Utawala wa Awamu ya 5 kulikuwa na kampeni ya wazi ya kutaka aliyekuwepo aongoze milele, Sababu hasa ya kampeni hii ilikuwa nini?

Karibu sana mkuu , nadhani ulichelewa kidogo , hizi mada si za Chadema ni mada zangu kwa ajili ya mwezi wa 3 ambao ni mwezi wa Mungu , kutokana na " Kwaresma na Ramadhan " kukutana , lengo langu ni kuhakikisha haya mambo hayajirudii tena
Ukijivua u-CHADEMA nitakuelewa; lakini sijakusoma ukieleza kuwa ulisha chukua hatua hiyo.
Inatosha, hili liachie hapa.
 
Ukijivua u-CHADEMA nitakuelewa; lakini sijakusoma ukieleza kuwa ulisha chukua hatua hiyo.
Inatosha, hili liachie hapa.
Maana yake ni kwamba nyuzi 20 ndio nilizoziandaa kwa ajili ya kuelezea habari utawala wa awamu ya 5 , huu uliouona wewe ni wa 5 , kila siku nadondosha mmoja , ni katika ule mpango wa NEVER AND NEVER AGAIN , Leo kuna mwingine uko hewani na kuna nyingine 14 zishaandaliwa .

Mkianza kutuzuia kuandika uchafu wa awamu ya 5 angalau kwa mwezi huu mtakuwa hamtutendei haki , Shetani katenda uovu kwa miaka mingi sana iliyopita lakini bado mpaka leo anasemwa misikitini na makanisani , tena kwa kurudiwa rudiwa
 
Ndugu mpandisha uzi,"utasema kweli daima"ila ukiwa upande ganiπŸ€”
 
Alikuwa anataka amwige mwenyekiti
 
Tena kwa mujibu wa Gen.Mabeyo, mahasidi hao walitaka kumwongezea muda hata akiwa ameshavuta tayari, nashangaa inakuwaje Majaliwa ni Waziri Mkuu hadi leo
 
Labda Mkapa na Mwinyi walinga mkono.
JK sidhani.
Lakini watu hutamani kiongozi fulani aendelee kutokana na utendaji wake unavyowagusa.
Mifano ni mingi
China ()Xi Jinping) Ujerumani (Angela merkel) Chadema (Freeman Mbowe) n.k
Chadema Freeman Mbowe πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mkianza kutuzuia kuandika uchafu wa awamu ya 5 angalau kwa mwezi huu mtakuwa hamtutendei haki , Shetani katenda uovu kwa miaka mingi sana iliyopita lakini bado mpaka leo anasemwa misikitini na makanisani , tena kwa kurudiwa rudiwa
Nilisema" inatosha" na nilitaka kuliacha hili lilale, lakini naona kwa maksudi kabisa unaamua kunivunjia heshima kwa mistari yako hii niliyo nukuu hapo juu, na hasa kipande cha mstari wa kwanza.
Kwa hiyo nami sasa niseme Erythro katekwa kwenye kundi la Mbowe? Hili ndilo tatizo la siasa za nchi hii; ni mara chache sana kukutana na mtu mwenye msimamo thabiti juu ya lolote lile lihusulo maslahi ya wananchi wetu. Kila mtu ana bei inayomtosha (na siyo lazima iwe bei ya pesa au mali).
Sitakujibu tena kwenye hili.

Nimekumbuka kitu, hasa kuhusu "shetani". Huo mstari wako wa "kanisani na misikitini" , na kwingineko, jaribu kuupa tafakuri zaidi. Kuna jambo unalokosa kulielewa vizuri.
Na kumbuka, shetani huja katika maumbo mabalimbali. Usishangae kuona kuna shetani wa kutisha sasa hivi kuliko uliyewahi kumshuhudia maishani mwako. Kumbuka, sina wajibu wa kumtetea shetani wa aina yoyote ile.
 
Tatizo letu ni kwamba siasa na uongozi tumefanya ni kama ngazi ya kuupata utajiri sio kuwa hizo ni kazi za wito tu !

Ndio maana utaona watu wengi wanataka uongozi wa juu ili tu wakajineemeshe !!
Nchi changa na zinazoitwa masikini zinatakiwa kwa sasa zitawaliwe na mtu mmoja kwa miaka mingi ili ziweze kupata maendeleo ya kweli kabisa !

Muhimu ni ni kwamba huyo mtu atakayetawala kwa muda mrefu awe ni muadilifu kweli kweli na awe anaogopewa pia na wateule wake kama alivyokuwa akiogopewa yule jamaa !!

Hii system ya demokrasia ya kubadili badili viongozi kila baada ya miaka mitano au kumi inazifaa nchi zilizokwisha kuendelea kwa miaka mingi na ina mifumo imara kabisa ya kuendesha Nchi !!

Kwetu sisi miaka kumi au mitano ya kuendesha Nchi ni michache sana kuweza kuleta maendeleo !

Sana sana watu watakuwa wakipiga na kujiandaa na uchaguzi mwingine ujao badala ya kuelekeza nguvu zote kwenye maendeleo ya Nchi !

Sina uhakika kama yule Mwamba alikuwa alikuwa ana sifa hizo ila Angalau alionyesha kwamba mtu mkubwa pale juu akiamua Nchi iendelee kwa haraka ni kitu kinawezekana kabisa !
Sauti ya kimamlaka ni muhimu katika hizi Nchi zetu masikini !
Japo ukiwa hivyo utaitwa Dikiteta !
Demokrasia iliyoletwa na Wazungu lengo lao ni moja tu ni kuwacontrol wale viongozi waliopo madarakani ili wafuate wanavyotaka wao katika kukwapua rasilmali za Nchi kwa kiini macho cha uwekezaji !!
Madini yote kwaheri ! Gesi yote kwaheri !
Tafakari πŸ™πŸ™πŸ™ !
 
Yani sugu katika kitu ambacho kinakuuma ni kushindwa uchaguzi 2020 na Dr Tulia wakati kiuhalisia hukuwahi kuifanyia chochote cha maana Mbeya.

Punguza chuki kwa JPM haitakusaidia kitu sana sana utapata mikosi tu na bungeni urudi ng'o hilo kaa ulijue
 
WANUFAIKA NA MAGUFULI WALITAKA WAENDELEE KUNUFAIKA NA MAGUFULI MWENYEWE ALIPOGUNDUA KUWA WATANZANIA NI WAJINGA AKATAMAANI ATAWALE MILELE
 
Mbowe atuachie na sie kidogo wanachama wengine tuongoze.
 
Katiba ni mali ya wananchi, wakiona uongozi mzuri ni kubadili katiba chapchap na kumuongezea mda. Angalia Rwanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…