Utawala wa Rais Samia tuupime kwa vigezo sawia

Mkuu, unachokisema ni kweli kwa Asilimia kubwa.
Mpaka sasa sijaelewa vipaumbele vya huyu mama,
By the way najarbu kufuatilia kwa umakini ili nijue
Dira yake inapoelekea, ila nashindwa kuelewa.
Still tumpe muda tuone
 
Suala la katiba co jepesi kama tunavyofikiria,hili suala akilianzisha anaweza jikuta hata nafac aliyokuwepo anatolewa,tukumbuke mzee wa msoga kilichomkuta,kwa upande wangu suala kubwa sasa hv ni kudai tume huru.
Uko sahihi sana, lakini bila mashinikizo hakuna chochote kitapatikana, sio katiba mpya, ama tume huru ya uchaguzi. Tutadai vyote, kimoja kikipatikana kitaleta kingine.
 
P1 mkuu ktk kudai haki
Uko sahihi sana, lakini bila mashinikizo hakuna chochote kitapatikana, sio katiba mpya, ama tume huru ya uchaguzi. Tutadai vyote, kimoja kikipatikana kitaleta kingine.
 
Uongozi siyo mchezo. Mnachoelezea ni sawa kabisa lakini tusitegemee makubwa sana. Mwalimu Nyerere alipowauliza wanaogimbea U Rais waeleze wanataka kwenda pale kufanya nini alikuwa amegundua jambo. Na ukiacha misingi ya uongozi aliotuachia hakuna aliyefuata akaongeza misingi mipya mizuri zaidi
Sababu zake kuu ni kwamba uongozi ni kipaji+shauku ya kujifunza kutoka kwa wengine+ kujenga taasisi madhubuti na kuteua watu kwenye nafasi za uongozi kwa misingi ya elimu, weledi na uaminifu.
Sasa tazama taasisi zetu anza na Bunge kisha Mahakama na Serikali Kuu.
Ukiona mambo safi basi sasa anza kupendekeza agenda za utekelezaji.
Kama kiongozi anashindwa kutambua kuwa huwezi kumpiga risasi Mtanzania mwenzio kwa sababu tu yuko upande mwingine wa siasa na ukashabikia suala hilo, Katiba Mpya hata ikipatikana itakuwa ya ovyo maana nani watatengeneza hiyo Katiba?
Nashauri twende hatua moja baada ya nyingine.
L
 

Mkuu una maelezo mazuri, ila hoja yako imejificha. Hoja yako ni ipi hasa? Weka kwa ufasaha kipi kifanyike ili hiyo hatua moja iwe imekamilika.
 
Mwanzo wa jambo lolote zuri huanzia kwenye fikra. Kuna wakati, kulikuwa na fikra zilizokuwa zikijengeka, na ambazo zilikuwa sahihi, mtu hapewi uongozi kama sehemu ya ulaji bali kama dhamana, yaani dhamana inayobeba majukumu mazito ya kutatua matatizo ya watu.

Uongozi ulionekana ni kwaajili ya watu wanaoweza kujitoa kwaajili ya wengi. Na Mwalimu Nyerere, wakati fulani alipata kunena, "uongozi ni mzigo, kila mahali unapopita, ukiona kuna shida, unajua, hili ni langu".

Hivi karibuni, wakati wa hotuba ya Rais pale Mwanza, Rais alionekana kuonesha kuwa kuteuliwa ni kupewa ulaji, ni kupewa ajira, ni kitu cha kumsaidia anayeteuliwa. Kukiwa na fikra za namna hii, watu hata wasio na uwezo watakimbilia madaraka maana ni ulaji. Walioteuliwa watahangaika kuhakikisha hawaachani na ulaji. Viongozi wa namna hiyo hawatajenga mifumo wala taasisi za kiutawala bali watajitahidi kuyajenga majina yao ili majina yao yaendelee kuwemo kwenye ulaji.

Mentality ya uongozi imepotoshwa, na ndiyo maana tuna matatizo makubwa ya kuwapata viongozi wazuri. Viongozi ndio walio mstari wa mbele kutotaka mabadiliko, kutotaka katiba mpya, kutotaka sheria na kanuni zinazosimamia haki, demokrasia, na uwajibikaji kwa sababu kabla ya chochote, wanafikria mabadiliko yatakavyoathiri ulaji wao.

Tumpongeze Rais anapofanya yaliyo sahihi, tumkumbushe anapojisahau, tumkosoe anapopotoka, tumsisitizie anapolegea. Kwa sasa tumwambie kwa kauli thabiti:

Tunataka asimamie ujenzi wa mifumo imara, taasisi imara za uongozi, katiba iliyo bora, sheria zinazolinda misingi ya haki, uhuru na demokrasia. Asipoyafanya hayo, pamoja na unafuu wake katika uongozi, hatakuwa amelisaidia Taifa kutoka kwenye matatizo ya msingi.
 
