Utetetezi wa Sabaya, haupo kisheria, na pia unavunja kanuni za Kijasusi

Unajuaje hajarikodi??

Mnamfanya Sabaya mjinga sio?? Mnadhani amekurupuka kutumia hiyo karata aliyoitumia???
Kama ushahidi wake huu utakidhi vigezo vya ushahidi kisheria, basi si tu hautamsaidia kumwokoa na hukumu iliyo mbele yake....

Bali utaibua mambo mengine mabaya zaidi dhidi ya serikali ya Magufuli na huyu aliyepo na itakuwa silaha muhimu na hatari kwa wapinzani wa serikali....
 
Walitakiwa wamshitaki kwenye mahakama ya kijeshi lakini wamefanya kosa mamlaka kumpeleka kwenye mahakama ya kiraia huku wanasiasa wakiruhusiwa kumkejeli wakati mamlaka wakijua kwamba kile alichokuwa akikitekeleza kiliidihinishwa na wao kwahiyo hapo hakuna cha kutunza siri tena. Tambua usalama wako tayari kwa lolote watakalo kabiliana nacho wakati wakitekeleza majukumu waliyotumwa siyo kwa mtindo walioamua mamlaka kumdhalilisha kisa kuwafurahisha watu fulani ambao hata hivyo hazingatii kama kuna haki yoyote inatendwe.

Mamlaka za uteuzi huwa hazifi ila mtu hufa.....shughulikeni na mamlaka ya uteuzi ambayo bado ipo pamoja na kwamba mtu kabadilika.

Rejea "Rais Hakosei"-SSH ila mtumwa ndio hukosea!!!! Maajabu ya DUNIA ya SABA
 
Wanaomchukulia Sabaya poa nawashangaa hahahah
 
Ndio tatizo la kuchukua kila uvccm eti ni Tiss ndio madhara yake haya sasa wanaropoka kwa vile hawakupikwa kiweledi kwa Kazi hizo Ili wasiache alama
 
Kama ni kweli Ole Sabaya ni TISS Agent kama inavyosemekana japo Mimi nitakuwa wa mwisho Kuamini basi atakuwa ni miongoni Wana Usalama wa Taifa Wapumbavu kuwahi Kuajiriwa hapo.

Na hata hao waliofanya Recruiting yake nao watakuwa ni Wapumbavu maradufu na wangetakiwa hata wawe wameshakuwa Executed kabisa kwani wameiaibisha Taasisi ambayo Kimsingi inatakiwa kuwa na Watu Weledi na wenye Maadili ya hali ya juu sana.
 
Tunajuaje kama amefanya hivyo purposely ili chama ki-act???

Tunadhani Mheshimiwa Sabaya kule ndani amekaa tu na hafanyi harakati zozote juu ya hili??

Time will tell
 
Kulikuwa na ulazima wa kumpeleka Mahakamani ili baadhi ya mambo yafanikiwe.
 

Basi tufanye ataombewa msamaha na mke wa marehemu kama wale wa kapinga.
 
Alifanya uhalifu na anastahili kupata alichokitafuta

Kama ni mission ya Pesa bandia - basi angefocus kwenye mission na siyo kuteka watu nyara
 

Angekuwa huko, hii kesi isingekuwepo. Kazi maalum huwa haisemwi popote hususan mahakamani. Unatumika; mambo yakiharibika, unaishia kuwa “fall guy” - unapotea Kimya kimya. Waliokutuma hamjuani tena. Asubiri msamaha wa Rais.
 
Government moves on paper. Hata iwe operesheni kubwa kiasi gani na sensitive sana, lazima ita exist kwenye paper somewhere, sema itakuwa n Top top secret. Ukiona unapewa maagizo kwa simu, hiyo si operesheni halali. Utetezi wake hauna mashiko. Hana uthibitisho wowote wa kutumwa
 
Wangeweza kumchunia, mbona abuse of office watu wengi tu walifanya. Inawezekana alivuka mipaka, na ndio katolewa kafara hivyo

Nimejiuliza sana. Naona kuna wazito huko CCM/serikalini Sabaya aliwatibua sana enzi za Magufuli.

Hawa watu kwenye kulipa kisasi huwa hawajali aibu. Sasa Ofisi ya Rais (kama taasisi) inachafuka na uharaka wa katiba mpya ndio unazidi kudhihirika ili kuondokana ujinga wa aina hii mapema iwezekanavyo.
 


Ndivyo maelezo yake mahakamani yanavyomtambulisha.

Sasa aliagizwa afanye hayo yeye Kama Nani, maana kazi za DC zinafahamika,
 


Ikiwa ni hivi na Hana ushahidi kazi anayo
 
Huu umeandika ni UPUUZI MTUPU.
 
Okey.

Ila Sabaya na wote wanaohusika wnajua wanalolifanya
Wewe mbona huna hoja unaruka ruka tu, Ilhali unakwepa uhalisia na hoja yw msingi kuwa jamaa amevunja sheria kwa kufanya uhalifu hata kama ni kweli ametumwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…