SoC03 Utawala dhaifu katika Taifa

SoC03 Utawala dhaifu katika Taifa

Stories of Change - 2023 Competition

kadamlo

Member
Joined
Jul 15, 2023
Posts
8
Reaction score
16

Utawala dhaifu​

Utawala dhaifu ni utawala ambao haujajikita katika njia moja ya kiutawala ambayo ni imara na ya haki, ndani ya utawala kuna itikadi na misimamo tofauti,ndani ya serikali hakuna kundi la kudumu la waamuzi,ukoloni mambo leo una watumia baadhi ya watawala,utawala usio jitegemea kiuchimi na kisiasa.

SABABU ZA UTAWALA KUWA DHAIFU​

Utawala dhaifu hupimwa jinsi taasisi za umma zinavyoendesha shuguri za umma kwa kukosa kuhakikisha upatikanaji wa haki za binadamu kwa sababu zifuatazo.

1.itikadi​

Itikadi za kidini au kisiasa hutengeneza imani ya kundi furani la serikali au taasisi ya umma kulikosesha haki kundi furani la raia kwasababu ya dini zao au itikadi zao kisiasa.

Utawala huu unakuwa dhaifu hasa ikiwanyima haki watu wa itikadi furani za dini na wakati nchi sio ya kidini au kuwanyima haki watu wenye itikadi furani ya kisiasa wakati nchi ni ya kidemokrasia na haina itikadi moja ya kitaifa.

2.ujinga​

ujinga ni hali ya mtu kutojua jambo ambalo anastahili kulijua kutokana na nafasi yake katika jamii. haijalishi elimu ya mtu ila akikosa kuyajua yale yanayomuhusu zaidi mtu huyo ni mjinga.

utawala ukiwa na viongozi wengi wenye ujinga unaosababishwa na mazingira,uzembe au kibuli cha madaraka ambapo ujinga wao unaathiri mchakato wa kiutawala kutokana na upofu wao wa fikra na kupelekea ukosefu wa haki za binadamu au umasikini,basi utawala huo ni dhaifu sana kwasababu wajinga hawapendi changamoto.

3.demokrasia​

Uongozi ndani ya chama tawala kwa nchi za kidemokrasia ni hajira isiyo ya kudumu,kiongozi hutumia nguvu kubwa sana kulinda cheo chake kwa jasho na damu ili aendelee kuwepo pale alipo,

Kiongozi huyu huwa ni kivuli kwa watu waliomzidi cheo lakini pia yeye na kundi lake la watawala hutumia nguvu kubwa sana kulinda chama kisitoke madarakani kwa kutumia akili kubwa kuliko akili ambayo walitakiwa kuitumia ili kutengeneza njia za kiuchumi au kiutawala bora, viongozi hawa wa vyama humpa nafasi Yule anaye jipendekeza kwa chama tawala na kunyima haki za watu wengine na kupelekea utawala kuwa dhaifu sana na usio na mabadiliko.

4.umasikini​

Umasikini hufanya utawala kuwa dhaifu kwasababu ya serikali kutoweza kutekeleza miradi ya kiserikali na kupelekea wananchi kukosa imani na serikali yao,hali hii ya serikali kuwadanganya wananchi kupitia sera hutokana na utofauti kati ya mahitaji ya wananchi na uharisia wa nchi kiuchumi, hali hii upelekea wenye nguvu kupata huduma na wasio na nguvu kukosa haki zao huku serikali ikiwa haina nguvu ya kusimamia haki kwasababu haijatekeleza maitaji kikamilifu kwa taasisi zake,

lakini pia Tatizo hili ufanya serikali kuingia katika madeni makubwa sana ili kupambania uhai na uhuru wa serikali na raia wake lakini mwisho inakosa nguvu ya kulipa madeni na kupelekea kuwa taifa dhaifu mbele ya mataifa mengine kwa kukosa misimamo.



Kwanini binadamu wanaitaji utawala?​

Binadamu wana madeni mawili ya asili ambayo ndio yanayofanya waitaji utawala bora na madeni hayo ni kama yafuatayo.

1.deni la uhai​

Deni la uhai ni deni linalomfanya binadamu ahangaike kila siku ili asipoteze uhai wake na deni hilo ni kula ,kujilinda,kutibiwa n.k, Binadamu huwa mtawala kwa familia yake na kuwapa chakula,kuwalinda na kuwatibia pale wanapougua.

