wananchi na kujenga taifa huru linaloheshimu demokrasia ya vyama vingi, haki za binadamu, utawala bora, maendeleo endelevu na kuwa na taifa linalojitegemea.
Ni muhimu pia kuweka maadili na miiko ya uongozi na utumishi wa umma, kwa kubainisha kwamba uongozi ni dhamana na mtu akichaguliwa au akiteuliwa kuwa kiongozi basi kuchaguliwa au kuteuliwa kwake kuzingatie sifa za uongozi, uadilifu wake, uwazi, mchakato huru na wa haki na ushauri mzuri wa mamlaka za uteuzi. Mabadiliko ya mara kwa mara ya sheria zetu ni ishara wazi kwamba tunahitaji Katiba bora itakayozaa sera, sheria na kanuni nzuri na za haki zinazoweza kudumu kwa muda mrefu.
Kushiriki kwa wananchi na sekta binafsi
Wananchi hawana budi kushiriki katika shughuli za serikali yao na katika masuala yote yanayohusu maisha yao wao wenyewe, kupitia vikao vyao halali au wawakilishi wao na kupata mrejesho kwa wakati wa nini kifanyike kuhusu maendeleo yao na ya taifa lao. Hii ni pamoja na kushiriki kwa sekta binafsi, ambayo ndiyo injini ya maendeleo ya taifa letu kwa kuajiri watu wengi zaidi. Hivyo, Tanzania tunayoitaka ni ile yenye maendeleo shirikishi kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
Mgawanyo na usimamizi mzuri wa rasilimali za taifa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imebarikiwa kuwa na ardhi nzuri na yenye rutuba na rasilimali nyingi ambazo hazipatikani katika nchi zingine Afrika na duniani. Kuna madini ya aina mbalimbali, mafuta, gesi asilia, mbuga nyingi za wanyama na maeneo saba ya urithi wa dunia na mengine matano yanasubiri kuidhinishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco).
Kuna pia wanyama, ndege na mimea ya aina mbalimbali kama vivutio vya utalii, ambavyo kama vikitunzwa na kuendelezwa kwa manufaa ya wote ni mtaji mkubwa kwa maendeleo yetu, kwani vyote hivi vinatengeneza ajira nyingi na vinatuweka kwenye nafasi nzuri ya kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini. Hii ni pamoja na miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa sehemu mbalimbali nchini. Ni jukumu la kila mmoja wetu, hasa waliopewa dhamana kuzisimamia vizuri rasilimali za taifa kwa niaba yetu, kuhakikisha zinaendelezwa na kutumiwa kwa manufaa ya wote.
Uwazi serikalini
Uwazi katika ngazi zote za utendaji serikalini unajenga na kuongeza imani ya wananchi kwa serikali yao na kwa viongozi wao na kuondoa mashaka yasiyo ya lazima yanayosababishwa na kukosa taarifa sahihi. Uwazi hauna maana ya kuanika kila jambo hadharani hata siri za serikali au nchi, bali ni kuwapa wananchi taarifa sahihi za mambo muhimu yanayowahusu ili ziwasaidie kuona na kutumia vizuri fursa zilizopo katika taifa lao na kujiletea maendeleo.
Uchumi jumuishi
Ni muhimu kujenga uchumi jumuishi unaolenga kuinua maisha ya wananchi wote na kuondoa umaskini kwa wenye kipato cha chini, ambao mara nyingi wanaishi maisha ya dhiki kutokana na kukosa fedha na mbinu za kujikwamua kwenye dimbwi la umasikini linalowazunguka. Na pale wanapopata fedha hata kama ni kidogo ni muhimu kujenga utamaduni wa kuweka akiba kidogo kidogo, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuwekeza kwenye miradi inayowezekana na itakayowasaidia kuongeza kipato, kujitegemea na kuboresha maisha yao na ya familia zao. Kukua kwa uchumi inabidi kulete pia mabadiliko chanya katika maisha ya watu wa kawaida.
Uchaguzi huru na wa haki
Ni haki ya kikatiba wananchi waliofikisha umri wa kupiga kura na waliojiandikisha kushiriki uchaguzi wa viongozi wenye sifa na waadilifu na wanaotokana na mchakato huru na wa haki. Mchakato wa kuwapata viongozi wa kugombea au kuteuliwa uongozwe na sifa na uadilifu na kuwa kiongozi maana yake ni kuwa mtumishi wa wananchi na siyo bosi wao. Nafasi za uteuzi nazo zifuate mchakato wa haki kwa maana ya kwamba anayeteuliwa ana sifa za kushika nafasi hiyo na wala si zawadi au upendeleo.