Ongea kilichopo hapa we pumbavu,hata ukimchukia vp jiwe alikua rais hasa.
Hivi nyie mafala mlijuaje kuna JF.
Zamani tunajadili mada haswa hapa zinazoeleweka.
Nyie ngedere sijui mmetoka wapi mnaongea upuuzi tu
Mfuate uyo dikteta jiwe kaburini Kama unampenda sana
 
Kwa kifupi, Mama hatoshi.
Dah, hii Nchi hata ashushwe Malaika aje kutuongoza bado tutalaumu tu,mama ana siku mia tayari hafai,
Ndiomaana Mungu alimleta dikteta Ngosha atunyooshe, Sasa akiondoka mama naomba mungu Ndugai achukue madaraka mlimie meno aisee
 
Naomba niwe mkweli,na ukweli utaniweka huru.
Mimi Ni mmoja wa watu humu jamvini waliofurahia Sana Mama huyu kukalia kiti.
Nilifurahi sio kwa sababu ya uwezo wake lahasha,nilifurahi huku nilijua kabisa hawezi kubadilisha mahitaji mapana ya kidemokrasia ya nchi hii,kwa sababu yeye Ni mwana CCM na CCM Ni adui mkubwa wa demokrasia.
Nilifurahi kwa sababu Mungu ametuondolea yule mwovu na akatupa huyu mama angalau tupumzike kidogo.
Yule mwovu alikua katili huyu mama Ana utu.
Na utu wa huyu mama utaondilewa na CCM kwa sababu CCM Ni chama Cha kiovu.

Mwisho nilifurahi kwa sababu yule mwovu angeweza kubadili kipengele Cha katiba ili atawale milele.huyu mama sidhani kama atakua na tamaa hiyo.akifikia kutamani hivyo tutasali Tena.
Ukweli Ni kwamba mama Hana jipya labda hofu yake kwa Mungu na wema wake ndio unaomtofautisha na yule Mwovu.
Na hiyo ndio ilikua furaha yangu.
 
Safj sana mleta mada, umeandika mambo ya msingi sana.

Tunampongeza na kumshukuru rais Samia kwa kurekebisha baadhi ya mambo mabaya ya Magufuli lakini pamoja na hayo Tunataka sasa ajikite kwenye mabadiliko ya kimfumo ya nchi hii. Tunataka abadilishe katiba ili kesho na keshokutwa asipokuwa kwenye hicho kiti basi Taifa liongozwe kwa sheria na katiba nzuri.

Bila kubadili katiba, anaweza kuja rais katili mara kumi zaidi ya Magufuli na akaumiza watu huku katiba hii ya sasa ikimlinda.
 
Katiba Mpya ya wananchi, Rasimu ya Warioba ndiyo jibu la mambo yote. Tuzidi kumuombea Rais SSH Mungu azidi kumuangazia, kumpa busara ili atuachie Katiba
 
Ongea kilichopo hapa we pumbavu,hata ukimchukia vp jiwe alikua rais hasa.
Hivi nyie mafala mlijuaje kuna JF.
Zamani tunajadili mada haswa hapa zinazoeleweka.
Nyie ngedere sijui mmetoka wapi mnaongea upuuzi tu
Ni mwemdawazimu tu misukule ndiyo watashangilia namna Mwendazake alivyoyawala HOVYO nchi yetu. Na Mungu wetu anatupenda ndiyo maana kamfurusha jehanam takataka yule
 
Siku 100 ni standard, sio lazima ziwe kapimo cha kila mtu. Ndani ya siku 100 sio kipimo, bali ni kutoa mwenendo halisi wa utawala wake kwa ujumla, kwa kuangalia mwanzo wake. Ama huo utawala wake ni eneo moja tu la katiba mpya?
Tatizo la kusubiri siku mia zinakufunga mdomo kukemea mengine, na zaidi, siasa ni kama vita, huwezi kujiweka kando siku mia ili kufanya uchunguzi wakati adui yako yuko field.
 
Huyu ni mtoto wa Nassor Moyo ameteuliwa DC Iringa mjini wakati ni raia wa Zanzibar kisheria ni makosa kwasababu ukuu wa wilaya au ukuu wa mkoa sio sehemu ya muungano at all yaani is it possible kwa Paul Makonda kuwa RC Chakechake?

