Utendaji kazi wa Rais Magufuli ni kilio kwa Upinzani nchini

Utendaji kazi wa Rais Magufuli ni kilio kwa Upinzani nchini

Trump2

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
1,553
Reaction score
2,610
UTEKELEZAJI wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mpinduzi (CCM) unaofanywa na Rais John Pombe Magufuli umekuwa kilio kwa vyama vya upinzani, hususan Chadema na CUF.

Kubwaga manyanga kwa wabunge na madiwani wa vyama hivyo wakiunga mkono jitihada za Rais Magufuli ni ishara tosha kwamba, Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kutatua kero za wananchi zilizokuwa zikipigiwa kelele na wapinzani, hivyo wameona hawana namna nyingine zaidi ya kuhamia CCM ili kuonga mkono jitihada hizo.

Hali hiyo inafuatia Mbunge wa Liwale kupitia CUF, Zuberi Kuchauka, naye kutangaza kujiuzulu uanachama wa chama hicho pamoja na kujivua ubunge na kuhamia CCM kuendelea kuunga jitihada za Rais Magufuli.

Kuchauka alitangaza uamuzi huo jijini Dar es Salaam leo na kupokewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally Kakuru, kwenye Ofisi Ndogo za chama Mtaa wa Lumumba.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dkt. Bashiru alisema kwamba, utendaji wa Rais Magufuli ndiyo kichocheo kikubwa cha wapinzani kuhamia CCM, kwani wanaona hakuna kilichobakia kwao kuendelea kukipigia kelele.

Kuchauka alitaja sababu za migogoro ya ndani ya CUF na siasa za makundi kwa ujumla kwamba ndizo zilizomlazimu kurudi CCM.

"Nimechoshwa na siasa za makundi na migogoro ndani ya CUF, nilishindwa kufanya kazi vizuri, yaani kuna wakati mwingine unakwenda jimboni kufanya shughuli za siasa, halafu wananchi wanakuuliza; Wewe CUF Lipumba au Maalim? Sasa nikaona nashindwa kufanya kazi zangu vizuri," alisema.

Alisema utendaji kazi wa Rais Magufuli umevutia kufanya naye kazi kwa karibu, kwani kwa kipindi kifupi cha miaka mitatu ameweza kutekeleza sera ambazo wapinzani walikuwa wakizipigia kelele.

"Raisi Magufuli amenivutia pia utendaji wake wa kazi, sisi wapinzani tulikuwa tukipigia kelele rushwa, ufisadi, Rais Magufuli ameweza kuyasimamia kikamilifu mpaka kuanzisha mahakama za mafisadi, sasa nibaki upinzani natafuta nini?" alihoji.

Kuchauka amekuwa mbunge wa tano wa upinzani kubwaga manyanga na kujiunga na CCM katika kipindi cha takriban miaka miwili na nusu ya awamu ya tano.

Mtiririko mzima wa matukio ya wabunge wa upinzani kubwaga manyanga na kujinga na CCM ni kama ifuatavyo:
Desemba 2, 2017: Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia CUF, Maulid Mtulia, aliamua kujiuzulu uanachama na hatimaye kujiunga na CCM.

Mtulia mwenyewe alisema: "Mimi Maulid Said Abdallah Mtulia, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Civic United Front – (CUF) Chama cha Wananchi kwa hiari yangu nimeamua kujiuzulu uanachama wa CUF na kujiuzulu nafasi zangu zote za uongozi nilizokuwa nashikilia. Nimefanya uamuzi huu leo tarehe 02/12/2017 kwa utashi wangu na bila shinikizo la mtu yeyote.
"Sababu za kufanya hivi ni kutokana na uzoefu nilioupata kwa miaka miwili ya ubunge wangu ambapo nimebaini kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni chama tawala inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo sisi upinzani tuliahidi kuyatekeleza.

"Kwa kuwa nia yangu ni kuwatumikia wananchi, sioni sababu ya kuendelea kuwa upinzani na badala yake nimeona ni vema niungane na juhudi za Serikali kwa kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo na kukabiliana na kero mbalimbali.

