Utawala wa JPM ulitengeneza mabilionea wa kichina, Uturuki na waarabu, ,Nyerere, Mwinyi Mkapa na JK walitengeneza matajiri wazawa

Hata paschal mayala kampuni yake ya PR alinyanganywa tenda baada au kabla ya lile swali la ikulu
 
Mabilionea wa JPM ni Makonda na Sabaya
 
matajiri wengi wazawa walikufa sana awamu ya JPM na hata hawa maskini wenye unafuu waliyumbishwa yumbishwa sana awamu ya mwendazake

siku hizi hatuoni misafara ya wakuu wa wilaya waliojihami kwa askari wenye bunduki wakienda kukagua duka la muuza sumu ya panya kama ana machine ya EFD
 
Kwa hiyo kipande cha SGR Tabora-Isaka Mama yenu atawapa wazawa? 😁.
 
Acheni kupotosha jamii na kujidanganya ni mfanya biashara gani tanzania anajihusisha na ujenzi wa relly bara bara nk. Mbona bakhresa ajafungwa mo deuji mengi na wengineo walio kwenda jela ni mafisadi na wezi wahuni na wakwepa Codi .Leo nchi inakua haieleweki lkn kwakua wasaliti mnaanza kupewa nafasi ya usalitishaji nchi ndo mnakua mnaropoka tu....
 
Watu wa ndani kama wakandarasi hawakupewa Kazi Kwa visingizio kibao lakini kikubwa ni wawe maskini Ili awatawale vizuri..

Walipoondoa pesa zao kwenye mabenki Ili wasiporwe na kuzuiliwa , Mwendazake alitoa biti kwamba anajua wameweka pesa ndani na atabadili noti na sarafu..

Watu wa dizaini hii ni hatari sana kwa ustawi wa Nchi,hawafai kabisa ndio maana Nchi zilizostaarabika huwa zinapiga marufuku kabisa itikadi za namna hii.
 
Kweli kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…