Utengenezaji wa Sabuni za Aina Mbalimbali: Fahamu Mahitaji, Mchakato wa Uzalishaji na Masoko

Utengenezaji wa Sabuni za Aina Mbalimbali: Fahamu Mahitaji, Mchakato wa Uzalishaji na Masoko

Mashine hii pia inatumia ktk utengenezaji wa sabuni ya Miche pia. Ukishachanga caustic soda ktk Maji kisha ikishapoa na kuwa tayari kuchanganya na mafuta mashine hii hutumika kuchanganya kwa kuwa kuchanganya kwa mkono husumbua hivyo mashine hii hupendwa
 
Soko la sabuni ya Maji liko vizuri kwa wale wanaotumia vifungashio vya kisasa km hiki

cbe9caa5_c26139ae_0cfb_48b6_8f30_507235f9b146.jpg


Sasa unakuta wajasiriamali wetu wa natumia vile vidumu huwa tunaweka maziwa ambayo huwezi peleka hata supermarket wakuizie kwa kuwa having hadhi. Unapowrka sabuni yako ktk kifunngashio km hicho hapo juu, ukaweka barcode na jina na nembo hata supermarket wataokubali kukuuzia kwa kuwa bidhaa yako INA hadhi ya kimataifa
mkuu naweza pata chupa za kisasa kama hio hapo juu lakini ndogo? una contact za supplier yoyote?

maana naona wengi wanatengeneza chupa za quality ya chini kama za maji
 
Mashine hii pia inatumia ktk utengenezaji wa sabuni ya Miche pia. Ukishachanga caustic soda ktk Maji kisha ikishapoa na kuwa tayari kuchanganya na mafuta mashine hii hutumika kuchanganya kwa kuwa kuchanganya kwa mkono husumbua hivyo mashine hii hupendwa
Mkuu naomba namba yako haraka!
 
Habari wanaJF..
Tutengeneze sabuni ya maji

MALIGHAFI
MASHINE YA KUTENGENEZEA IWE JABA AU KARAI

MAJI LITA KUMI

SULPHONIC ACID LITA MOJA

SLESS NUSU LITA

GLYCERINE VIJIKO VINNE VYA CHAKULA

SODA ASH VIJIKO VITANO VYA CHAKULA

FORMALINE VIJIKO VITATU VYA CHAKULA

MANUKATO KIJIKO KIMOJA CHA CHAI

RANGI YA SABUNI NUSU KIJIKO CHA CHAI

JINSI YA KUTENGENEZA

HAKIKISHA MASHINE YA KUTENGENEZEA NI SAFI
Weka Sulphonic acid na slees koroga vichanganyike weka soda ash koroga weka maji koroga vizuri hakikisha hakuna mabonge mabonge

Weka glycerine, formaline, perfume, rangi na chumvi kisha koroga kwa dakika 15.

Paki kauze....

ANGALIZO
SULPHONIC ACID IPO KAMA ASALI WEKA MBALI NA WATOTO MAANA NI KEMIKALI HATARI.

ASANTE

-QUEEN___
 
Napenda kujifunza jinsi utengenezaji sabuni za maji pamoja na sabuni ngumu, kwa anayejua tafadhali anicheki kwa nipo dDr napenda kujiajiri
 
Watu wengi wamekuwa wakiulizia sana khs vifungashio. Ukienda pale sido vingunguti opposite ya sido ukivuka barabata Utakuta maandishi makubwa ya kampuni inaitwa Omar packaging. Hawa wana vifungashio vzr sana
 
Utengenezaji wa sabuni za gharama nafuu.
Utengenezaji wa sabuni za gharama nafuu ni teknologia mpya ya kutengeneza sabuni bila ya kutumia kemikali ya aina yeyote, na utengenezaji wake hauhitaji mtaji mkubwa kama sabuni zinazotengenezwa viwandani na sabuni za magadi,zinazotumia malighafi nyingi na kemikali kali zinazo changia uharibifu wa mazingira kwa kiasi kikubwa,pia huleta madhara makubwa kama tahadhari hazito chukuliwa wakati wa utengenezaji wake. Sabuni hizo hutengenezwa kwa kutumia migomba iliyovunwa kwa kukata mikungu ya ndizi, na mafuta ya mawese/mise/pamba n.k.

Gharama za uzalishaji wa sabuni hizi rahisi kama nilivyotangulia kusema hapo mwanzo,kutokana na aina ya malighafi zinazotumika kutengeneza sabuni hizo hasa kwa wanaotengeneza/kuzalisha katika maeneo ambayo mafuta yanapatikana kwa urahisi(Kigoma,Mara,Mwanza,Morogoro na Mbeya).Na nguvu kazi(rasilimali watu) kidogo hutumika, pia uzalishaji wa sabuni hizi ni rafiki wa mazingira.

Namna ya utengenezaji/uzalishaji:
Chukua mgomba ulio vunwa ukate vipande vidogo vidogo kasha vianike hadi vikauke.Baada ya kukauka kusanya vpande vyote na uvichome moto,baada ya majivu kupoa yakusanye, kasha yaweke kwenye ndoo ya lita 20 yakiwa na ujazo wa lita/kilo 10 na uyaloweke kwa saa 24(siku moja),andaa mafuta yako pamoja na box la kutengenezea sabuni,ikiwa upo katika mchakato wa kutengeneza/kuzalisha hakikisha umeandaa ndoo ya ziada.

Kanuni(form)
Chukua majivu yaliyo lowekwa lita 1 na mafuta lita 1, lakini pia unaweza kuchanganya kiasi kikubwa(chochote) kwa uwiano huo kwa mfano majivu yaliyo lowekwa lita 20 na mafuta lita 20, changanya kwenye chombo kimoja anza kukoroga mpaka majivu na mafuta yachanganyike vizuri, kasha mimina kwenye box la kutengenezea sabuni baada ya saa 24 sabuni itakuwa tayari kukatwa, baada ya kukata anika sabuni kwenye sehemu yenye ubaridi isiyofikiwa na mwanga wa jua anika kwa muda wa siku 5-7 baada ya siku hizo sabuni yako itakuwa tayari kwa kutumika.
Pia unaweza kuweka rangi/manukato/virutubisho kama sabuni za viwandani na za magadi

Zaidi niandikie kileoseif@gmail.com
 
Nimesoma statement moja kwamba baada ya kutengeneza sabuni unapaswa uiache kwa muda wa wiki 8 mpaka 12
Sasa huu si muda mrefu?

Je, hakuna kuweka kwa muda mfupi?
Je, upatikanaji wa vifaa vya kutengenezea madukani?
 
Sabuni ipi hiyo ya mche ya maji?
Kama ni ya mche ikikauka tu ipo tayari kutumia, kwanini uiache muda wote huo?
 
Back
Top Bottom