FIBROIDS NI NINI?
Ni vimbe ambazo hutokea katika sehemu za uzazi wa mwanamke. Ni vimbe zinazotokea katika kizazi (uterus). Vimbe hizi hazimaanishi kuwa ni kansa. Zinatengenezwa na kambakamba zilizofungamana (muscle fibre) Fibroids huanza kwa ukubwa kama wa njegere, lakini huweza kukua kwa ukubwa wa tikiti maji. Inakadiriwa kwamba asilimia kati ya 20-50% ya wanawake wana hili tatizo au watakuwa na hili tatizo katika kipindi Fulani cha maisha yao. Fibroids hupatikana zaidi kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 30-40 na hupungua ukubwa mara baada ya umri wa utu uzima. Uchunguzi uliofanyika huko Marekani unaonesha kwamba Fibroids huwapata wanawake wa Kiafrika mara tisa zaidi ya wanawake wa kizungu.
Nini kinachosababisha Fibroids?
Ingawa sababu/chanzo hasa cha Fibroids hakijulikani, utafiti unaonesha kwamba fibroids huchochewa na oestrogen mwilini. Mara nyingi fibroids hukua kwa mwanamke pale ambapo kiwango cha oestrogen kimeongezeka mwilini, na pia fibroids hupungua pale ambapo kiwango cha oestrogen nacho kikipungua.
Oestrojen ni nini?
Ni mkusanyiko wa homoni ambazo ndizo zinazoukuza mwili wa mwanamke kijinsia, mfano ukuaji wa viungo kama matiti na kupata hedhi.
Pia wanawake ambao wana uzito zaidi ya kg.70 wana hatari kubwa zaidi ya kupata fibroids, pia hii ni kutokana na kiwango kikubwa cha oestrogen katika umri huu. Wakati wa zamani fibroids ingeweza kusababishwa na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango. Hii ni kwa sababu vidonge hivi vilikua na kiwango kikubwa cha oestrogen. Lakini kwa hivi sasa vidonge hivi vya uzazi wa mpango havina kiwango kikubwa cha oestrogen kama ilivyokuwa hapo awali.
Aina za Fibroids
Fibroids zinatofautishwa kutokana na sehemu ambapo imetokea. Yapo makundi mawili yanayoweza kugawanya aina za fibroids.
1) Fibroids zinazotokea ndani ya mji wa mimba,
2) Fibroids zinazotokea kwenye kuta za nje ya mji wa mimba.
Dalili za Fibroids
Inakadiriwa kwamba, asilimia 75% ya wanawake wenye fibroids hawana dalili zozote na wala hawajui kama wana fibroids. Kuweza kujua dalili za fibroids, inategemea na ukubwa wa fibroid na wapi zilipo kwenye kizazi. Hii pia inachangia aina ya dalili atakazopata mtu. Mfano: Fibroid ndogo ambayo ipo kwenye kuta za kizazi haitakuwa na dalili sawa na Fibroid kubwa inayoota kuelekea nje ya kizazi. Dalili kubwa inayofahamika ni ile ya kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi. Dalili nyingine ni kama maumivu ya tumbo, inaathiri mfumo wa haja (kubwa na ndogo), kuhisi mkojo mara kwa mara, mkojo kutoka kidogokidogo/kuvuja, mkojo kushindwa kutoka kirahisi, kukosa choo (constipation), kuwa tasa (kutoshika ujauzito), maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Fibroids na Ujauzito
Fibroids zinaweza kusababisha matatizo yafuatayo kwenye ujauzito:
1. Kuharibika kwa mimba/ujauzito
2. Inachangia kwa mwanamke kutoshika mimba kutokana na kubanwa kwa mirija ya uzazi.
3. Pia kutokana na msukumo unaosababishwa na fibroids, mirija ya uzazi hubanwa na hivyo kushindwa kupitisha mayai kuelekea kwenye kizazi (uterus)
4. Mwanamke anapokuwa mjamzito na pia akawa na fibroids kwa wakati huo, mwili unaweza ukasitisha kupeleka damu kwenye fibroids na kuifanya fibroid kusinyaa. Kama hili likitokea husababisha maumivu makali ya tumbo, na pia kufanya kizazi kutanuka na kusinyaa, baadae mimba huweza kutoka kabla ya wakati wake.
5. Wakati wa kujifungua, kama fibroid itakuwa kwenye njia ya kutolea mtoto inaweza kusababisha damu nyingi kutoka, au ikishindikana mama hufanyiwa upasuaji ili kumtoa mtoto.
Utaweza vipi kugundua kama una Fibroids?
Kama hakuna dalili inawezakana tu kwa kufanya vipimo. Dalili zikiwepo na kuhisi unalo tatizo la fibroids, mwone daktari kwa ajili ya kupata vipimo ili kujua kama una fibroids au la.
Vipimo vya Fibroids
Daktari huweza kufanya uchunguzi kwa vipimo kati ya hivi vifuatavyo:-
- Ultrasound scan (Mionzi)
- Hysteroscopy (kifaa kidogo ambacho huingizwa kwenye kizazi kupitia sehemu ya uke (vagina)
- Laparoscopy (upasuaji wa sehemu ndogo ya tumbo pamoja na kuwekewa kifaa kidogo sehemu ya uke (vagina)
Kuishi na Fibroids (wanavyoshauri hospitali)
Njia iliyozoeleka ya kuishi na fibroids zinazotoa damu nyingi ni kuzilinda na si kuzitibu. Utashauriwa kupata uangalizi/uchunguzi wa mara kwa mara lakini bado utahisi unahitaji msaada zaidi kwa jinsi unavyojisikia
Matibabu ya Fibroids (Hospitali)
Zipo njia kuu mbili za kihospitali za kutibu fibroids:-
1. Kutumia dawa (drug treatment)
2. Kufanyiwa upasuaji (surgical procedures)
1. Kutumia Dawa
Mkusanyiko wa dawa zijulikanazo kama GnRH analogues hupunguza kiwango cha oestrogen mwilini na hivyo kusababisha fibroid kusinyaa. Uchunguzi unaonesha kwamba dawa hizi zikitumika kwa miezi sita hupunguza ukubwa wa fibroid kwa asilimia 50%. Pia dawa hizi husitisha mzunguko wa mwezi (hedhi). Inashauriwa kwamba matumizi ya dawa hizi (GnRH analogues) yasitumike zaidi ya miezi sita kwani dawa hizi huweza kuleta madhara makubwa. Pia mara baada ya kuacha kutumia dawa hizi, wiki chache baadae fibroids huanza kukua tena, na mwanamke huanza kupata hedhi tena kama awali, ikiambatana na maumivu makali. Kwa baadhi ya wanawake huwa hawapati tena hedhi hadi kifo.
2. Kufanyiwa upasuaji
Upasuaji unahusisha mambo yafuatayo:-
- Kuiondoa fibroid yenyewe na kuacha kizazi(Myomectomy)
- Kukiondoa kizazi kabisa (Hysterectomy)
- Kuzuia damu kwenda kwenye fibroids (Uterine artery embolisation)
Ipo njia ambayo haijazoeleka sana, ambayo mtu huchomwa sindano nne tumboni zikielekea ilipo fibroids kwa ajili ya kuiua kwa kemikali maalum.
Hii ni elimu nzuri kwa ajili ya afya yako pia usiwe mchoyo uipatapo mshirikishe na mwingine aweze kupata uelewa. Kwa msaada pia kuepuka hali hiyo kukupata kuna food supplements ambazo zipo.