Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Bila ya kuwa na chuki na mtu yeyote, ukweli ni kwamba Mama Samia ana bahati kubwa kwenye utawala wake.
Bahati yake kubwa ni utawala uliomtangulia. Utawala uliomtangulia ulikuwa ni utawala wa chuma, ulikuwa ni utawala ulioumiza wengi. Hivyo, yeye akifanya jambo kidogo tu la kuwaletea nafuu wale walioonja machungu ya utawala uliopita, basi pongezi, furaha ja uungwaji mkono unakuwa mkubwa. Lakini laiti kama utawala wa Mama Samia ungefuata baada ya utawala wa Mkapa au Kikwete, sidhani kama angeonekana amefanya makubwa kwa haya ambayo mpaka sasa ameyafanya.
Kwa hiyo tusifurahie sana na kupongeza sana kwa mafanikio au mabadiliko kidogo.
Kiongozi makini hutumia muda mwingi kujenga mifumo imara ya uongozi na usimamizi. A good leader always creates leaders by creating collective leadership.
Kwa sasa tunafurahia sana kuona mbaazi zimezaa sana mwaka huu kwa sababu ya kuwa na mvua za kutosha ilihali hatujawa na mfumo wa kuhakikisha mbaazi zinazaa kila mwaka, kuwe kuna mvua au hakuna mvua.
Mama Samia hata atoe maelekezo mengi ya kuwaletea umafuu wananchi kiasi gani, kama hataenda kwenye msingi wa matatizo yetu, hatakuwa amelisaidia Taifa, naye atapita bila kuacha legacy yoyote ya maana, kama watangulizi wake, ukimwondoa mwanafalsafa Mwalimu Nyerere.
Kuna mambo ya msingi ambayo Rais Samia anatakiwa kuyapa muda mwingi kuliko kwenda kukagua madaraja, hospitali au barabara. Mambo hayo ya msingi:
1) Upatilanaji wa katiba bora yenye kulinda haki za kila mmoja
2) Kuondoa sheria zote gandamizi, na kwa kiasi kikubwa zinazokinzana na hata hii katiba yetu ya sasa
3) Kutengeneza sheria mpya zitakazohakikisha watu wanatendewa haki, na uhuru wao kama raia unalindwa. Kwa sasa, Tanzania unaweza kubambikiwa kesi yoyote wakati wowote, ukakosa dhamana, ukaishia hata jela bila ya kuwa na hatia
4) Kutengeneza mfumo mzuri wa utawala, na kuondokana na utitiri wa vyeo visivyokuwa na maana wala mchango wowote kwa maendeleo ya Taifa. Nafasi kama za wakuu wa Wilaya na mikoa, maRAS na maDAS, ni ufajaji wa pesa za wananchi kwa sababu kazi zao zingeweza kufanywa kwa ufanisi na wakurugenzi, OCD na RPC
5) Kuondoa mfumo wa sasa wa utawala ambao unawafanya watu wengi kujikomba na kujipendekeza kwa Rais ili wapate uteuzi. Nafasi nyingi zitegemee weledi, na ziombwe. Kuwe na chombo cha uteuzi. Rais abakie na watu wachache sana wa kuwateua, hasa kwenye ngazi ya kitaifa.