Rakhshan Ally
New Member
- Sep 14, 2021
- 2
- 1
Utetezi,ni mchakato wa kupata msaada mkubwa kwa sababu fulani au sera fulani yaani kuwapa watoto wa mitaani sauti kwa kuwataka wawe na nguvu na ushawishi wachukue hatua ili waweze kujitetea na kuhakikisha kuwa wanasikilizwa matatizo yao katika jamii.
Kazi yetu ya utetezi inashirikiana na watu katika kila kutoka kwa familia na jamii hadi serikali za kitaifa hadi mashirika ya ulimwengu kama umoja wa mataifa (UN).
Zipo sababu nyingi zinazosababisha kuwa na watoto wamitaani ikiwemo kufiwa na wazazi na ndugu wengine waliobakia kuwakataa kuwalea,kupewa manyanyaso na familia zao ikiwemo kunyimwa chakula ,kupigwa na hata kuchomwa moto na pia kutokupatiwa malezi mazuri na wazazi.Hivyo ni vizuri kuwapa watoto malezi bora ili tupunguze watoto wa mitaani.
NJIA ZA KUTUMIA ILI KUPUNGUZA NA KUPATA HAKI ZA WATOTO WA MITAANI.
Tunaamini kuchukua njia ya haki za watoto kwa utetezi,hii inamaanisha kwamba tunatambua na kusisitiza kuwa watoto wa mitaani wana haki sawa na kila mtoto mwenginena kwamba wanapaswa kushiriki katika kufanya maamuzi juu ya kile kinachotokea katika maisha yao.Mahali pa kuanza kwa njia zetu ni÷
Kutumia mkataba wa umoja wa mataifa (UN)juu ya haki za watoto. mkataba wa haki za binadamu uliosaini zaidi katika historia mkataba unaeleza haki ambazo watoto wote wanazo bila ya kujari asili zao au hali zao.haki hizo ni kama kupewa ulinzi kutokana na vurugu,unyanyasaji na kupuuzwa,kupewa elimu inayowawezesha kutimiza malengo yao,kupata matibabu pindi wanapokuwa wagonjwa,kupewa malezi bora kama watoto wengine na wapewe nafasi ya kutoa maoni yao na kusikilizwa.
Kuweka watoto wa mitaani katika ajenda za ulimwengu.Tunaamini kwamba taasisi za kimataifa kama umoja wa kimataifa(UN) zinajukumu muhimu katika kusukuma maendeleo kwa watoto katika kiwango cha kitaifa.Wanatakiwa kutoa mapendekezo yanayofaa kusaidia nchi kuboresha sheria, sera na huduma zao na kushikilia serikali kuwajibika wakati hawatimizi wajibu wao wa haki za watoto wa mitaani.
Kuimarisha utaalamu wa mtandao wa ujasiri katika utetezi.consortium for street children (CNS) ni mtandao ambao unawasaidia watoto wa mitaani.Wana mipango kadhaa ya kuimarisha na kutetea haki za watoto wa mitaani,CNS inachapisha majalida na vitabu kwa lugha kiswahili, kiingereza,kirusi,kihispania,kihinfi,kichina,kifaransa na lugha nyingine nyingi ili watu dunia nzima tuweze kusoma na kujua haki za watoto wa mitaani.
Mwisho wa yote japo mimi nimezielezea njia hizi kwa kifupi najua zipo njia nyingi mbalimbali ambazo ni salama kuzitumia kwa maisha yao ili tuweze kupunguza na kuondosha kabisha wimbi la watoto wa mitaani na kuwafanya waishi maisha yao kwa furaha na amani.

Upvote
1