"Nawashukuru wananchi wa Jimbo la Kinondoni kwa kunipa dhamana ya ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita na nawaahidi kuwa nipo tayari kuendelea kushirikiana nanyi katika maendeleo nikiwa katika uwanja mwingine wa siasa ambao ni Chama Cha Mapinduzi.

"Pia nawaomba wananchi na viongozi wengine ambao wanatambua mchango wa Rais Magufuli na Serikali yake kutosita kuungana nae katika kazi za kuitumikia nchini badala ya kuwa wapinzani," alisema Mtulia ambaye sasa ni mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM.

Desemba 14, 2017: Mbunge wa Jimbo la Siha, Godwin Aloyce Mollel (Chadema) alijivua wadhifa huo na kuhamia CCM.
Dkt. Mollel, ambaye alirejea tena bungeni kwa tiketi ya CCM, naye aliandika katika taarifa yake: “Nimeona nia ya dhati ya Serikali CCM kutetea rasilimali za Taifa, nikaona niweze kujiuzulu nafasi yangu ya ubunge ili niweze kwenda kujiunga kwa vitendo katika kulinda rasilimali za Taifa letu, aminini watu wangu wa Siha nimeona mbali katika maamuzi haya, wana CCM napendekeza na nyie mnipokee.”

Julai 28, 2018: Mbunge wa Ukonga, Mwita Mwikwabe Waitara (Chadema) ajiuzulu na kuhamia CCM huku akitaja sababu kwamba ni kutofautiana na viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema baada ya kuhoji kuhusu matumzi ya ruzuku pamoja na demokrasia ndani ya chama.

Alisema kwamba, alihoji matumizi ya shilingi milioni 237 za ruzuku kwani mpaka sasa Chadema haina Ofisi Kuu, ya Kanda wala Mkoa.
“Mimi nataka niende mahali ambako kuna kazi za kufanya,” Waitara aliwaambia waandishi na kuongeza kwamba anatamani kuwa Waziri Kamili.

Julai 30, 2018: Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (Chadema), alijiuzulu na kuhamia CCM na kupokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.
Kalanga, ambaye alikuwa 'Team Lowassa" mwaka 2015, alisema: "Siasa za uhasama, malumbano na chuki zimeniondoa Chadema. Nimeamua kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa maslahi ya taifa... Kwa sababu huwezi kufanya hivyo ukiwa upande wa pili, lazima utaonekana msaliti tu... Wana Monduli naombeni mnielewe, nitakuja kuzungunza nanyi."
Agosti 13, 2018: Mbunge wa Jimbo la Liwale (CUF), Zuberi Kuchauka, ametangaza kujiuzulu na kuhamia CCM na kupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Bashiru Ali.

Akasema: "CCM imebadilika. CCM niliyoiacha mwaka 2005 siyo hii ya leo. Hii CCM ya awamu ya tano nimekubali kwamba imerejea kwenye Misingi ya TANU. Misingi ya TANU imerejea, hivyo sikuona kigugumizi cha kurejea."
Lakini wachunguzi wa masuala ya siasa wanaeleza kwamba, mafukuto ndani ya Chadema na CUF yameondoa matumaini ya wabunge, madiwani na wanachama wengi wa vyama hivyo, ambao wameamua kujiunga na CCM.

"Kuna fukuto ndani ya Chadema na CUF ambapo baadhi ya wabunge wanadhani future zao hawazioni ndani ya vyama vyao. Mbaya zaidi, hawa wabunge walisombwa na (Edward) Lowassa ambaye wanadhani hana future ndani ya Chadema na Ukawa," amesema mwananchi mmoja ambaye hakutaka kutajwa gazetini.

Katika kipindi hicho pia imeshuhudiwa madiwani zaidi ya 50 wa upinzani wakihamia CCM huku ikielezwa kwamba wimbi hilo ni kubwa na litawazoa wengi.
 
