Utekelezaji wa Elimu ya Lazima Miaka 10 kuanza Mwaka 2027/28

Utekelezaji wa Elimu ya Lazima Miaka 10 kuanza Mwaka 2027/28

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 kuhusu elimu ya lazima kuwa ya miaka 10 utaanza Mwaka 2027/28 ambapo wahitimu wa elimu ya msingi ya miaka 6 watakutana na wahitimu wa mwisho wa elimu ya msingi ya miaka saba wote wataanza kidato cha kwanza.
Snapinsta.app_461175012_1478335746203933_7961648614135897234_n_1080 (2).jpg

Snapinsta.app_461252827_838302661812413_1302297728360085221_n_1080 (1).jpg

Snapinsta.app_461285897_1541171727280554_849427512197644814_n_1080 (1).jpg
Prof. Mkenda amesema hayo Mkoani Ruvuma Septemba 26, 2024 akitoa mada juu ja mageuzi ya Elimu katika Kongamano la Mafunzo kwa Umoja wa Wanawake Tanzania, ambapo ameongeza kuwa ifikapo Mwaka 2027/28 Mtoto ambaye hatakaa shuleni kwa miaka 10 hatua zitachukuliwa kwa mzazi au mlezi.

Waziri huyo amesema kuwa Wizara ilifikia hatua ya kufanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na kuboresha Mitaala baada ya watanzania kulalamika juu ya elimu inayotolewa na namna inavyomuandaa mwanafunzi kuingia kwenye ulimwengu wa ajira na ndipo Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa maelekezo ya kufanya mapitio hayo.
Snapinsta.app_461321061_1182066476390971_8604480096754741114_n_1080 (1).jpg
 
Tunaomba pro. Mkenda awepo mpaka mwaka huo inshallah , maana unaweza kushangaa katimuliwa mwakani au siku kadhaa mbele .

Nia ni nzuri ila hatuna taasisi ya kusimamia malengo ya muda mrefu kama hayo , bora uwaziri uwe ni taasisi ili kuwa na mipango ya muda mrefu bila kuharibu utekelezaji.
 
Hayo madarassa na facilities za kuwabeba watoto double year mnayo? Au ndio mambo yale yale ya unakifunga kiti na meza kwa kamba unachora na jina lako hahahaha
 
Tunaomba pro. Mkenda awepo mpaka mwaka huo inshallah , maana unaweza kushangaa katimuliwa mwakani au siku kadhaa mbele .

Nia ni nzuri ila hatuna taasisi ya kusimamia malengo ya muda mrefu kama hayo , bora uwaziri uwe ni taasisi ili kuwa na mipango ya muda mrefu bila kuharibu utekelezaji.
Kama ule mwaka Physics iliumganishwa na Chemistry.
 
Hayo madarassa ya kuwabeba watoto double year mnayo?
Asilimia kubwa ya shule (hasa zisizo mjini), Zina madarasa ya ziada kwa Sasa (Tena yapo Hadi yaliyojengwa baada ya Rais Samia kuingia madarakani). Imani yangu suala Hilo litakuwa limeshachakatwa na kuandaliwa mkakati wa kukabiliana nalo kwa shule zenye upungufu wa madarasa.
 
Back
Top Bottom