UTAWALA kimajimbo una faida/madhara gani. Tuchambue ili watu waelewe

Ibrah wa kiwira

Senior Member
Joined
May 17, 2023
Posts
179
Reaction score
167
Jamani, mimi binafsi naanza kuafiki idea ya chadema ya utawala wa kimajimbo.

Inaweza kuforce maendeleo Kwa kasi sana kulingana na ukubwa wa inchi yetu.

Lakini nimekutana na pingamizi, hacha wanaccm hawaafikiani na utawala huu.

Please tujadili faida na madhara yake humu.

NAWASILISHA.
 
Nakataa wazo hili, wachaga ni binafsi mno watataka kaskazini yote iwe yao
Katika shughuri zao watainufaisha serikari kuu, ubnafsi utakua katika mambo yasio ya serikari. Inchi yetu ni kubwa. Muundo wa utawala tulionao haufiki kwenye maeneo husika.

Organisms wanakitu kinaitwa cell differentiation, hii inasaidia mwili kufanya shughuri zote Kwa ufanisi na Kwa wakati,
 
Jamani, mimi binafsi naanza kuafiki idea ya chadema ya utawala wa kimajimbo.
Inaweza kuforce maendeleo Kwa kasi sana kulingana na ukubwa wa inchi yetu.
Lakini nimekutana na pingamizi, hacha wanaccm hawaafikiani na utawala huu.
Please tujadili faida na madhara yake humu, NAWASILISHA
Kwa kifupi sana, utawala wa majimbo unafanya kazi katika muundo huu. Nchi inagawanywa katika vipande kadhaa vya utawala wa ndani (utawala wa ndani=Wananchi wenyewe kupanga maendeleo+kusimamia rasimali zao).
 
Je

Je Kuna mambo yoyote ya kijamii ambayo yanakua ya pamoja kama Taifa? Je kama yapo kama yapo?

Inchi nyingi zenye idad kubwa ya watu hutumia huo mfumo, huenda una uzuri sana kuliko hasara
 
Jamani, mimi binafsi naanza kuafiki idea ya chadema ya utawala wa kimajimbo.
Wewe ni CHADEMA?? Umeafiki kivipi....yaani umetumia ulinganishi upi
Inaweza kuforce maendeleo Kwa kasi sana kulingana na ukubwa wa inchi yetu.
ikilinganishwa na wapi au kwa nchi gani kwa kulinganisha. ikilinganishwa na (kwa), Utawala wa nchi gani ambayo imelazimisha maendeleo au kuleta maendeleo kwa watu wake ikilinganishwa na, ikilinganishwa na, kinyume na, kinyume na, wapi?
Je, haya ni matamanio yako au, ni matakwa ya Mbowe?

Lakini nimekutana na pingamizi, hacha wanaccm hawaafikiani na utawala huu.
Unasingizia CCM hapa! Kuna wana CHADEMA wengi wasioafiki na Utawala huu.....

Please tujadili faida na madhara yake humu, NAWASILISHA
Ibrah, Umewasilisha kwa kiupendeleo, kwa hivyo ufunguke kupingwa kwa mtindo huo huo

Isitoshe haujaonyesha hayo "maendeleo" yatakuwa "forced" vipi.

Kwa kuwa naelewa maendeleo huletwa na watu, huoni itakuwa ni Udikteta kuja ku "Force" maendeleo? kwa kuwalazimisha kuafiki utawala huo? Yaani kwa kuwapigia kura CHADEMA?
 
Wewe ni CHADEMA?? Umeafiki kivipi....yaani umetumia ulinganishi upi

ikilinganishwa na wapi au kwa nchi gani kwa kulinganisha. ikilinganishwa na (kwa), Utawala wa nchi gani ambayo imelazimisha maendeleo au kuleta maendeleo kwa watu wake ikilinganishwa na, ikilinganishwa na, kinyume na, kinyume na, wapi?
Je, haya ni matamanio yako au, ni matakwa ya Mbowe?

Unasingizia CCM hapa! Kuna wana CHADEMA wengi wasioafiki na Utawala huu.....

Ibrah, Umewasilisha kwa kiupendeleo, kwa hivyo ufunguke kupingwa kwa mtindo huo huo

Isitoshe haujaonyesha hayo "maendeleo" yatakuwa "forced" vipi.

