Utengenezaji wa Sabuni za Aina Mbalimbali: Fahamu Mahitaji, Mchakato wa Uzalishaji na Masoko

Utengenezaji wa Sabuni za Aina Mbalimbali: Fahamu Mahitaji, Mchakato wa Uzalishaji na Masoko

Nitumie bro email yangu ni karimusudi7@gmail. Com
 
JIFUNZE KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI YA KUNAIWIA MIKONO

Ingredients.jpg

Moja kati ya mahitaji makubwa ya watu ikiwemo wafanyabiashara za mama lishe,mabucha na nyingine,ni sabuni ya kunawia.Kutokana na mahitaji makubwa waliyonayo watu na kukosekana kwa bidhaa hiyo wahitaji hujikuta wakitumia sabuni ambazo hazikutengenezwa kwa kazi hiyo kama sabuni za unga,shampoo na sabuni za vipande ambazo huwasababishia madhara bila kujijua. Leo katika somo letu tutajifunza jinsi ya kutengeneza sabuni za kunawia mikono.fuatana nami mwanza mpaka mwisho.

MAHITAJI:
Sulphonic acid .soda ash .maji yaliyochujwa vizuri .pafyum .Rangi yoyote inayovutia .sless .Chumvi

JINSI YA KUTENGENEZA
Andaa vizuri chombo chako kwaajili ya kutengenezea sabuni yako kama ndoo au pipa pamoja na kuandaa malighafi zako huku ukizingatia usafi. Tanguliza kumimina ssulphonic acid vijiko vitano vya chakula kwenye chombo chako. Endelea kuweka soda ash iliyochanganywa na maji vijiko vitatu vya chai.

Weka maji lita tano ukifuatiwa na sless robo lita,chukua pafyum yoyote na uweke kijiko kimoja na nusu cha chai. Ongeza rangi kijiko kimoja cha chai na uanze kunyunyizia chumvi ambayo huleta uzito na kufanya sabuni yako isiharibike na kukaa muda mrefu. Koroga vyote kwa pamoja kwa muda wa dakika ishirini na sabuni yako itakuwa tayari.
 
UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA MICHE

external-content.duckduckgo.com.jpg

A)MAHITAJI:-
Kostik soda ya unga au ya mabonge Maji safi Mafuta ya mise/pamba/nazi/mawese n.k Rangi ya kutengenezea sabuni za miche(blue/pink/kijani n.k Marashi upendayo lemon/apple n.k Tanbihi:kama unata kutengeneza sabuni za tiba(virutubisho)utahitaji kuwa na kirutubisho unacho taka kutumia kwa mf:Aloe Vera/Ubuyu/Papai/Mwarobaini n.k Box la kutengenezea sabuni na vibao vya kukatia sabuni vyenye ukubwa wa mche wa sabuni. Ndoo kubwa za maji angalau 3 na ndoo ndogo 3,conduse ya plastiki kwa ajili ya kukorogea.Sodium Siliket,magadi soda,Hydrometa nzito pamoja na meza ya kukatia sabuni.

Kanuni:-
kostik kg 1 Maji lita 3 Mafuta lita 6 Sodium siliket grm 500 Magadi soda vijiko vikubwa vya chakula 10 Rangi kijiko 1 cha chakula Pia utahitaji eneo la kufanyia kazi pamoja na rasilimali watu angalau wawili. Loweka kostik soda kwa masaa 24,kasha ikoroge na uipime nguvu yake kwa kutumia hydrometa iwe bomee 25-30bm Ikiwa imezidi bm 30 haifai kwa matumizi ya binadamu ipunguze nguvu kwa kuongeza maji kiasi na upime tena,

Chukua ndoo ndogo ya maji na uweke mafuta,soda ash,sodium siliket,manukato na uchukue mafuta kidogo uweke kwenye spray(kiasi cha nusu lita)na uchananye na rangi au virutubisho na ukoroge vizuri baada ya kukoroga vizuri changanya na kostik soda koroga tena mpaka ichanganyike vizuri weka nailoni laini kwenye box kuzuia mchanganyo wa sabuni kumwagika(kuvuja) anza kupulizia rangi kwenye box na endelea kumimina mkorogo(mchanganyo wa sabuni kidogo kidogo huku ukiendelea kupulizia rangi kwa awamu mpaka mwisho mwisho weka contena la sabuni(box)kwenye sehemu nzuri ambapo ardhi imenyooka na usubiri kwa masaa 24

Bonge la sabuni litakuwa tayari kukatwa na ili sabuni ikauke vizuro anika chini kwenye sakafu lakini tanguliza magazeti na chumba kisiwe chenye kuingiza mwanga wa jua.
 
Back
Top Bottom