Mwambie sasa hivi kachelewa, hakuna mtu anayejielewa atapiga kura tena. Muambie akariri maneno yote anayepewa kisha angoje siku ya uchaguzi kurudiwa aone atapata wapiga kura wangapi wanauonga mkono huo utendaji wa rais.
 
Hakuna haja kupiga kura tena, wanatufanya mabwege.
Huko wanakokwenda utashangaa 2020. Patachimbika na chama litakuwa na hali mbaya Sana.
 
Mpelampela wa awamu ya tano sio wa kitoto. Watu wamemtazama kaka wa Hai, wakagundua ni msanii ambaye alitumia uhuru wa enzi za JK kwa kuweza kuziteka akili za watu. Hata CUF na yenyewe ni kama kamba iliyoelemewa na nguo nyingi hivyo inasubiri kukatika tu.
 
Ninachokiona ni Kwamba huenda huko mbele CCM itawakumbatia wengi walio upinzani na kuwaacha wale wakongwe na matokeo yake hao wakongwe watahamia upinzani .
 
Kiukweli Chadema kwa muda mrefu wamekuwa ni watu wa kujenga hoja zitokanazo na matukio na si utafiti.

Rais Magufuli alipoingia madarakani Chadema walianza kumvizia wakiamini kwamba atakwama mahali ili wapate matukio ya kujengea hoja zao.

Walianza kuvizia ATCL ifeli lakini wamechemka kwani juzi meya wa jiji la Dsm Isaya Mwita ( Chadema) amempongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wa busara wa kununua ndege. Mwita alishiriki uzinduzi wa safari za ATCL kwenda South Africa na alisafiri hadi bondeni.

Wamevizia kwenye madini nako wamechemka kwani jana tumeshuhudia BoT ikikabidhiwa mzigo wa kutosha wa madini.

Sasa wanavizia kwenye Taifa stars nako watachemka.

Mambo yote waliyopigania Chadema na Dr Slaa kwa zaidi ya miaka 20 Rais Magufuli ameyamaliza chini ya miaka mitatu, tumpongeze kwa kweli.

Jumapili njema
Maendeleo hayana vyama!
 
Kama kuna utendaji mkubwa namna hiyo kwanini bado anawabana mikutanoni,kwenye vyombo vya habari,takwimu hadi NGOs?
 
Mbinu inayotumika na serikali ya awamu ya tano, ni zile mbinu zilizotumika huko ulaya Mashariki kwenye nchi zanazoamini katika mabavu. Mbinu hizo ni kuhakikisha vyombo vyote vya habari vinabanwa na kuhubiri mambo ya serikali tu. Mtu yoyote anayeamsha waliolala yanamkuta ya Lissu. Chombo chochote cha habari kinachotoa habari isiyombeba mtawala kinafungiwa. Taasisi yoyote itakayotoa ukweli kuhusu udhaifu wa mtawala yanawakuta yaliyowakuta Twaweza.

Ukweli mchungu, Magufuli sio rais mzuri na hatakaa awe rais mzuri, bali ni rais anayesimamia mitazamo yake bila kujali ni mizuri ama la. Rais anayejikita kwenye eneo moja la nchi la mambo ya miundo mbinu sio rais mzuri bali anapaswa kuwa waziri wa ujenzi. Rais mzuri ni yule anaye balance mambo yote kama uchumi, biashara, kijamii nk. Alichofanya Magufuli ni kuanzisha dhehebu jipya ndani ya nchi la kumsifu na kumtukuza na kuhakikisha hakuna mwingine anayesema wala mapungufu yake kuwekwa wazi ili kubalance mambo. Ushahidi wa ubora wake ungepimwa kwenye box la kura, lakini huko ndio kashindwa kabisa kupaheshimu.
 
Ukiwauliza hasa hoja yao kuu ni nini?
Watakwambia mara bashite kafanye vile, mara mikutano ya siasa na mambo mengine useless kabisa
 
Huu ni utawala uliofeli kuliko wowote ule ktk historia ya nchi hii. Unahusishwa na vitendo vingi vya ukiukwaji wa haki za raia na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.

This regime is a liability to the disenchanted people of this country. It's only good at coercing cheap support from the dejected and limbless people of this country. Very hopeless to say the least.
 
Mbinu inayotumika na serikali ya awamu ya tano, ni zile mbinu zilizotumika huko ulaya Mashariki kwenye nchi zanazoamini katika mabavu. Mbinu hizo ni kuhakikisha vyombo vyote vya habari vinabanwa na kuhubiri mambo ya serikali tu. Mtu yoyote anayeamsha waliolala yanamkuta ya Lissu. Chombo chochote cha habari kinachotoa habari isiyombeba mtawala kinafungiwa. Taasisi yoyote itakayotoa ukweli kuhusu udhaifu wa mtawala yanawakuta yaliyowakuta Twaweza.

Ukweli mchungu, Magufuli sio rais mzuri na hatakaa awe rais mzuri, bali ni rais anayesimamia mitazamo yake bila kujali ni mizuri ama la. Rais anayejikita kwenye eneo moja la nchi la mambo ya miundo mbinu sio rais mzuri bali anapaswa kuwa waziri wa ujenzi. Rais mzuri ni yule anaye balance mambo yote kama uchumi, biashara, kijamii nk. Alichofanya Magufuli ni kuanzisha dhehebu jipya ndani ya nchi la kumsifu na kumtukuza na kuhakikisha hakuna mwingine anayesema wala mapungufu yake kuwekwa wazi ili kubalance mambo. Ushahidi wa ubora wake ungepimwa kwenye box la kura, lakini huko ndio kashindwa kabisa kupaheshimu.
Kwani Lowassa aligaragazwa kwenye box la nini?!!
 
CCM ndiyo inakufa kwani siku hizi sisikii serikali ya CCM bali inasikika serikali ya mtu mmoja kwa hiyo akiondoka madarakani ndiyo mwisho wenu,endeleeni kufurahia kifo chenu.
 
Kiukweli Chadema kwa muda mrefu wamekuwa ni watu wa kujenga hoja zitokanazo na matukio na si utafiti.

Rais Magufuli alipoingia madarakani Chadema walianza kumvizia wakiamini kwamba atakwama mahali ili wapate matukio ya kujengea hoja zao.

Walianza kuvizia ATCL ifeli lakini wamechemka kwani juzi meya wa jiji la Dsm Isaya Mwita ( Chadema) amempongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wa busara wa kununua ndege. Mwita alishiriki uzinduzi wa safari za ATCL kwenda South Africa na alisafiri hadi bondeni.

Wamevizia kwenye madini nako wamechemka kwani jana tumeshuhudia BoT ikikabidhiwa mzigo wa kutosha wa madini.

Sasa wanavizia kwenye Taifa stars nako watachemka.

Mambo yote waliyopigania Chadema na Dr Slaa kwa zaidi ya miaka 20 Rais Magufuli ameyamaliza chini ya miaka mitatu, tumpongeze kwa kweli.

Jumapili njema
Maendeleo hayana vyama!
NI KWELI MANA HATA MBINU YA KUPORA KOROSHO ZA WAKULIMA BILA KULIPA HAIJAWAHI KUWEPO
hata mbinu ya kuzibinya taasisi za kiraia haikuwepo kabisa.
hata mbinu ya kupambana na CAG haikuwepo
 
NI KWELI MANA HATA MBINU YA KUPORA KOROSHO ZA WAKULIMA BILA KULIPA HAIJAWAHI KUWEPO
hata mbinu ya kuzibinya taasisi za kiraia haikuwepo kabisa.
hata mbinu ya kupambana na CAG haikuwepo
Muulize Cecil Mwambe kama wakulima wa korosho hawajalipwa!
 
seli ekari yawasiojulikana,hofu kila mahala anawahofia mpaka wananchi wake
 
Back
Top Bottom