Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #441
Lulu ana mwili mdogo sana ukilinganisha na Kanumba. Je alitumia nguvu gani kuweza kumsukuma Kanumba hadi aanguke?
Kwa sababu walikuwa wawili chumbani basi mtu pekee ambaye anaweza kusema kilichompata Kanumba ni Lulu mwenyewe hata kama kitakuwa cha uongo na hakutakuwa na mtu wa kuthibitisha kuwa ni uongo. Kanumba angekutwa amejeruhiwa kwa kutumia silaha, hapo Lulu angekuwa hana la kujitetea.
Tuiachie mahakama ifanye kazi yake.
Jamani tuwe na busara kidogo, huu umoja wa wasanii mimi binfsi ninashangaa sana, msanii mwenzao Lulu amepata matatizo wapo kimya hata kumsaidia hawataki sijui kwa nini.
Kwa mtizamo wangu ninaona Lulu kuna uwezakano mkubwa akaachiwa huru, kwani mpaka sasa sioni kama kuna ushahidi wowote wa kuweza kuthibitisha tuhuma zinazomkabili
- Ripoti ya madaktari, kimsingi ripoti hii inamjenga zaidi Lulu kuliko upande wa mashitaka Prosecution kwa sababu ripoti hii inaeleza kwamba Mwendazake (Kanumba) kifo chake kimesababishwa na Brain Concussion ambayo inasababishwa na kugongwa na kitu kichwani, majeraha pamoja na kuanguka. This is undisputed facts all we do concur after having read the named report. Lakini haisemi kama Lulu ndio aliyemsukuma ama gonga kichwani marehemu, bado haiweza kuinganisha name alimgonga au mwangusha marehemu, uchunguzi inabidi uende mbali zaidi kuweza kupata ushahidi pasipo shaka/zaidi ya ukomo wa mashaka to prove beyond any reasonable doubt wa kwamba Lulu ndiye aliyemsukuma au mwangusha Kanumba kwa tunakubaliana ripoti ya polisi haiwezi kusisima peke yake kwa hiyo tunaipiga chini/tupa huko!.
- Ripoti ya madaktari haikwenda mbali kuweza kubaini kumbukumbu ya marehemu kama kuna magonjwa mengine yalikuwa yanamsumbua marehemu kabla ya kumkuta mauti, kwani hayo ndio yanaweza kuwa ndio sababu ya kifo chake tunapiga tena chini ripoti ya madaktari.
- Ripoti ya mkemia mkuu, hata ikisema kulikuwa na sumu, lazima atafuta nani aliiweka hiyo sumu na sio kumsingizia Lulu, vile vile lazima iseme ni sumu ya aina gani na ina uwezo gani wa kuua, je ni kwa muda mfupi namna ile, lakini Kanumba kuwa na sumu sio sababu ya kumfunga lulu kwa sababu inategemeana na sampuli ya machozi au aina yeyote (specimen), imechuliwaje kwa sababu yawezekana hiyo sampuli imechanganyikana na vipondozi anavyotumia marehemu kama mafuta, lotion n.k kwani wazi vipondozi hivi vina sumu kwani kuna wakati TFDA walitangaza vipodozi vyenye sumu, huenda watanzania wengi wana sumu mwilini mwao ndio maana leo kuna dawa za kutoa sumu mwilini, yawezekana hata wewe au mimi tuna sumu.Nayo ripoti tunapiga chini.
- Tunakuja kwa polisi hapo ndipo tuna rise doubt mpaka mheshimiwa hakimu ashangae kwanza kwa nini mdogo wake na Kanumba hakuwekwa chini ya ulinzi, kwani best practice tunao kwamba mtu akifa watu wote kwenye tukio mnakuwa watuhumiwa, na kama haukuhusika ni baadaye huko mwishoni ndio unatoka, lakini leo tumeona from day one mdogo wake Kanumba yote nje na ana mislead investigation kwenye media. Je hivyo vinywaji ambavyo vinaweza kutumika kama vielelezo vilichukuliwa kwa utaratibu yaani shihidi ni nani(independent witness/shahidi huru) ie mwenyekiti wa serikali za mitaa, mjumbe kama hakuwepo tunavipiga chini. Kwani mdogo wake haiwezekani amuwekee sumu kaka mtu tumeona matukio kibao ndungu wanauana. Kumbuka vinywaji hivyo Kanumba alikuwa anavnywa kabla possible mtu mwingine akawa amemuwekea. Vile vile polisi hawakumkamata Lulu alienda mwenyewe polisi hii ni ushahidi tosha kwamba alikuwa hana nia ya kuua, vile vile yeye ndiye toa taarifa kwa mdogo wa marehemu na kutoa ushirikiano.
