Umefanya ulinganishi na wapi? Manake hili sio suala dogo ibrah, kama inavyoonekana, unavyolichukulia.
Kwa hayo majibu yako, unasema watu hawako organised......hiyo siyo kweli. Tanzania tunaanza kuwa organised kutoka nyumba kumikumi, haya nitajie Nchi yenye majimbo iliyokuwa organised kutoka nyumba kumikumi na kuridhiwa na Serikali?
Narudia, umefanya ulinganishi na wapi? ili niweze kujadili hizo faida za "forced' Development kama ulivyowasilisha.
A: Katika mfumo huu, kutakuwa na;
1. Serikali kuu (Central Government).
2. Serikali za majimbo (Profince/States Government)..
===Serikali za Majimbo zitakuwa na mamlaka kamili katika baadhi ya mambo kwa kadiri itakavyokubaliwa na kuanishwa na katiba..
===Muhimu ni kuwa, serikali za majimbo zinapaswa kuachwa na kupewa mamlaka kamili ya kikatiba kujiamulia na kujisimamia zenyewe juu ya shughuli za maendeleo yao na kuweka/kujichagulia viongozi wao..
===================================
✓ On the other hand, ukitazama kwa makini ni kuwa, sera ya utawala wa majimbo ya CHADEMA haina tofauti na sera ya utawala ya CCM inayotumika sasa chini ya mfumo wa
serikali za mitaa (local governments).
✓ Na dhana ya serikali za mitaa maana yake ni kuwa na serikali za mitaa zenye mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yao kwa 100%
✓ Kasoro kubwa iliyopo kwa mfumo huu uliopo sasa chini ya CCM ni kuwa, serikali hizi za mitaa chini ya mwavuli wa vijiji/mtaa, Kata, Tarafa, Wilaya na Mkoa ni kukosa mamlaka ya kujiamulia mambo ya maendeleo yao na namna ya kujichagulia viongozi wao
===================================
✓ Ziko nchi nyingi zinazotumia mfumo huu wa utawala Afrika na duniani kote kwingine...
✓ Kwa Afrika ziko nchi kama Kenya, Africa Kusini, Nigeria, Swaziland, Lesotho, Namibia nk nk..
✓ Huko ktk Dunia nyingine ziko nchi kama Marekani, Ubelgiji, Uingreza, China, Japan nk nk