barakandesambur
Member
- Jan 17, 2011
- 19
- 1
kaka umeona mbali utabiri wako sehemu kubwa utatimia cha ajabu kmbe lulu hajui umri wake ni mpaka vyeti ndo vinajua hii kesi ni danganya ***** tu watatuzugaaa then itaisha hii ndo tz bwanaaaa ina wenyeweee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Advocate RUTA
Hebu nisaidie hapa. LULU kaithibitishia dunia anamika 18, ukizingatia yeye ni Celebrity alipata coverage yakutosha kwenye media kuthibitisha hilo, magazeti yapo, clips za youtube zipo zikionyesha sherehe yenyewe na amahijano ya nini anaeleza na kutarajia baada ya kutimiza miaka 18
Ana drive anamiliki na kudrive mkoko inamaa na driving license anayo, je sheria za driving license zinasemaje?
Na hata ulikuwa ukimuuliza binafsi ana sema anamiaka 18.
Hebu nisaidie kisheria ikoje kama unakuja kukamatwa naye eti ni underage
Na katika kesi hii ina effect gani?
Ruta,
Nadhani wengi hawajaelewa mantiki ya unachozungumizia. Unachosema ni namna ambavyo Lulu anaweza kuchomoka endapo atasema vile ulivyojenga ushahidi wako. Siku zote wakili yoyote huamini utetezi wake ndio bora zaidi. Ni kazi ya mahakama kupima utetezi na kutoa hukumu. Kithibitisho official cha umri wa mtu ni cheti halali cha kuzaliwa-haya mambo ya birthday, Tv interviews, sijui nini hayo ni kachumbari tu- mahakama haiwezi kupokea picha za birthday na mahojiano kama kielelezo wakati cheti cha kuzaliwa kipo. Mimi huwa nahesabu mwaka mpya kila napoingia mwaka mpya, bila kujali tarehe na mwezi wangu wa kuzaliwa umefika, mfano kama nimezaliwa 13 September 1986, basi ilipofika 1/1/1987 nilijihesabu nina mwaka mmoja.
Kama mngebahatika kuwasikia baadhi ya polisi wa Oysterbay wanaohusika na kesi hii, au mama mwenye nyumba aliyopanga SK, marafiki wa karibu wa Kanumba, mdogo wake SK na Lulu mwenyewe nadhani mtazamo wenu juu ya hii kesi ungekuwa tofauti kabisa.
Kimsingi SK alikuwa na mahusiano yasiyofaa na Lulu, na siku zote jambo ovu haliwezi kuzaa jambo jema, mbona Polisi wanamfahamu huyo ''mheshimiwa'' aliye pia na mahusiano na Lulu, kwanini hawekwi hadharani?. Mimi mtazamo wangu ni kuwa kwa vyoyote vile Lulu hakuwa na NIA ya kumuua SK na nina uhakika haihitaji mwanasheria mwenye weledi wa Ruta kujenga hii hoja. Lulu hawezi kutoka jela leo atakaa hata miaka mitatu ili ''kumlinda'' na hasira za mashabiki wa SK
utetezi huu haumtoi kwenye kesi, sheria za ndoa Tanzania zinaruhusu binti kuolewa akiwa na miaka 14, sina uhakika kama zilishafanyiwa marekebisho. Ndiyo maana miaka ile kabla mwamko wa kwenda sekondary haujawa mkubwa mabinti walikuwa wanamaliza darasa la saba na kuolewa na ilikuwa ni kisheria kabisa.
Duh waitu Rutashubanyuma marehemu SK ww wamwita "MWENDAZAKE" ww ni nouma au ulikuwa una mind kiaina jamaa kubanjua HOTLULU(MRUDIZAKE)? Kama itathibitika kuwa SK aka MWENDAZAKE alimpombesha MRUDIZAKE(HOTLULU) hiyo inazidi kujenga utetezi kwa MRUDIZAKE. Natamani case hii igongwe mwanzo mwisho huku MRUDIZAKE akiwa kapewa dhamana tutapata Bonge la Precedent Bongoland. Hapo High Court wateu Judge mwenye kiu ya haki sio mteule wa ki- politic
Hakuna kesi ambazo naziogopa kama ya kubaka, kwani hata Wauzaji miili yao au mke wako unayelala kitanda kimoja akiamua kukupoteza anakupoteza. Hii Kesi kwa mimi siioni kama inauzito wa kufungwa huyo Binti kama akiyapangilia maneno yake na Ushahidi atakaotoa anaweza kumwagika uraiani na kuendelea na shughuli zake. Lakini Mahakama zetu za Tanzania haziaminiki na hazitimizi wajibu wake.
Mkuu
Huyu Dogo Janja atafungwa! Why?
1. Ameiaminisha Dunia Nzima kuwa ana miaka 18 including Kanumba
2. Dunia nzima itamshuhudia kuwa ni Mchafu
3. Live Video na Watangazaji wa TV watatoa ushahidi wa Mahojiano wa Ukware wake.
4. Picha zake za kimitego na ulevi zitadhihirisha uchafu wake (waliomuuzia pombe under 18 nao watafungwa?).
5. Dotnata ameshadhihirisha nia njema ya Kanumba kuwa alitaka Kumwoa na alikuwa na taarifa rasmi. Lulu alikubali na alisema tatulia lipotakiwa kufanya hivyo. Wamekuwa marafiki for 6 months na Kanumba hakutaka wawe in Spotlight mpaka atangaze Uchumba. Kuna wanaojua walikuwa wanapika na kupakua.