Rais wenu anatuona watanganyika mafala na wajinga maana yako kimya tu hata hayaoji, nchi inatawaliwa kibaguzi kiasi hakuna mtanganyika anaruhusiwa kuwa DC ama mbunge ama hata kumiliki ardhi tu ,Leo wao wanakuja huku bara na kupewa wilaya kirahisi halafu raia wa bara wanabaki wanaimba mapambio tu pumbavu sana mijitu ya bara tuamke,tunaupenda muungano lakin sio katika namna hiyo..

Tunataka kwa zama za leo,muungano wetu ubaki kwenye masuala ya ulinzi na usalama pekee hayo mambo mengine ni kutuumiza watanganyika na kutuona sisi wajinga,wapumbavu,leo umevunja sheria na miiko ya kimuungano kututeulia watu walio demand code yao ni 259 na si hapo tu,masuala ya local government au serikali za mitaa si mambo ya kimuungano,kwann katiba inabakwa namna hii??

Majuzi,makam wa rais alisema county code yao sio 255 ni 259,broh huelewi tu?? Watanganyika hatujawah kuwa na hisia hizi lakini tukianza kuhoji tutakuwa ni watu wabaya kuliko,sasahv umeunda tume ya wanzanibar pekee bila ku balance kufuatilia masuala ya madini for what reasons?? Tunajua wewe sio muumini wa Muungano basi ukishindwa kuulinda basi usituvurigie taifa letu..

255🇹🇿✊
MAMA SAMIA HESHIMU KATIBA
 
Tatizo la kusubiri siku mia zinakufunga mdomo kukemea mengine, na zaidi, siasa ni kama vita, huwezi kujiweka kando siku mia ili kufanya uchunguzi wakati adui yako yuko field.

Siku mia ni katika muktadha upi? Kumbuka siku mia sio za kuanza kukemea ukiukwaji wa sheria, au uvunjwaji wa haki za binadamu, bali siku mia ni za kutoa tathmini. Usichanganye kukemea siku yoyote, na kutoa tathmini pls.
 
Siku mia ni katika muktadha upi? Kumbuka siku mia sio za kuanza kukemea ukiukwaji wa sheria, au uvunjwaji wa haki za binadamu, bali siku mia ni za kutoa tathmini. Usichanganye kukemea siku yoyote, na kutoa tathmini pls.
You know what, una miss point ndogo sana; iko hivi, after hiyo analysis utayo make after 100 days, then utajikuta unarudi kule mwanzo kuanza kukemea, kupigania, na mengine, coz kwenye analysis yako utatumia udhaifu uliouona kwenye utawala kama silaha kuanza kushambulia tena.

So kwangu naona siku mia ni kama kujizubaisha tu, why uione silaha ya kumpiga adui sasa ila ukae kimya kusubiri 100 days ambazo zikifika bado kuna uwezekano ukaitumia silaha ile ile ya mwanzo kumpigia adui yako?

Hapa kuna tofauti kati ya siasa za magazetini (analysis siku mia) na siasa za field (Katiba Mpya inahitajika hata sasa lazima ipiganiwe).

Au wewe unataka kutumia hiyo analysis ya siku 100 kuandika kitabu? inawezekana una lengo tofauti na ninalofikiria mimi. Hii mambo ya analysis wangeachiwa wachambuzi wa siasa na mambo ya uchumi wakaweke kwenye magazeti yao, ndio style yao, lakini kwa aina ya siasa za "tit fot tat" nataka hiki ili nifanye kile, mfano Tume Huru ili nishiriki uchaguzi, analysis kwangu ni kupoteza muda tu.
 

Kwa haraka haraka hapa naona kama unasaka ushindi kwenye hoja hii. Kama ni ushindi unasaka, basi naweza kusema umenishinda.

Kimsingi hakuna mtu yoyote anayesubiri analysis yangu, na wala hiyo analysis ya siku 100 haizuii mtu yoyote kukosoa. Naona unalazimisha kufanya hiyo analysis kuwa ni Katazo la ww au yoyote kukosoa. Isitoshe mpaka sasa watu wanakosoa, labda huoni post hizo za kukosoa. Na hiyo unayosema katiba mpya inadaiwa toka 1992 enzi za mfumo wa chama kimoja kuingia vyama vingi, ila kuna wakati nguvu ilikuwa kubwa, na kuna wakati inashuka. Hivyo kama ni kukosoa ww kosoa tu, na kama ni katiba mpya ww idai tu maana hakuna Katazo hilo. Imeisha hiyo.
 
Acha chuki mkuu. Unajuaje kama huyo Moyo asili yao ni Iringa?. Wazenji wengi kwao ni huku bara.

Jenga hoja kwa umakini ili usionekane mbaguzi.
 
Nimeshajitoa mapema sana kumsapoti JUMONG nimeona mbali sana. Najua jambo zuri ni yeye kutokuwa kama Magufuli Ila mengine yote ni hakuna kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…