UTENGUZI: Rais Samia awatumbua Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TASAC, Posta na Posta Masta. Avunja Bodi ya Wakurugenzi Posta

Hahahaaaa.... Mzee wa Mombasa Renatus Mkinga!
 
Mbona wote hao ni wasitafu,
Msigwa bado yupo Ikulu?
 
Mbona wote hao ni wasitafu,
Msigwa bado yupo Ikulu?

Website ya TASAC mpaka leo tarehe 4 May 2021 inaonesha kuwa hao ni wajumbe wa bodi. Rejea linki Wajumbe wa Bodi |Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania na kama ni wastaafu inaonesha jinsi TASAC ilivyo na uzembe katika ku update taarifa zao za mtandaoni na kutia shaka kama kampuni hii ya umma inaweza kuwasiliana na wateja wao ki- dijitali kuendesha shughuli zao kwa ufanishi na kiushindani.

Soma zaidi.

Wasiliana Nasi​

Kurasa za Karibu​

Tovuti Mashuhuri​

Ungana nasi kupitia​

©2021 TASAC . Haki zote zimehifadhiwa.
Imesanifiwa, Imetengenezwa, na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) na Inaendeshwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania
Source : Wajumbe wa Bodi |Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania
 
Renatus Mkinga alitumia fursa vilivyo ya kuropoka mpaka akapata kuaminiwa na Mwendazake.

Mimi ni kati ya wasiokubaliana na ushawishi wake kwa Mwendazake kuirudisha TASAC iliyokuwa NASACO. Ni upuuzi Serikali ku deal na clearing ya mizigo bandarini
 
Ila cccm inaumiza sana hii Nchi sasa vibabu kama hivi vitakuwa na jipya gani kusaidia Shirika

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Hapo kwenye posta wamenigusa shirika linaendeshwa kizamani sana yani wamekosa kabisa kuendana na teknolojia na hali ya sasa.tatizo lingine wateja kupotelewa na mizigo/parcels zao.
Hapo umesema. Na hili ni tatizo kubwa sana na wateja wamelalamika bila tatizo kushughulikiwa.

Kwa vyovyote vile hili la kupotelewa parcels ni lazima lipatiwe ufumbuzi kwanza.
 
Nchi hii hata ateuliwe malaika, ataiba tu......kinachofanyika ni kubadilisha muonekano wa chupa tu ila mvinyo ni uleule tu
Mkuu mbona unaongea kama umemuona huyo Malaika?

Na kama Malaika tuliomsoma kwenye vitabu vya dini hawezi kufanya kwa akili kama ya binadamu ya wizi.
 
Shirika limejaa wazee tupu hakuna ubunifu
17 June 2020

TPC) LATOA TAARIFA YA MAFANIKO NA MATARAJIO YA SHIRIKA KWA MWAKA 2019/ 2020​



Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mafanikio na matarajio ya shirika hilo, kwa mwaka 2019/2020, mara baada ya Mkutano Mkuu wa Pili wa Mwaka, (2nd Annual General Meeting), jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, akisisitiza jambo

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, mara baada ya mkutano huo. Kulia waliokaa ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bibi Kitolina Kippa na Mwakilishi wa Msajili wa Hazina, Bw. Elikana Mtumweni. Aliyesimama kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu (TCRA), Bw. Wilfred Maro.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, katika picha ya pamoja na menejimenti ya Shirika la Posta Tanzania.

Habari kwa hisani kubwa ya: https://hakipensheni.blogspot.com/2020/06/shirika-la-posta-tanzania-tpc-latoa
 
Mbona wote ni wazee tu tena wenye sura nzito balaa palikuwa na ubunifu kweli hapo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…