6. Mama yake atabomolewa mbali kwa malezi hafifu, rafiki zake watapondwa kuwa ni marafiki wabaya na wasiomshauri,
7. Sumu zake na SMS zake zimeshachunguzwa. Alikuwa na mpenzi mwingine kitu kinachoonyesha ukomavu katika tasnia ya Ngono (siyo Filamu) (Lulu atasema naye alikuwa anambaka?)
8. Lugha yake ya kejeli na mzaha itawatia hasira majaji maana hana staha, records zipo.
9. Alishawahi kupatikana na makosa mahakamani na kuhukumiwa kwa mwenendo mbaya na matusi
10. Jamii yenye hasira haimtaki ndo maana walivamia kituo cha polisi Oysterbay.
Mi si Mwanasheria, lakini Advocate Ruta una kazi ya ziada kama utetezi ni huo. hauna mashiko! Hana pa kutokea!
Hakuna kesi ambazo naziogopa kama ya kubaka, kwani hata Wauzaji miili yao au mke wako unayelala kitanda kimoja akiamua kukupoteza anakupoteza. Hii Kesi kwa mimi siioni kama inauzito wa kufungwa huyo Binti kama akiyapangilia maneno yake na Ushahidi atakaotoa anaweza kumwagika uraiani na kuendelea na shughuli zake. Lakini Mahakama zetu za Tanzania haziaminiki na hazitimizi wajibu wake.
Hyo iko waz hatakama atakutwa ana hatia lazma asote hata miaka nane hivi itakuwa safi.
kauli yake haina maana ulipaswa kujihakikishia anayoyasema ni kweli kama hata kuwasiliana na wazizi wake au utafute mbinu nyingine kupata uthibitisho..........ndugu yangy Paulss kutokuijua sheria siyo utetezi na hata kudai ulipotoshwa siyo utetezi..................ni kama mtu kajenga kwenye hifadhi ya barabara na bomoabomoa inamkuta anadai ya kuwa yeye hakujua hiyo ni hifadhi ya barabara au aliyemwuuzia kiwanja alimdanganya kwa hiyo aachwe aendelee kuvunja sheria kutokana na uzembe wake wa kutofanya utafiti wa kutosha wa kujihakikishia ya kuwa yuko kwenye mstari wa sheria.................
Mimi pia siyo Mwanasheria lkn nataka kuunga mkono hoja ya Allien kuwa utetezi wa Bwana Ruta hauna mashiko,anafikiria mambo kwa juujuu sana,anasahau kabisa kuwa technology siku hizi inaweza kurahisha mambo mengi tofauti na zamani...kwanza nikianza na suala la umri,nakumbuka mwaka jana tukielekea mwishoniX2 Lulu alifanya bonge la party ya birthday yake ya kufikisha miaka 18 na ndo hapo alipokuja na kauli mbiu ya kuwa yeye si "WATOTO SHOW" tena bali ni "WAKUBWA SHOW" sasa iweje leo hii arudie kwenye miaka 17 tena?!! nafahamu Wanasheria wake watakuwa wanamfunza namna atakavyoweza kuepuka mkono mkali wa sheria kwa kigezo cha kutofikisha umri wa ki'utu uzima lkn kama Washtaki watakuwa makini lazima watamtia hatiani tena kwa kosa lingine la kujaribu kudanganya umri hata kama watakuwa wametengeneza cheti kingine cha kuzaliwa kitakachokuwa kinamuonyesha ana miaka 17,trust me guys.
2. Suala la kukana kuwa Kanumba hakuwa Mpenzi wake halipo ksbb technolojia pia inaweza kulithibitisha hilo pasipo shaka yeyote kupitia mawasiliano waliyokuwa wakifanya siyo siku hiyo tu hata siku za nyuma, na katika hilo mawasiliano ya mtu na Mpenzi wake lazima yataonekana tofauti na yale ya mtu na Mbakaji wake, na si hivyo tu hata kitendo cha yeye kukiri kuwa Kanumba alikuwa ni Mpenzi wake na kisa cha ugomvi wao siku ile ni yeye kupokea simu ya Basha'ke mwingine siyo tu kinaondoa maswali katika hili bali pia kinaonyesha(kama alivyosema Bwn Allien) ni jinsi gani alivyokomaa katika tasnia ya ugawaji uroda usio na mpangilio.
3. Napenda kumkumbusha Bwana Ruta kuwa watakaotakiwa kuthibitisha kuwa Lulu alipigiwa simu na nani siyo marafiki zake ni Service provider(i.e Tigo,Voda etc) ambao mtandao wao ulitumika katika mawasiliano yale kwahiyo utetezi huu na wenyewe ni "0"
4. Tayari Madaktari wameshatoa report ya kiichosababisha kifo chake ambacho ni mtikisiko wa Ubongo kwa jina la kitaalamu inajulikana kama "brain concussion" na hii inaweza kusababishwa na mtu kijigonga kichwa sehemu ya nyuma,huwa haitokei tu mtu amekaa au amelala ubongo ukatikisika,wataalamu wanasema lazima kichwa kigonge sehemu fulani,sasa tukiunganisha na kukiri kwake kuwa walikuwa na ugomvi ndo tunapata taswira ya kuwa alimsukuma na kusababisha aliyekuwa Msanii wenu Nguli kuwa "Mwendazake"
Kwahiyo kwa mtazamo wangu mimi Dogo hawezi kukwepa mkono wa sheria,lazima atatiwa hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia ambalo definately litakuwa lina disqualify utetezi wa kuwa Kanumba ndiye alimpigia simu kumuita aende wakajadiliane vitu gani sijui.
I can bet kama sheria itaachwa ichukue mkondo wake Dogo haruki hata iweje.