Kwa kuwa naelewa maendeleo huletwa na watu, huoni itakuwa ni Udikteta kuja ku "Force" maendeleo? kwa kuwalazimisha kuafiki utawala huo? Yaani kwa kuwapigia kura CHADEMA?
Ni kweli, maendeleo huletwa na watu, lakn watu Hawa lazima wawe organized na wawe ruled na viongozi wazalendo. Viongozi wa MAJIMBO watakua na uchungu na Jimbo lao, zen viongoji watalazimika wawe na vision na mikakati, swala uchaguz wenye sifa za haki na uwazi utakuepo Kwa asilimia walau za kuridhisha.

Inchi yetu ni kubwa, sio rahisi Kwa serikari kuaford mahitaji ya kila maeneo
 
Faida[emoji116]
[emoji117] Kukua kwa miji mipya,
[emoji117] Maendeleo kukua ktk miji na majiji ambayo yanaongoza kuchangia pato la taifa ambalo hapo kabla majiji hayo yalikuwa yakinyonywa mapato ya maeneo hayo kupelekwa kufanya maendeleo sehemu zingine.

Hasara[emoji116]
Kuibuka kwa ukabila, mitengano na chuki za kisiasa baina ya kanda fulani na kanda fulani pia ubaguzi wa kikanda na kibabila.

Kiuhalisia Mfumo wa majimbo kwa nchi za Afrika haufai, maana muafrika ili apate maendeleo ni lazima aishi ktk utamaduni wa Umoja na mshikamano tofauti na hizo nchi mnazoforce tufanane nao, mfumo wa Majimbo HAUFAI ni bora itafutwe namna iliyo bora.
 
Ni kweli, maendeleo huletwa na watu, lakn watu Hawa lazima wawe organized na wawe ruled na viongozi wazalendo. Viongozi wa MAJIMBO watakua na uchungu na Jimbo lao, zen viongoj watalazimika wawe na vision na mikakati, swala uchaguz wenye sifa za haki na uwazi utakuepo Kwa asilimia walau za kuridhisha.
Inchi yetu ni kubwa, sio rahis Kwa serikari kuaford mahitaji ya kila maeneo
Umefanya ulinganishi na wapi? Manake hili sio suala dogo ibrah, kama inavyoonekana, unavyolichukulia.

Kwa hayo majibu yako, unasema watu hawako organised......hiyo siyo kweli. Tanzania tunaanza kuwa organised kutoka nyumba kumikumi, haya nitajie Nchi yenye majimbo iliyokuwa organised kutoka nyumba kumikumi na kuridhiwa na Serikali?

Narudia, umefanya ulinganishi na wapi? ili niweze kujadili hizo faida za "forced' Development kama ulivyowasilisha.
 
Kuwa organized Kwa upana wa kijimbo,
Inchi nyingi za afrika zenye idad kubwa ya watu wanatumia mfumo huu. Mfn Nigeria, South Africa, Egypt, nk. Na inch Zina maendeleo makubwa,
Natural resources husika zitalindwa na wenye Jimbo, na zitawanufaisha wenyewe Kwa namna watakavotaka. Na shughuri zinazofanyika Jimbo husika economically zitakua own na wahusika. Wao ndio watapanga tuuze sh ngapi, tumuuzie nani.

Ujenzi wa miundo mbinu ya afya, elimu, usafiri na kazi

Itajengwa Kwa budget ya Jimbo husika, so lazma msubiri mama aseme neno. Na mengne mengi nayaona
 
Mfumo wa majimbo kwa nchi zetu ni kutafuta kuigawanya nchi na kupelekea upande mmoja utake kujitoa na kusimama wenyewe. Wengi wamejawa ulafi wa madaraka hapa TZ mtu akiona ana serikali yake ya jimbo na jeshi lake anaweza kukinukisha muda wowote yawe ya Ethiopia
 
Faida[emoji116]
[emoji117] Kukua kwa miji mipya,
[emoji117] Maendeleo kukua ktk miji na majiji ambayo yanaongoza kuchangia pato la taifa ambalo hapo kabla majiji hayo yalikuwa yakinyonywa mapato ya maeneo hayo kupelekwa kufanya maendeleo sehemu zingine.

Hasara[emoji116]
Kuibuka kwa ukabila, mitengano na chuki za kisiasa baina ya kanda fulani na kanda fulani pia ubaguzi wa kikanda na kibabila.

