Utendaji mbovu wa BRELA unaathiri uchumi wa nchi. Rais Samia tafadhali shughulika na taasisi hii

Utendaji mbovu wa BRELA unaathiri uchumi wa nchi. Rais Samia tafadhali shughulika na taasisi hii

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Taasisi ya kusajili makampuni ya BRELA inafanya kazi bila weledi. Rushwa, uzembe na dharau kwa wateja vimetawala. Tafadhali mheshimiwa rais shughulika na watendaji wabovu BRELA.
 
Rushwa imeanzia kule juu kwa huyo unayemtaka ashughulike nayo chini, ule mkataba wa hovyo wa bandari umethibitisha hivyo, sasa unapomwambia kiongozi wa wahuni awaadhibu wahuni wenzie sioni kama upo sawa.

Unatakiwa useme Samia anatakiwa kujiuzulu, nchi imemshinda, hajui anachofanya.
 
Kiongozi mbovu wa hiyo taasisi alitokea BoT iliyofeli kuhifadhi dola unategemea ufanisi upi sasa. Akiona wakuu wa Idara wanamzidi ufanisi kazi yake ni kuwahamisha na kuleta wachawi wenzake wa kumlinda kishirikina.

Kuna ki afisa utumishi kishirikina ndio kinaongoza hiyo taasisi wanakiita Mpina. Kwa ufupi yule Nyaisa hamna kitu zaidi kujisifu utafikiri ni mteule wa Rais kumbe ni mjinga mmoja wa kuteuliwa na Waziri wa viwanda. Ondoa huyo weka mtu aliyesomea Biashara sio huyo Boharia.
 
Kabisa Brela ni hovyo kabisa!
 
Brela wanakacheni Fulani ka Rushwa, ukitaka kusajiri kampuni unaletewa maoni online marekebisho at last unapewa namba ya focal person utakaachoambiwa utashangaa.
 
Taasisi ya kusajili makampuni ya BRELA inafanya kazi bila weledi. Rushwa, uzembe na dharau kwa wateja vimetawala. Tafadhali mheshimiwa rais shughulika na watendaji wabovu BRELA.
Ni kweli kabisa unachoandika. Inatokana na tabia ya sasa ya uteuzi ambao haushindanishwi kwa "merit" hata kwa kazi zinazohitaji taaluma; ni sura yako na mtandao wako kama unaendana na mteuzi. Halafu ndiyo unasema una sera yako ya kutangaza uwekezaji wakati taasisi yenye majukumu makubwa kama Brela haifanyi kazi kwa weledi. Mwenye jukumu la kwanza na ambaye anatakiwa ajue nafasi ya Brela kwenye uchumi ni Waziri wa Viwanda. Lakini hata yeye sijasikia kama ametengua "definition" ya kiwanda ya Waziri wa zamani wa Viwanda, Bwana " "Sound" aliyesema charahani kadhaa zikiwekwa pamoja hicho ni kiwanda! Kuna kesi nimeisoma ambayo inayohusu Brela kuhamisha hisa bila utaratibu ambao umesababisha mateso makubwa kwa baadhi ya wanahisa; Mahakama Kuu imetoa uamuzi wa haki na wenye mantiki ambayo Brela ilikosa lakini Brela hawakubaliani na uamuzi wanathubutu kukata rufaa wakati Brela hawapati faida wala hasara uamuzi ukiangukia upande wo wote ule wa pande zinazogombana! Nchi hii uwezo wa kuongoza unapungua jinsi watu wengi kwenye uendeshaji ni wale wanaofuzu Phd! Watoto wataanza kugoma kwenda shule!
 
Back
Top Bottom