- Caution or plain statement ya polisi tunaipiga chini, regardless imechukuliwa chini ya kiapo kama kuna vitu amekiri (confess) basi tunaamsha taratibu za kukiri lazima awepo mlinzi wa amani tofauti na hapo tunapiga chini.
- Ni nani alimwita mwenziye kati ya Kanumba au Lulu kama ni Kanumba alimwita aende nia ya kuua tunaitilia shaka, siku zote mwenye nia ya kuua haitwi anakuja mwenyewe na kutekeleza azma yake.
- Kuna ushahidi gani kwamba Lulu alikuwepo chumbani kwa Kanumba, ushahidi wa mdogo wa kunumba unapigwa chini kwa sababu kimsingi nay eye anatakiwa awe mtuhumiwa na vile vile ana maslahi kwa marehemu(bias/interested).
- Mwili wa marehemu umezunguka sana kabla ya polisi kuanza uchunguzi kiasi kwamba umebadili mwelekeo wa uchunguzi makini, kwanini polisi hawakuweza kufika eneo la tukio na kuzuia kwa ajili ya uchunguzi na kuchukua taarifa mbalimbali ie finger prints za maeneo mbalimbali kama vitasa, glass, chupa za vinywaji n.k
- Baada ya hapo tunakuja na defence ya kwamba Marehemu alitaka kubaka mpendwa wetu Lulu kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 132 (Penal code contray to Sect 132.)
- 132. Attempted rape Act No. 4 of 1998 s. 8
(1) Any person who attempts to commit rape commits the offence of attempted rape, and except for the cases specified in subsection (3) is liable upon conviction to imprisonment for life, and in any case shall be liable to imprisonment for not less than thirty years with or without corporal punishment.
(2) A person attempts to commit rape if, with the intent to procure prohibited sexual intercourse with any girl or woman, he manifests his intention by
(a) threatening the girl or woman for sexual purposes;
(b) being a person of authority or influence in relation to the girl or woman, applying any act of intimidation over her for sexual purposes;
(c) making any false representations for her for the purposes of obtaining her consent;
(d) representing himself as the husband of the girl or woman, and the girl or woman is put in a position where, but for the occurrence of anything independent of that person's will, she would be involuntarily carnally known.
(3) Where a person commits the offence of attempted rape by virtue of manifesting his intention in the manner specified in paragraph (c) or (d), he shall be liable to imprisonment for life and in any case for imprisonment of not less than ten years.
- Lulu ni girl or woman na tafsiri inapatikana katika sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 129A. Definition of woman
In this Chapter "woman" means any female person and, unless the context requires otherwise or it is otherwise expressly provided, irrespective of age.
- Mwisho, na ikumbukwe kwamba kazi ya mtuhumiwa ni kutia shaka juu ya hoja zinazotolewa na upande wa mashitaka, upande wa mashitaka una jukumu la kuthibitisha tuhuma pasipo acha shaka tuhuma inayo mkabili mtuhumiwa. Lulu hana hatia ila tu kwa mfumo wetu wa uendeshaji wa mashitaka huwa unachukua muda mrefu ndio ambayo itamgharimu. Na nyinyi maaskari wa kike ambao mnamsindikiza Lulu mahakamani naomba muwe mnampa ushauri na kumtia moyo msimtenge sana ni mwanamke mwenzenu.
Unajua kuna watu humu wamesoma Bsc (civil) Eng; na M.A (Public Admin) na ni watu wazima sana halafu wao ndo wanajiona Wanasheria waliofuzu kumbe wanapotosha umma.
Sheria ya mwenendo wa kesi ya kubaka ni tofauti sana na sheria ya mwenendo wa kesi ya mauaji.
Hebu twende taratibu, Lulu kashtakiwa kwa kosa la mauaji na wala si Kanumba kashitakiwa kwa "Tuhuma za Kusadikika" za Kubaka.
Sheria ya Tanzania inatambua umri tofauti kwa makosa tofauti. Mfano, katika kesi za kubaka ni offence kama ukimbaka mtu mwenye umri chini ya miaka 18.
Wakati huo huo sheria ya ndoa inatoa haki kwa huyu mtoto wa miaka 18 kuolewa kwa ruksa ya wazazi. Wakati Lulu na Kanumba enzi zao walikuwa wanapika na kupakua mama Lulu alikuwa anajua na kuwapa baraka zote. may be kwa kuwa naye aliona matunda yake. Nia ya Kanumba ilikuwa njema kabisa ni Kumwoa Lulu. Mama yake Mlezi Dotnata na Kanumba alifahamishwa hivyo na hata alipomwuliza Lulu kama ataacha Ukicheche aliahidi kuwa atatulia. Kanumba alikuwa anataka kum-transform abadilike. Lulu alikuwa ameiaminisha Dunia kwa matendo na maneno kuwa yeye ni mtu mzima above 18 (Achana na cheti, cheti ni nini bana), ushahidi wa watu wachache wakimshudia kuwa amekuwa akikiri kuwa na umri wa 18 na hivyo kumwaminisha kanumba na watu wengine kuwa yeye ni mtu mzima unatosha kumtia hatiani kama ni binti mwongo na asiyeaminika na hivyo ni mtu mzima ajibu mashtaka. Unajua kusema uongo ni kosa.
