Utekelezaji: Shule ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ruvuma

Utekelezaji: Shule ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ruvuma

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
Mwonekano wa Ujenzi wa Shule mpya maalum ya Sekondari ya Bweni na sayansi ya Wasichana katika Mkoa Ruvuma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita iliyosajiliwa rasmi kwa jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya Namtumbo.

Ujenzi wa shule hiyo Mpya unatekelezwa kupitia Mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa gharama ya shilingi bilioni 4 ambapo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo.leo tarehe 06 Januari 2023.

Ujenzi unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ya utekelezi wa mradi huo ulianza tarehe 6 April 2022 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Januari 2023 na itatumia fedha Kiasi cha bilioni 3.

Katika awamu hii ya kwanza vinajengwa vyumba vya madarasa 12, jengo la utawala 1, maabara 4, matundu ya vyoo 16, chumba cha jenereta 1, bwalo 1,mabweni 5, mitaro ya maji, kichomea taka 1, matanki ya chini ya maji, matanki ya plastiki, uzio, njia za kutembea na nyumba za walimu 2.

Awamu ya pili ya mradi huu unatarajiwa kuanza wakati wowote ndani ya mwaka huu kwa fedha na fedha kiadi cha shilingi kiasi bilioni 1 kitaletwa kutoka Serikali Kuu ambapo yatajengwa madarasa 10 yenye ofisi za walimu 3, chumba cha ICT, Maktaba, nyumba nne za walimu na mabweni manne (4).

324404721_484418830542745_1970285690092263545_n.jpg
324407888_833457627720629_8899505898582107761_n.jpg
324467371_3853683614858092_9086408218532651061_n.jpg
324396994_574596364501346_6632070420035833527_n.jpg
324552936_676793964147349_2798661164442801953_n.jpg
324404721_484418830542745_1970285690092263545_n.jpg
 
kama una uwezo kumpeleka mwanao shule za umma yataka moyo mkuu though sisi wengi tulisoma hizo hizo wakati huo, Msalato, Mazengo, Bihawana, Kibaha, Tabora boys & girls, Moshi tech, Ifunda nk miaka ya 80 - 90.

Wengi wanawapeleka za high school baada ya kujitambua.
 
shule hata ukuta hakuna!

mnamaliza maeneo tu si mjenge maghorofa
Bro mbona unamaliza maneno hivyo ujenzi wake haujakamilika bado, shule za ghorofa zinajengwa kuwa mfatiliaji moja iko Wilaya ya Temeke shule ya Dovya, Kuna ya Tabata Liwiti una uhaba wa taarifa
 
Back
Top Bottom