Uchaguzi uzingatie mchakato huru, wa wazi na wa haki wa kumpata mgombea, kumpigia kura, kuhesabu na kutangaza matokeo kwa wakati na mgombea anaweza kuwa ni mtu anayetokana na chama cha siasa au mgombea huru. Ikitokea kuna malalamiko ya ukiukwaji wa utaratibu au mchakato wa uchaguzi na kama ni lazima kuchukua hatua, walalamikaji waweze kukata rufaa kwa vyombo vinavyohusika na usikilizaji wa malalamiko, kuyapitia na kuyatolea uamuzi wa haki. Ni muhimu pia kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi inayotimiza majukumu yake kikamilifu.
Njia mojawapo ya kufanya Tume Huru ya Uchaguzi kuendelea kufanya kazi kwa haki ni kuweka utaratibu wa kuweza kupinga matokeo yanayolalamikiwa mahakamani kwa mgombea yeyote wa uchaguzi, endapo wadau wa uchaguzi watakuwa na sababu za kufanya hivyo. Tukifanya hivi tutaepuka malalamiko kwamba baadhi ya viongozi tunaowachagua si wale waliochaguliwa na baadhi ya wale waliochaguliwa si wale tuliowachagua wakati wa kupiga kura.
Uvumilivu wa kisiasa na maoni mbadala
Tujenge utamaduni kwamba kuwa na vyama tofauti vya kisiasa na kuwa na maoni mbadala ndiyo demokrasia yenyewe na si uadui na haiwezekani kwa watu tofauti kufikiri na kutenda kwa namna inayofanana. Demokrasia inatutaka tuvumiliane na tuishi pamoja katika tofauti zetu na kwamba hakuna aliye bora au mwenye haki zaidi ya wengine. Ingawa demokrasia hutumia kanuni ya “wengi wape”, hutumia pia kanuni ya “wachache wasikilizwe” wakati wa kufanya uamuzi.
Uvumilivu wa kisiasa na maoni mbadala ni fursa ya ushindani chanya kwa siasa na kwa maendeleo ya nchi yetu. Utatuzi wa migogoro kwa njia ya majadiliano na kufikia muafaka wa pamoja kwa yale yanayolalamikiwa ni njia sahihi ya kukabiliana na matatizo yetu sugu. Ni dhahiri, tukifanya hivi tutakuwa tumeelewa maana ya kuwa au kufanya siasa safi kuliko kuendekeza chuki na uadui wa kisiasa ambao ni rahisi kuenea hata katika jamii na kuturudisha nyuma.
Uhuru wa maoni
Tunapojenga taifa linalozingatia utawala bora na uwajibikaji, tunakubali kufanya mambo yetu bila kuonewa au kumwonea mtu. Tufahamu kwamba, kila mtu ana haki ya kikatiba ya kutoa maoni yake hadharani, kujumuika na wengine, kupata au kutoa habari na kueleza fikira zake. Vyombo vya habari ni kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi kwa maana ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii.
Hivyo, wanasiasa, waandishi wa habari, wafanyakazi, wanafunzi, asasi za kiraia na wananchi kwa jumla wana haki ya kutoa maoni na kuonyesha hisia zao hadharani na kufikisha ujumbe wao kwa mamlaka husika kwa njia zinazokubalika kikatiba.
Juhudi za kupambana na kuzuia rushwa
Rushwa ni adui wa haki (kutoa au kupokea rushwa). Serikali ambayo lengo lake kuu ni ustawi wa wananchi na inayowajibika kwao haina budi kupambana na kuzuia rushwa katika vyombo vyake na taasisi zake zote na katika ngazi zote za utendaji. Rushwa inafanya huduma za jamii zitolewe kwa ubaguzi na kwa hiyo inarudisha nyuma maendeleo.
Hitimisho
Tukiwa na vyombo huru na imara vyenye mamlaka ya utendaji, utoaji haki kwa wakati na vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma tutakuwa na taasisi na mifumo imara za uendeshaji wa shughuli za serikali na nchi na kuleta maendeleo endelevu.
Kwa hiyo, ni muhimu kila mmoja wetu atimize wajibu wake kikamilifu na hasa serikali na vyombo vyake ionyeshe mfano mzuri ili iwe rahisi kwa wananchi pia kutimiza wajibu wao. Kiongozi yeyote wa umma afahamu cheo ni dhamana na afanye kazi kwa kujituma kama mtumishi wa wananchi na siyo kama bosi au anayetaka kutumikiwa na wananchi. Mabadiliko kuelekea Tanzania tunayoitaka yanawezekana!

Upvote
1