Uongozi siyo mchezo. Mnachoelezea ni sawa kabisa lakini tusitegemee makubwa sana. Mwalimu Nyerere alipowauliza wanaogimbea U Rais waeleze wanataka kwenda pale kufanya nini alikuwa amegundua jambo. Na ukiacha misingi ya uongozi aliotuachia hakuna aliyefuata akaongeza misingi mipya mizuri zaidi
Sababu zake kuu ni kwamba uongozi ni kipaji+shauku ya kujifunza kutoka kwa wengine+ kujenga taasisi madhubuti na kuteua watu kwenye nafasi za uongozi kwa misingi ya elimu, weledi na uaminifu.
Sasa tazama taasisi zetu anza na Bunge kisha Mahakama na Serikali Kuu.
Ukiona mambo safi basi sasa anza kupendekeza agenda za utekelezaji.
Kama kiongozi anashindwa kutambua kuwa huwezi kumpiga risasi Mtanzania mwenzio kwa sababu tu yuko upande mwingine wa siasa na ukashabikia suala hilo, Katiba Mpya hata ikipatikana itakuwa ya ovyo maana nani watatengeneza hiyo Katiba?
Nashauri twende hatua moja baada ya nyingine.
L
Mwanzo wa jambo lolote zuri huanzia kwenye fikra. Kuna wakati, kulikuwa na fikra zilizokuwa zikijengeka, na ambazo zilikuwa sahihi, mtu hapewi uongozi kama sehemu ya ulaji bali kama dhamana, yaani dhamana inayobeba majukumu mazito ya kutatua matatizo ya watu.
Uongozi ulionekana ni kwaajili ya watu wanaoweza kujitoa kwaajili ya wengi. Na Mwalimu Nyerere, wakati fulani alipata kunena, "uongozi ni mzigo, kila mahali unapopita, ukiona kuna shida, unajua, hili ni langu".
Hivi karibuni, wakati wa hotuba ya Rais pale Mwanza, Rais alionekana kuonesha kuwa kuteuliwa ni kupewa ulaji, ni kupewa ajira, ni kitu cha kumsaidia anayeteuliwa. Kukiwa na fikra za namna hii, watu hata wasio na uwezo watakimbilia madaraka maana ni ulaji. Walioteuliwa watahangaika kuhakikisha hawaachani na ulaji. Viongozi wa namna hiyo hawatajenga mifumo wala taasisi za kiutawala bali watajitahidi kuyajenga majina yao ili majina yao yaendelee kuwemo kwenye ulaji.
Mentality ya uongozi imepotoshwa, na ndiyo maana tuna matatizo makubwa ya kuwapata viongozi wazuri. Viongozi ndio walio mstari wa mbele kutotaka mabadiliko, kutotaka katiba mpya, kutotaka sheria na kanuni zinazosimamia haki, demokrasia, na uwajibikaji kwa sababu kabla ya chochote, wanafikria mabadiliko yatakavyoathiri ulaji wao.
Tumpongeze Rais anapofanya yaliyo sahihi, tumkumbushe anapojisahau, tumkosoe anapopotoka, tumsisitizie anapolegea. Kwa sasa tumwambie kwa kauli thabiti:
Tunataka asimamie ujenzi wa mifumo imara, taasisi imara za uongozi, katiba iliyo bora, sheria zinazolinda misingi ya haki, uhuru na demokrasia. Asipoyafanya hayo, pamoja na unafuu wake katika uongozi, hatakuwa amelisaidia Taifa kutoka kwenye matatizo ya msingi.