Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kwa wale wanaojua historia ya Uganda, watakuambia wazi kwamba utekaji na uuaji unaofanyika hivi sasa nchini Tanzania ni sawa kabisa na vyombo vya dola na usalama vilivyowafanyia wananchi wa Uganda wakati wa utawala wa dikteta Idd Amin Dada wa Uganda.
Polisi na chombo kilichoitwa State Research Bureau (SRB) of Uganda, ambacho kilikuwa ni sawa na TISS ya Tanzania, walifanya utekaji na uuaji wa wananchi wa Uganda walioonekana kupinga hadharani au kisiri utawala wa dhalimu Idd Amin Dada. Mara nyingi waliwavamia wananchi wakiwa ofisini, mitaani na hata nyumbani, kuwaingiza kwenye magari kwa nguvu na kutokomea nao. Waliwaua na kuwatupa msituni au mitoni, pamoja na Mto Kagera.
Polisi na SRB wa Uganda walifanya haya mbele za watu, na wananchi walikuwa wameingiwa uoga hawakuweza kufanya kitu wala kutoa msaada wowote pale ambapo waliona wananchi wenzao wakitekwa, japo walijua wanaenda kuuawa!
Kama inavyofanyika Tanzania, Polisi wa Uganda wakati huo walitoa matamko ya juu juu tu kuhusu watu kutekwa, na Raisi Idd Amin aliwasifu SBR na Polisi kwa kazi nzuri ya kusimamia amani na utulivu nchini Uganda, kama vile tu ambavyo hapa Tanzania tumesikia jeshi letu la Polisi likisifiwa kwa kazi nzuri katika kipindi hiki kigumu cha utekaji na uuaji.
Na utekaji na uuaji nchini Uganda ulianza taratibu, lakini kadiri muda ulivyozidi kwenda, Polisi watekaji na SRB (sawa na TISS) hawakuogopa tena. Walifanya utekaji huu waziwazi kabisa. Kumekuwa na kila dalili kwamba hata hapa Tanzania tunaona watekaji wakizidi kuwa na ujasiri wa kuteka watu bila kuogopa, hata mchana kweupe!
Ilifikia mahali ambapo waliotekwa na kuuawa nchini Uganda walitia ndani raia, wanasiasa waliopinga utawala wa Idd Amin, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi za serikali nk.
Utekaji na uuaji Uganda ulikuja kukoma baada ya vita vya Kagera pale ambapo majeshi ya Tanzania yalimwondoa Idd Amin Uganda. Ndio maana hata sasa hapa nchini wananchi wameanza kuona kwamba pengine tunahitaji nguvu kama hiyo ili kukomesha utekaji na uuaji ambao asilimia kubwa sana ya wananchi nchini wanauhusisha na vyombo vya dola dhidi ya watu wanaoonekana kuwa na upinzani dhidi ya utawala serikali iliyopo madarakani