Mr RoundAbout
Member
- Oct 6, 2023
- 74
- 89
Kwa Hali inavyoenda Sasa ni Bora magufuli angetawala miaka 20 angetuacha kama ulaya,,,,mama kapyaya na washauri wake wengi hawana sifa za kiongozi ni wapambe tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We ni mtu dikiteta....ishia huko huko kwenye familia yako.Kwa Hali inavyoenda Sasa ni Bora magufuli angetawala miaka 20 angetuacha kama ulaya,,,,mama kapyaya na washauri wake wengi hawana sifa za kiongozi ni wapambe tu
Alimradi mwanae anafyonza kuku kwa mrija na alisaidiwa kukalia kiti kule mzee wa watu angekataaje?Siasa za Tanzania kwa kiasi kikubwa ni za kuangalia watu, si za kuangalia sera.
Nilisikitika sana kuona Rais Ali Hassan Mwinyi (RIP) naye kashadadia ujinga huu.
Yeah ni kweli MkuuWapambe walikuwa wanaangalia ulaji tu. Muswada ungepelekwa bungeni nani angepinga chini ya bunge la chama kimoja? Inahitaji akili ya kawaida tu kujua kwamba hata magufuli tayari alikuwa ameridhia kuendelea kukalia kiti kwa kisingizio cha kukamilisha miradi.
Unadhani kisheku angeweka pingamizi? Unadhani gwajima angeweka pingamizi? Kabudi? Mhagama? Simbachamwene? Nani angepinga?Yeah ni kweli Mkuu
Wapambe walikuwa tayari Mwamba aendelee hata miaka 20 zaidi 😅
Hatari sana Mkuu 😅🙌Unadhani kisheku angeweka pingamizi? Unadhani gwajima angeweka pingamizi? Kabudi? Mhagama? Simbachamwene? Nani angepinga?
😄we kwa mwendo wa yule bwana naona shughuli zako za pori ziliongezeka muda wa kukaa pori usijedakishwa uhujumu uchumi bure.
Wapambe hawakuelewa hiloMtu ataongozaje milele? That’s not even humanly possible.
Si umeona mwenezi alivyotajirikaKuna wajanja waliokuwa wananufaika na utawala ule wakawa wanawatumia wapiga mbinja inawezekana hata wapiga mbinja hawakujua kama wanatumiwa.
Mfano wale waliokuwa wanachukua fedha za watu kwa nguvu.
Mkuu,Alimradi mwanae anafyonza kuku kwa mrija na alisaidiwa kukalia kiti kule mzee wa watu angekataaje?
Nakiri kabisa kwa sababu ni mwendelwzo wa kulinda circle ya ulaji kwa vizazi vyao vya mbele.Mkuu,
Unafikiri kweli kabisa Mwinyi kawa motivated na ulaji, na si kwamba hajaamini kikweli kabisa bila kujali ulaji kwamba Magufuli angefaa kukaa madarakani beyond term limits?
Unahakikishaje Mwinyi alikuwa motivated na career ya mwanawe na si kuamini kwa ukweli kabisa kifalsafa kwamba Magufuli ni mwamba anayefaa kuongezewa muda?
Hujahakikisha, hujathibitisha, umeweka conspiracy theory.Nakiri kabisa kwa sababu ni mwendelwzo wa kulinda circle ya ulaji kwa vizazi vyao vya mbele.
how to hug a porcupine
View attachment 2938427
Hoja iko wapi na mwenyewe alishasema hataki kuongeza hata dk moja madarakani sio kama mbowe ukizungumzia nafasi yake kesho unasalimia kuzimu!Nje ya mada , inasikitisha sana kwa vijana wa ccm kukosa hoja kabisa hapa Jf kiasi cha kutia aibu .
yaani aongoze milele kama chairman Mbowe au 🐒Tunaendelea na nyuzi zetu za mwezi wa 3, ambao ni mwezi wa Mungu.
Ni wazi kila mwananchi anafahamu kuhusu kampeni za wazi kabisa za kutaka Rais wa awamu ya 5 Dkt John Magufuli aongezewe muda wa utawala wake kinyume kabisa cha Katiba ya Tanzania, yaani baada ya kumaliza utawala wake wa miaka 10, bado aongezewe miaka mingine isiyo na idadi.
Kampeni hii kabambe iliongozwa na kundi lisilo rasmi lililopachichwa jina la "Sukuma gang" na baadaye kuanza kuungwa Mkono hadharani na baadhi ya watu , na hatimaye likatua bungeni likiletwa na mbunge wa ccm Jimbo la Nkasi (zipo taarifa kwamba nyuma yake kulikuwa na kundi kubwa), Huku hoja yake ikiungwa mkono na Spika wa Bunge hilo Job Ndugai , na kwamba inasubiriwa muda ufike lipelekwe bungeni ili lijadiliwe na Katiba ya Nchi ibadilishwe.
View attachment 2938286
Hata baada ya Jambo hilo kupoa kidogo likaibuliwa tena na Mbunge wa Bahi Juma Nkamia , akisisitiza umuhimu wa kumuongezea John Magufuli muda wa uongozi , huku akisisitiza kwamba muhula wa Urais uwe miaka 7 badala ya mitano iliyowekwa kwenye Katiba ya Nchi .
Wale wote waliopinga jambo hili walionekana Wasaliti na walishughulikiwa chini kwa chini na Wateule wa Rais kuanzia kwenye chama hadi serikalini , huku Wateuliwa wengi wakichekelea na kuvimba kwa kiburi wakijua watakuwa wateule milele (Hapa ndipo ilipoanzia sumu aliyolishwa Mangula)
Ushahidi wa wapinga milele kushughulikiwa ulikuja kuthibitishwa na Juma Nkamia mwenyewe , alipokiri hadharani kwamba Alilazimika kutamka kwamba Magufuli aongezewe muda ili kunusuru uanachama wake ndani ya ccm , kwamba kulikuwa na mpango wa kumvua uanachama , na kwa vile mkubwa alifurahishwa na kauli ya Nkamia ya kumuongezea muda , Nkamia hakutimuliwa tena .
View attachment 2938287
Wakati haya yakiendelea , Viongozi karibu wote wastaafu walikuwepo huku wakinyamaza kimya as if hakuna uchafu unaopangwa , Wakuu wa vyombo vya dola wakiwa kimya ikiwa ni ishara ya kuunga mkono uharamia huo .
Sasa Swali letu ni hili , Waliokuwa wanafanya Kampeni hiyo haramu walichagizwa na nini hasa , Je ni Utendaji bora wa Magufuli na kwamba hakuna Mwanaccm mwingine angeweza kutenda kama Yeye , ama walichagizwa na Uroho wa madaraka ili waendelee kula miaka yote baada ya Rafiki yao kuwa madarakani milele ?
NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO