Utengenezaji "White Sauce"

Jade_

Senior Member
Joined
Apr 19, 2015
Posts
122
Reaction score
214
Habari zenu, natumai mpo salama. Mara ya mwisho nilipika pilau na leo napika white sauce inayosindikiza pilau au chakula kingine chochote kinachohitaji mchuzi.

Kama kawaida ukitaka kuangalia video ya haya mapishi unaweza kuangalia hapo chini. Ukipenda unaweza “kuilike” hiyo video, “kusubscribe” kwenye channel yangu na kuangalia video nyingine.


Turudi kwenye mapishi yetu.

Nilianza kupika white sauce kwa kuyeyusha siagi kwenye sufuria ya moto jikoni. Baada ya siagi kuyeyuka kabisa nikakorogea unga wa ngano taratibu (unaweza ukatumia unga wa mahindi), halafu nikakorogea maziwa.


Siagi imeyeyuka


Nikikorogea unga wa ngano kwenye siagi


Nikikorogea maziwa

Baada ya hapo nikakorogea maji ya vuguvugu taratibu, na nikaendelea kukoroga mpaka mabonge yote yakaisha na nikaacha mchanganyiko uendelee kuchemka mpaka unga ukaiva na maji yakapungua mchuzi ukawa mzito nikauweka pembeni.


Nikikorogea maji ya vuguvugu


Nikiendelea kukoroga mabonge yaishe


Mchanganyiko ukiwa jikoni unachemka

Kwenye sufuria nyingine nilikaanga kitunguu kwenye mafuta ya mzaituni (olive oil). Vitunguu vilivyolainika niliweka pilipili manga nikaendelea kukaanga kidogo. Baada ya hapo nikakorogea ule mchanganyiko wetu wa mwanzo nikaucha uchemke kidogo.


Nikikaanga kitunguu kwenye olive oil


Nikikaangia pilipili manga kwenye vitunguu


Nikikorogea mchanganyiko wa mwanzo kwenye vitunguu


Mchanganyiko ukiwa jikoni unachemka

Kufikia hapo white sauce ilikuwa tayari na nikaiweka kwenye kibakuli kidogo ili kuila na pilau. Unaweza ukaweka viungo vingine mbalimbali kwenye white sauce ili iwe na ladha unayoipenda wewe.


Nikiweka white sauce kwenye bakuli


White sauce kwa ukaribu
 
Habari zenu, natumai mpo salama. Mara ya mwisho nilipika pilau na leo napika white sauce inayosindikiza pilau au chakula kingine chochote kinachohitaji mchuzi.


White sauce kwa ukaribu
Naonaga kwenye picha insta, nimeongeza kitu.
 
Kuna Mgahawa niliwekewa sijui walitia viungo vingi, nilipoteza funguo siku 3 🥲
 
Kuna Mgahawa niliwekewa sijui walitia viungo vingi, nilipoteza funguo siku 3 🥲
Nimecheka mpaka nimepaliwa. Pole sana mkuu. Migahawa mingi vyakula vyao... mhmmm...Mungu anajua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…