Sasa tuangalie umri katika kesi za mauaj: angalia kiambatanishi pia:
"mtu mzima" maana yake ni mtu mwenye umri wa au zaidi ya miaka kumi na sita;
"mtoto" maana yake ni mtu ambaye hajatimiza umri wa miaka kumi na sita;
"Kijana mdogo" maana yake ni mtu aliye chini ya umri wa miaka kumi na sita;
CHAPTER XIXA inazungumzia Murder and Manslaughter
195. Any person who by an unlawful act or omission causes the death of another person is guilty of the felony termed "manslaughter" An unlawful omission is an omission amounting to culpable negligence to discharge a duty tending to the preservation of life or health, whether such omission is or is not accompanied by an intention to cause death or bodily harm.
196. 'Any person who of malice aforethought causes the death of another person by an unlawful act or omission is guilty of murder.
197. Any person convicted of murder shall be. sentenced to death: (of course kuna exceptions)
Nimeongea na Kiongizi mmoja Police Force wa Kitengo cha Crime na haya ndiyo yaliyojili:
1. Ushahidi walionao wa awali unatosha kumshitaki Lulu kwa Murder kwa kuwa ni above 16
2. Bado kuna ushahidi mzito katika simu yake na SMS for last few weeks na huenda kesi hii ikawavuta wengi.
3. Report ya daktari inayoonyesha SK alikufa kwa Brain Concussion imepelekea Police kupata ushahidi wa kitu kilichomgonga, mpiga, au mwangusha wakati muda mfupi tu alikuwa mzima. Report inashuhudia SK hakuwa na maradhi mengine na alikuwa ni mtu wa Gym.
4. Report ya Mkemia Mkuu ambayo inasubiriwa inaweza kuwa na dondoo zingine.
5. Jukumu la mwendesha mashtaka ni kumshtaki mtuhumiwa kwa Murder (ambalo ni kosa la juu) ingawa mahakama kutegemea na uzito inaweza kumpunguzia adhabu ikawa Manslaughter (kosa dogo).
6. Elizabeth alikuwa Mlevi (Only over 18 unaruhusiwa kununua kilevi, alikuwa na mabwana kama alivyowahi kukubali mwenyewe kuwa hakuwa Bikra (na hao nao walikuwa wanambaka?). Yote haya yanahakikisha kuwa binti ni mtu mzima na anaweza kujibu tuhuma za mauaji.
7. Jamuhuri ikishamtia katika hatia kuwa Lulu ni Mwongo mbele ya jamii na kuwa kadanganya miaka na kuwaaminisha watu kuwa yeye ni mtu mzima, basi mziki mnene unamsubiri, maana mahakama tayari inaushahidi kuwa ni Mwongo na anatumia uongo kutake advantage. hapo Wanasheria wazuri au waendesha mashitaka watakuwa na kazi ya kumbomoa kwa kila analosema. Aombe tu yote atakayoongea hayatakinzana na aliyotenda na kufanya na ambayo yatakuwa na ushahidi.
8. Bra bra zingine kuwa Kanumba kabaka bila ushahidi wowote na hayupo kujitetea in nothing other than wishful thinking lakini sheria iko wazi.
Ni vema tuache kupotosha watu na tuiachie mahakama ifanye kazi yake.
Allien usipoteze muda na sifa za mleta mada wewe kazana kubeza khoja zake...........sifa hazina maana kama mada yenyewe hukubaliani..........................nayo na zina maana kama khoja zake wakubaliaana nazo.....................tafsiri zako zozote umezijenga katika msingi mmoja ya kuwa penal code is above all laws.........well, you are dead wrong.............the sexual offences act Cap 101 now supersedes penal code...................twende polepole tutakufikisha kwenye huu uchambuzi.......................kwa hiyo utetezi wa kubakwa lazima usikilizwe kabla ya tathmini ya tuhuma za mauaji.......................be blessed.
Wanasema si rahisi kuwa mtaalamu wa kila kitu...ila kila mtu anaweza kuwa informed lakini asijue technical know how. Mtoa hoja hii - @Ruta anashindwa kuelewa kuwa hakuna uhusiano kati ya umri na kosa nanalotuhumiwa kwalo.
Ni vigumu kutaka watu waamini kuwa ukiwa under 17 huwezi kutuhumiwa kufanya kosa katika nchi hii. Niseme swala si kuwa anapashwa kuwa huru au la...tumeona kesi ambazo ni damaging (Zombe, Vijana waliouawa na Polisi Arusha etc) kuliko hii ya Lulu. Ukweli ni kwamba Lulu anayotuhuma ya kujibu period.
Madam Ingekuwa vizuri kama ungewataja hao wanasheria. I don't see any room for technical discussions in a case which has not started. People need to hear arguments from both parties first. Kinachoendelea sasa ni what if and its legal implications in the future direction of the case.
Unajua kuna watu humu wamesoma Bsc (civil) Eng; na M.A (Public Admin) na ni watu wazima sana halafu wao ndo wanajiona Wanasheria waliofuzu kumbe wanapotosha umma.
Jamani inshu iko mahakamani mbona mmekuwa na jazba
kuweni wapole punguzeni jazba au nendeni mahakamani mkatoe utetezi wenu
LAKINI KWA HILI NI RAHISI TU kuhakiki, maana kuna Birth certificate, unless kama inawezekana kufoji cheti hicho kwa kupunguza umri!
Kati yenu wote hamna hata mmoja anayejua LULU alitoa maelezo gani kuhusu kesi inayomkabili,vile vile hatuelewi ushahidi wa awali unaviashiria gani ambavyo DPP atakua anavyo na ndiyo vilivyopelekea aamue kesi itajwe.Kwahiyo si sahihi kusema DPP ni bomu au Lulu hana kesi ya kujibu hadi pale tutakapokuwa na vielelezo vyote.hoja zako zinanisaidia kuthibitisha ya kuwa DPP ni bomu.......ilkuwaje amkamate Lulu wakati kumbe hata post-mortem ripoti haijakamilka, kumbe kuna hata mawasiliano ya simu hayajulikani yanasema nini na taarifa ya mkema mkuu haijulikani? Sasa DPP akiwa hana vielelezo hivi alifikiaje kumtia nguvuni masikini mtoto wa watu na kumfungulia makosa ya jinai wakati hana hata chembe ya ushahidi?
kwa khali hii hata wewe DPP anaweza sasa hivi kukutia ndani na kukufungulia kesi ya hii ya mauaji kwa madai anasubiria vielelezo muhimu kutoka kampuni ya simu, post-mortem report na ripoti ya mkemia mkuu...............Am very sad with the way this nation is heading..................yaani haki za raia zinachezewa kama za kuku ambaye uhai wake na uhuru wake uko mikononi mwa mbabaishaji yoyote yule kama huyu DPP............
ni vyema tiukaanza kuangalia haki za mtuhumiwa..........2day it Lulu 2morrow could be you.....................na kwa bahati mbaya hutakuwa unahushishwa na mauaji ya celebrity or a self-proclaimed number one Bongo movie superstar like mwendazake.............
Kabla ya kujadili mada hebu tuangalie kwanza sheria zinazohusu tuhuma, sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16 ( kifungu cha 195 – 205), The Penal Code chapter 16 (Sect 195-205), nimesikia kwa makini hati ya mashitaka ya Lulu (Charge sheet) inasema anatuhumiwa na kosa la kuua kwa kukusudia kinyume na kifungu cha 196(angalia chini) yaani Murder sect 196.
Kati yenu wote hamna hata mmoja anayejua LULU alitoa maelezo gani kuhusu kesi inayomkabili,vile vile hatuelewi ushahidi wa awali unaviashiria gani ambavyo DPP atakua anavyo na ndiyo vilivyopelekea aamue kesi itajwe.Kwahiyo si sahihi kusema DPP ni bomu au Lulu hana kesi ya kujibu hadi pale tutakapokuwa na vielelezo vyote.
If what you are saying is true then I think she is being overcharged and it will be a tall order for the prosecution to prove their case beyond a reasonable doubt.
Hakuna kinachoshindikana tia mguu vizazi na vifo, sitashangaa nikisikia death certificate inatoka bila marehemu :embarrassed1:
ni kweli mbumbumbu wengi wa shule tumewasukumia polisi hata mwanang u mmoja alikuwa shule ni kafupi infact mtoto wa baba mdogo wenzake walifanya fujo wakaenda kukamatwa walipofika kwake wakamuuliza hata wewe unafanya na ufupi wako unahisi utaishia langapi akasema la saba akaulizwa na polisi alafu uwe na nani na elimu yako
akasema nataka niwe polisi baada ya la saba huyu ni mtoto anajua kule wamejaa..........