Utawala bora zama za awamu ya tano upo

Utawala bora zama za awamu ya tano upo

Ivan said

Member
Joined
Feb 14, 2021
Posts
83
Reaction score
107
Enzi zile unaenda ofisini kuonana na afisa elimu au mkurugenzi unakuta wabeba mafaili wanakushikiniza uwaambie kwanza unataka kumwambia nini unaetaka kumuona na bila kuwambia hivyo viranja/wabeba faili unapewa jibu kuwa bosi hayupo bila kujali umbali na gharama za nauli, vumbi ulilokunywa na msongo wa mawazo uliyonayo.

Zama za JPM ni tofauti kabisa, nafahamu kipeleka barua kwa Mkuu wa idara yeyote ni lazima ataijibu tena kwa wakati na asipoijibu napanda ngazi/mamlaka iliyo juu yake tena bila kikwazo. Nikitaka kuonana na Mkuu wa idara husika sikutani na vikwazo kama enzi zile za wabeba mafaili kutaka niwaambie hitaji langu ndipo waniruhusu kuonana na bosi wao.

Zama za JPM utawala bora unaonekana kwa vitendo.
 
Ni msimamizi Bora Ila ni mbovu kwenye uchumi .... Watanzania jipimeni wenyewe kama mnataka msimamizi Bora au mnataka uchumi Bora ..... Your choice
 
Utawala bora wa kutowapandisha wafanyakazi madaraja kwa miaka sita ili kununua ndege! Kuwaumiza wapinzani! Kuendesha nchi kwa vitisho! Kuwaendekeza wanafiki na waimba mapambio kama wewe mtoa mada!! Ok.
 
Msimamizi bora wakati ni mwizi na fisadi? Unakuwaje msimamizi bora kwa kudharau katiba, Bunge, mahakama na raia? Unakuwaje msimamizi bora kwa kukwapua hazina 2.7 trillions kisha unazuia uchunguzi huru? Unakuwaje msimamizi bora kwa KUKURUPUKA kununua ndege kwa 3 trillions bila idhini ya Bunge kisha unamzuia CAG akague manunuzi husika na kuikagua ATCL ili kuficha hasara kubwa ndani ya ATCL? 😳😳😳


Ni msimamizi Bora Ila ni mbovu kwenye uchumi .... Watanzania jipimeni wenyewe kama mnataka msimamizi Bora au mnataka uchumi Bora ..... Your choice
 
Unaweza kukuta huyu yupo kwao anasubiri chakula.
 
Hizi ni propaganda za kijinga,hakuna kilichobadilika katika uendeshaji wa shughuli za serekali.

Tena kipindi hiki hali inazidi kuwa mbaya kuliko awamu zote tangu tupate uhuru.
 
Back
Top Bottom