2.deni la uhuru​

Deni la uhuru ni deni linalomfanya binadamu ahangaike ili aepukane na ghasia na deni ilo ni kuvaa,kulala,uhuru wa kuamua,elimu.

binadamu huchukua jukumu la kuiondolea ghasia familia yake kwa kuipa mavazi,malazi na kuilinda

Kumbuka​

Madeni haya mawili anadaiwa binadamu mmoja mmoja na serikali pia,

-Deni la uhai kwa serikali ni kupambana ili nchi iwe na amani na serikali iendelee kupata kodi na kuwa hai kwa kuilinda vinavyowakilisha taifa.

-Deni la uhuru kwa serikali ni kupambana ili serikali isiingiliwe kimaamuzi na isitawaliwe na serikali zingine.

NJIA ZA KUONDOA UTAWALA DHAIFU KATIKA TAIFA​

1.utawala wa hesabu​

Utawala wa hesabu ni utawala ambao viongozi na raia wake wanatumia akili nyingi katika kupanga mambo ili yalete matokeo makubwa kiuchumi,kisiasa na kiteknolojia .

Kinachoitajika zaidi katika taifa ili utawala usiwe dhaifu ni usimamizi bora wa taasisi za umma na kuwa na nguvu.

nguvu inapatikana kwa fedha na fedha izo zipo mataifa mengine na kuzipata fedha izo ni kwa njia ya kuuza bidhaa au huduma.

watawala wa hesabu hukuza njia wanazozitumia raia wake kupata mapato madogomadogo ya ndani na kuzifanya ziwe njia kubwa za maingizo ya fedha kimataifa,lakini pia hutengeneza mfumo wa elimu unao wafanya watu wao kutamani nguvu kubwa na kujitegemea ili wajilinde na sio kulaumu wengine.

mtawala wa hesabu huwakuza na kuwatangaza wana sanaa kama vile waandishi wa vitabu,waigizaji,waimbaji,wachoraji,wachongaji vinyago,n.k

Nchi kama india,marekani,korea ya kusini na zingine,huingiza fedha nyingi kupitia filamu, lakini pia hutumia vipaji vya watu kuongeza uchumi wa taifa na teknolojia.

lakini katika bidhaa gunduzi kama vile dawa za asili,watawala wa hesabu hufanya utafiti zaidi hasa ikiwa dawa iyo ni yakipekee na kuifanya kuwa bidhaa yenye kuweza kuuzika duniani kote.

Watawala hawa huitwa watawala wa hesabu kwasababu wanatumia sera ngumu sana na za akili kubwa kuleta matokeo makubwa kiuchumi na kisiasa na wakati mwingine huthubutu kutengeneza sera za kujitoa kwenye ukoloni mambo leo bila wakoloni kujua.

kumbuka​

lasilimali ya kwanza na yenye nguvu katika taifa ni akili za watu na vipaji vyao.

2. kuunda itikadi ya kitaifa​

Ikiwa nchi haina itikadi moja pia haiendani na ujamaa wala ubepali kutokana na watu wake au itikadi izo kupitwa na wakati ni lazima kuiandika itikadi ya kitaifa nyingine ambayo itaangalia jamii ilivyo kwa wakati huo na itatumika kwa miaka kadhaa na kulifanya taifa kuwa na nguvu, itikadi hii ni mkusanyiko wa sera za kiuchumi na kisiasa ambazo zitatumika zote kwa wakati mmoja ili nchi kujitengenezea uchumi mkubwa kwa miaka michache.

wasichojua watu wengi ni kwamba,maisha yana muda wa kupigana vita na muda wa kulinda kilichopiganiwa vita ivyo ikiwa nchi ni masikini ni lazima ipigane vita ili ipate uchumi wa kuulinda na vita iyo ni itikadi ya kitaifa.

Itikadi moja italeta hajira kwa kila raia asie na ajira ndani ya miaka mingi sana na nchi itazalisha uzalishaji mara dufu huku serikali ikipambana kutengeneza mikataba ya kibiashara na mataifa mengine kama ilivyowahi kufanyika urusi,china,ulaya magharibi na nchi zingine zilizotengeneza itikadi zao.

Kila taifa lenye nguvu sana duniani kote liliwahi kuwa taifa masikini na kitu pekee kilicholipa nguvu taifa ilo ni itikadi,itikadi izo ni kama vile quran,biblia,ubepali na ujamaa.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom