A GIRL OF THE GIRLS
Member
- Jul 21, 2022
- 29
- 163
Uwajibikaji ni kitendo cha kutimiza majukumu uliyopangiwa kiasili(kama mzazi katika familia) na mahala pako pa kazi na muajiri wako. Uwajibikaji ni neno linalotokana na neno wajibu linalomaanisha kufuata majukumu na kuwa mwangalifu wakati wa kufanya maamuzi au kufanya jambo. Kuna mifano mingi ya uwajibikaji kama ifuatavyo; wajibu kwa mtu binafsi(kujilinda), wajibu wa nyumbani (kama mzazi au mtoto), wajibu wa raia(kuwa mzalendo), wajibu wa kazini( kama mwajiri au mwajiriwa) na mifano mingine mingi.
Uwajibikaji unatumika katika maeneo mengi ya maisha yetu kwenye jamii, upo na unaendelea kwa sasa lakini ni asilimia kubwa kuwa hauna utu ndani yake. Namaanisha uwajibikaji uliopo una ubinafsi mwingi ndani yake.Mimi nazungumzia anuwai ya dhima ya kifamilia na kazini ambazo ni sehemu nyeti na muhimu, zikizingatia utumiaji wa utu katika uwajibikaji zitaleta mabadiliko chanya kwenye sekta mbalimbali hapa nchini kwetu na bara zima la Afrika.
Tufahamu maana ya neno Utu ambalo linafahamika pia kama ubuntu. utu ni uwajibikaji na ushirikiano wa watu katika jamii. utu hutuondolea ile dhana ya umimi na utuletea nuru ya umoja na mshikamano, Kwa lugha rahisi tunaweza kusema "Hakuna mimi bila wewe". Twende kuona umuhimu na faida zilizopo kwenye kuambatanisha utu katika utendaji kazi wetu katika familia na makazini.
Faida za uwajibikaji wenye utu katika anuwai ya uwajibikaji katika familia.
Familia ni kiini na kianzilishi cha sehemu ya kila kitu kizuri tunachokiona katika jamii zetu, kutoka ngazi ya mtaa mpaka taifa. Ni katika familia tunapata viongozi bora,walimu wazuri,watu wenye karama mbalimbali mfano; wahandisi, wachoraji, washonaji,madaktari,wafamasia, wachezaji,wanasheria na wengine wengi. kwa hiyo ili tuwe na watu wachapakazi maofisini, wanasanaa na wafanyabiashara wazuri lazima waandaliwe vyema na wazazi wao kutoka kwenye familia. wazazi na walezi wa watoto wana jukumu la kupalilia vipaji vya watoto wao na kuwaelekeza kwa upendo na utu katika njia sahihi. faida zinazoweza kupatikana zenye tija kwa jamii nzima ni kama ifatavyo;
Faida za uwajibikaji wenye utu katika anuwai ya uwajibikaji kazini
Ni uhakika kuwa kila mmoja wetu anaelewa maana ya kazi na umuhimu wa kazi katika maisha. Kitu ninachopenda tuzidi kuelewa ni kuwa "maisha ni kazi na kazi ni kujituma". Utendaji wetu wa kazi ukiambatana na utu utaleta manufaa mengi katika sehemu zetu za kazi na nchi yetu kwa ujumla. Hizi ndizo faida tutakazozipata iwapo tutaupa utu kipaumbele ;

- kuwa naongezeko la wasomi wengi na wenye kujiajiri; maana wazazi na walezi wakisimamia nafasi zao kikamilifu watawapa watoto haki yao yakusoma na watawafundisha karama zao binafsi walizonazo kama ushonaji, ususi, uchoraji, uhunzi na vingine vingi ambavyo vinaweza kuwafaa pale ambapo watakosa kazi ya kaujiriwa. Na hii itawezekanika kama wazazi watatenga muda wa kutosha hata mdogo tu wakukaa na kuwafunza watoto maarifa wanayoyajua .
- kupunguza jopo la ombaomba na watoto wamitaani; kwakweli sasahivi kwenye nchi yetu hasa kwenye mikoa yenye muingiliano sana ya kibiashara, kuna ombaomba na watoto wengi wa mitaani. Je, hawa watoto na watu wenye ulemavu na wazee hawana ndugu kabisa? au na sisi kwenye nchi tuanzishe nyumba za kulelea wazee kama ulaya ,labda tunabanwa sana na kazi mpaka tunashindwa kuwahudumia wazee wetu. Mimi najua hawa watoto na watu wanaoishi na ulemavu wanandugu lakini kinachowafanya wawe mitaani wanakosa msaada wa mahitaji yao muhimu kutoka ka wahusika na hapo ndio tunaweza kuuona ubinafsi.Wazazi na walezi wachukue nafasi zao kuwahudumia watoto tulio waleta dunia wenyewe, kama unajua una uwezo mdogo zaa watoto unaweza kuwahudumia kikamilifu.Lakini pia watoto tutunze wazee wetu walishafanya wajibu wao wakutulea mpaka hapa tulipo,tuwahifadhi na sisi mpaka hapo Mungu atakapowachukua tusiwaache watangetange mitaani. Na hao ndugu zetu waliozaliwa na ulemavu wana haki ya kuishi kama sisi tusiwatelekeze na huo ndio utu.
- Tutapunguza ongezeko la ndoa za utotoni na vifo vya watoto wa kike wajawazito; mpaka muda huu bado kuna wazazi wanaruhusu na kulazimisha watoto kuolewa au kuoa wakiwa na umri chini ya miaka 18. Mtoto akimaliza darasa la saba ndo amemaliza elimu yake anasubiri kuoa au kuolewa. Watu ambao bado wanafanya hivyo muache mnawasababishia madhara ya vifo kwa watoto wakike wakibeba ujauzito na pia watoto wanaozaliwa wanakuwa na ulemavu mbalimbali. Kuweni na utu msifikirie tu kuhusu faida binafsi za kupata mahali na heshima ya kuozesha , fikirieni na upande a pili wa watoto wenu.
Faida za uwajibikaji wenye utu katika anuwai ya uwajibikaji kazini
Ni uhakika kuwa kila mmoja wetu anaelewa maana ya kazi na umuhimu wa kazi katika maisha. Kitu ninachopenda tuzidi kuelewa ni kuwa "maisha ni kazi na kazi ni kujituma". Utendaji wetu wa kazi ukiambatana na utu utaleta manufaa mengi katika sehemu zetu za kazi na nchi yetu kwa ujumla. Hizi ndizo faida tutakazozipata iwapo tutaupa utu kipaumbele ;
- Tutakuza uchumi katika nyanja mbalimbali za maendeleo katika nchi yetu, hili litawezekana kama kila mtu binafsi sehemu yake ya kazi au mwenye kazi binafsi atafanya kazi kwa moyo na si kwa manufaa yake tu bali na watu wengine wanaomzunguka. Kwa mfano watu ambao wanafanya kazi kwenye utalii wakiwakaribisha na kuwapa huduma nzuri watalii.wataitangaza nchi yetu vizuri na kila mara tutakuwa na ongezeko kubwa la watalii ambayo inakuza uchumi wa nchi.
- Haki itazingatiwa makazini kwa kila mtu bila kujali huyu ana elimu kubwa, huyu ni kabila gani au huyu ni ndugu yangu. Haki ni zao moja wapo la utu, unajua tunapoomba kazi kila mtu anapewa majukumu yake na mwajiri pia huwa ana wajibu wake. kwa kipindi hiki makazini kumekuwa na mrundikano wa kazi kwa watu wachache na wengine wamerudisha na kuendekeza mambo ya undugu na ukabila katika kuajili.Tuachane na hizo kasumba mbaya tutumie utu katika kuamua na kugawa majukumu katika utekelezaji.
- Tutakomesha vitendo vya rushwa na ufisadi katika maeneo yetu ya kazi;Mimi nawawazia sana watoto wa makabwela wasiokuwa na uwezo wa kutoa pesa watapata wapi kazi?,lkn pia watoto wa kike wagumu wa kujirahisisha watapata lini kazi? Yaani kiuhalisia rushwa inatufanya tuwe wabinafsi mnoo.Na inaifanya huduma tunayotoa ionekane kuwa inajali maslahi ya watu wanaojiweza tu. Sasa sijui watu wa hali ya chini hawakupaswa kuwa kwenye hii nchi? Tunapohitaji kutoa huduma kwa watu tujtoe kwa moyo wote bila kutaka faida, maana maisha ni watu sio matajiri tu na maskini pia wanamchango wao mkubwa katika jamii.
Upvote
0