Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,884
- 21,175
Jordan ina watu 11m. Tanzania 65m.
Ukubwa wa Jordan ni kilomita za eneo 80, 000 na kidogo. Tanzania ni kilomita za eneo 950,000. Jordan inaingia kama mara 12 kwa tz.
Mto pekee Jordan ni mto Jordan wanaoshare na Israel. Ni nchi kame. Maji wanategemea ya visima. Hawana ardhi ya kulima. Tanzania ina mito, maziwa na zaidi ya ekari milioni 80 zinazofaa kwa kilimo.
Jordan hawana mafuta. Wanakiasi kidogo cha gesi cubic ft trilioni 12. Tanzania tuna gesi cft trilioni 57.
Jordan wanazalisha umeme MW 7,000+ na karibu nusu ni kwa kutumia hiyo gesi yao. Tz tunazalisha umeme kama MW 3500 hivi.
Pato(per capita ppp) la wastani kwa wajordan ni dola 12,000. Tanzania ni 4,000.
Jeshi la Jordan linazalisha silaha kama bunduki, risasi na mizinga.
Jordan inapokea watalii karibu milioni 8 kwa mwaka. Kivutio chao kikubwa ni mapango ya Petra.
Tanzania ni moja ya nchi yenye vivutio vizuri zaidi vya utalii duniani. Mbuga, milima na fukwe lakini haifikishi watalii 2m kwa mwaka.
Kwenye maendeleo ya watu Jordan ipo kiwango cha juu na Tz ipo kiwango cha kati.
Jordan wanachimba na kuuza nje madini ya phosphate yanayotumika kutengeneza mbolea. Tz madini ya phosphate huko minjingu sijui yanaendeleaje.
Jordan inatawaliwa kifalme. Tanzania inatawaliwa/inajenga utawala wa kidemokrasia.