Kiuhalisia Mfumo wa majimbo kwa nchi za Afrika haufai, maana muafrika ili apate maendeleo ni lazima aishi ktk utamaduni wa Umoja na mshikamano tofauti na hizo nchi mnazoforce tufanane nao, mfumo wa Majimbo HAUFAI ni bora itafutwe namna iliyo bora.
Kwa uchambuzi wako, hasara zinaweza kudhibitika. Japo ukabila ni jambo ambalo halitakua na kasi mno, tumeoana, wengine wamehamia, na wengine watahama Kutoka eneo moja kwenda lingine,
 
Mfumo wa majimbo kwa nchi zetu ni kutafuta kuigawanya nchi na kupelekea upande mmoja utake kujitoa na kusimama wenyewe. Wengi wamejawa ulafi wa madaraka hapa TZ mtu akiona ana serikali yake ya jimbo na jeshi lake anaweza kukinukisha muda wowote yawe ya Ethiopia
Jimbo litaweka ukomo wa kijeshi, lisije kukua kuliko jeshi la inchi. Na Ethiopia uliyosema, sio jeshi la Jimbo ndo limeleta shida, ni waasi waliotoka sehemu mbalimbali
 
Mzee huu mfumo una faida sana ila kwa Afrika hii hautufai kabisa, najua wanasiasa wanaupigia chapuo sababu utaongeza nafasi nyingi sana za kuchaguliwa lakini gharana kubwa ya uendeshaji itakuwa mara mbili yake. Nadhani unajua wazi wale jamaa miposho yao na mahitaji yao mengine kupitia kodi, fikiria sasa wakizidi zaidi kila jimbo wapo. Ni matumizi kiasi gani?

Achilia mbali hayo machafuko kupitia ubinafsi ambao umewajaa wengi sana kwa kutaka kuimarisha ngome zao za kisiasa na kutaka kuwa na madaraka makubwa. Nakwambia ipo siku utakuja kusikia serikali ya jimbo Morogoro imejitangazia uhuru na inataka itambulike kama nchi
 
Faida[emoji116]
[emoji117] Kukua kwa miji mipya,
[emoji117] Maendeleo kukua ktk miji na majiji ambayo yanaongoza kuchangia pato la taifa ambalo hapo kabla majiji hayo yalikuwa yakinyonywa mapato ya maeneo hayo kupelekwa kufanya maendeleo sehemu zingine.

Hasara[emoji116]
Kuibuka kwa ukabila, mitengano na chuki za kisiasa baina ya kanda fulani na kanda fulani pia ubaguzi wa kikanda na kibabila.

Kiuhalisia Mfumo wa majimbo kwa nchi za Afrika haufai, maana muafrika ili apate maendeleo ni lazima aishi ktk utamaduni wa Umoja na mshikamano tofauti na hizo nchi mnazoforce tufanane nao, mfumo wa Majimbo HAUFAI ni bora itafutwe namna iliyo bora.
Sauzi Kuna ukabila mkuu? Mbona wanatumia mfumo wa majimbo na maendeleo yapo juu!!
 
najua wanasiasa wanaupigia chapuo sababu utaongeza nafasi nyingi sana za kuchaguliwa lakini gharana kubwa ya uendeshaji itakuwa mara mbili yake. Nadhani unajua wazi wale jamaa miposho yao na mahitaji yao mengine kupitia kodi, fikiria sasa wakizidi zaidi kila jimbo wapo. Ni matumizi kiasi gani?
Sio kweli, serikali za majimbo zitapunguza namba ya wabunge kutoka 300+ Hadi 75 pekee.

Kumbuka sahivi Kuna madiwani pia Sasa kwa serikali za majimbo Hawa madiwani ndio wataunda bunge la Jimbo hivyo basi Ina maana nafasi za uongozi zitapunguzwa coz DC, RC na vyeo ambatanishi vitakufa.

Kimsingi ni kwamba halmashauri zilizopo tayari zitaongezewa tu mamlaka ya kujiendesha kwa uhuru. Mbona sijawahi sikia halmashauri zimetangaza kujitenga licha ya kwamba huwa zinakua za eneo Hilo Hilo ila Leo serikali ya Jimbo ndio itajitenga? How?

Kwahiyo sio kweli kwamba serikali ya Jimbo inaongeza gharama au italeta machafuko.
 
Hivi unajua kila jimbo nalo linakuwa na bunge lake dogo.
 
Hatuhitaji majimbo. Sisi tuweke mabaraza ya Maendeleo kila manispaa na tuyape nguvu ya kuajiri na kufukuza wakurugenzi Tu na watu wao. The rest will be history.
 
Kusiwepo na Jimbo la ubunge bila manispaa. ...
Na wakurugenzi wa manispaa au Halmashauri waombe kazi huko huko Kwa Baraza la Halmashauri ambao wajumbe ni madiwani na wenyeviti WA serikali ya mtaa...
 
Back
Top Bottom