Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad.

Akiongozwa na wakili Mosses Mahuna wakati akitoa utetezi wake mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Sabaya alidai yeye bado ni mtumishi wa Serikali ila alisikia tangazo la kusimamishwa kazi kutoka Kwa Rais Samia Suluhu.

Alidai kuwa siku ya tukio Februari 9 mwaka huu majira ya saa 9 kasoro alasiri alipigiwa simu na Mamlaka iliyomteua na kumpatia maelekezo ya kwenda kufanya kazi maalumu Arusha na kumtaka aongozane na watu wanne waliokuwa wakimsubiri uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro KIA.

Sabaya alidai kuwa walipofika Arusha wakiwa na wale watu wanne ambao ndio wenye taarifa zote walielekea eneo husika waliokuwa wameelekezwa na Mamlaka husika katika eneo la duka la Shaahid store lililopo mtaa wa Soko kuu jijini Arusha.

Akihojiwa na Wakili Mahuna kuhusu kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya tarehe 9.2.2021 ,Sabaya alidai alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani kilimanjaro na aliteuliwa na Rais Hayati Dkt John Pombe Magufuli tarehe 29.7.2018.

Lengai Ole Sabaya anaeleza mahakama kuwa alitumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 2 na miezi 10 na alikoma kuhudumu wadhifa huo tarehe 13.5.2021 baada ya Rais Samia Suluhu kutengua nafasi yake kupisha uchuguzi .

Sabaya ameieleza Mahakama kwamba baada ya kufikia katika duka hilo walimkosa Mmiliki wa duka na ndipo alipowasiliana na mamlaka iliyomtuma kazi hiyo, ambayo ilimjibu kwamba imeshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongozi na imeelekeza watu waliokutwa eneo la tukio wapelekwe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi ili kusaidia kupatikana Kwa mhusika wa duka aliyekuwa akitafutwa.

Anaeleza kuwa suala la yeye kupatiwa maelekezo na Mamlaka ya uteuzi ni Jambo la kawaida kwani miezi mitatu kabla ya siku ya tukio 9.2.2021 alipewa maelekezo ya kufanyakazi maalum na kubaini mtambo wa kutengeneza fedha bandia na kukamata fedha bandia sh,milioni 800 jijini Dar es salaam.

Sabaya anaeleza kuwa katika zoezi hilo alikuwa msimamizi mkuu ambapo Hata Gavana wa Fedha Prof Florian Luoga pamoja na aliye kuwa waziri wa Fedha hapa Nchini Dkt Philp Mpango ambaye kwasasa ndiye Makamu wa Rais wanalijua.

Sabaya amedai kuwa hajawahi kufikia katika duka la Shaahid Store na kupora kiasi cha sh, milioni 2,769,000 na kisha kumpiga human Jasim , Bakari Msangi, Salim hasani na Ally shabani na kuwatisha Kwa silaha na kwamba hamfahamu mshtakiwa mwenzake anayetajwa Kwa jina la Daniel Mbura na pia Silvester Nyegu hakuwa naye siku ya tukio.

Sabaya anaendelea kujitetea....

Huyu afunguliwe shtaka la ugaidi. Anataka kumchafua shujaa wetu
 
Kwahiyo UMEAMINI kwamba tulivyokuwa tunasema kwamba JIWE alikuwa anapora wafanyabiashara FEDHA? Si umeona JAMBAZI sabaya amesema ukweli mahakamani kwamba alitumwa na mamlaka ya UTEUZI? Haya tusisikie unamtetea tena JIWE.
Jiwe simjui kwa kesi hii mporaji Ni Sabaya sio Jiwe nisiemjua Ni sawa na kusema Chadema chama Cha Magaidi wakati gaidi Ni Mbowe
 
Ole Sabaaya ameshapotoshwa na wanasheria wake, kifungo kinam nyemelea huyu jamaa;

1) Amri Kutoka Kwa Wakuu Wake (Order From Higher Personnel) sio utetezi wa jinai (Sio Criminal Defence). Ni Heri hata angejitetea alikua amelewa kupita kiasi kwasababu Ulevi (Intoxication) inaweza kutumika kama Criminal Defence.

Hakuna defence katika jinai ya Kutimiza Amri Ya Kiongozi Wa Juu (Order From Higher Personnel). Hii haipo kwenye Penal Code CAP 16 na hata kwa wanajeshi haipo kwenye Marshall Codes & Laws.

Ref: Nurenmberg Trials and Nuremberg Codes.

Wanajeshi wa Nazi walitumia utetezi huo kujitoa katika hatia ya makosa ya jinai waliotenda dhidi ya binaadamu, walisema wao walitenda hayo mauwaji ila kwa kufuata na kutii amri za wakubwa zao jeshini. Ila mahakama ya kijeshi ya Nurenmberg ilikataa utetezi huo kwa hoja moja kuu "UNAPOPEWA ORDER NA MKUU WAKO YA KUFANYA JAMBO LINALOKWENDA KINYUME NA SHERIA AU HAKI ZA BINAADAMU, UNA WAJIBU WA KUKATAA KUTII ORDER HIO".

2) Ushahidi wa kumtaja mtu kwamba amekupa maagizo fulani kisheria unahitaji "CORROBORATION" ya ushahidi wa ziada kutoka kwa huyo mtu alietajwa. Magufuli hawezi kupatikana kwaajili ya kutoa ushahidi wa ziada ku-support na ku-confirm ushahidi wa Ole Sabaaya.

Kadanganywa na yule wa bukoba kisa cha mungu kuwa shaidi
 
Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad.

Akiongozwa na wakili Mosses Mahuna wakati akitoa utetezi wake mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Sabaya alidai yeye bado ni mtumishi wa Serikali ila alisikia tangazo la kusimamishwa kazi kutoka Kwa Rais Samia Suluhu.

Alidai kuwa siku ya tukio Februari 9 mwaka huu majira ya saa 9 kasoro alasiri alipigiwa simu na Mamlaka iliyomteua na kumpatia maelekezo ya kwenda kufanya kazi maalumu Arusha na kumtaka aongozane na watu wanne waliokuwa wakimsubiri uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro KIA.

Sabaya alidai kuwa walipofika Arusha wakiwa na wale watu wanne ambao ndio wenye taarifa zote walielekea eneo husika waliokuwa wameelekezwa na Mamlaka husika katika eneo la duka la Shaahid store lililopo mtaa wa Soko kuu jijini Arusha.

Akihojiwa na Wakili Mahuna kuhusu kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya tarehe 9.2.2021 ,Sabaya alidai alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani kilimanjaro na aliteuliwa na Rais Hayati Dkt John Pombe Magufuli tarehe 29.7.2018.

Lengai Ole Sabaya anaeleza mahakama kuwa alitumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 2 na miezi 10 na alikoma kuhudumu wadhifa huo tarehe 13.5.2021 baada ya Rais Samia Suluhu kutengua nafasi yake kupisha uchuguzi .

Sabaya ameieleza Mahakama kwamba baada ya kufikia katika duka hilo walimkosa Mmiliki wa duka na ndipo alipowasiliana na mamlaka iliyomtuma kazi hiyo, ambayo ilimjibu kwamba imeshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongozi na imeelekeza watu waliokutwa eneo la tukio wapelekwe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi ili kusaidia kupatikana Kwa mhusika wa duka aliyekuwa akitafutwa.

Anaeleza kuwa suala la yeye kupatiwa maelekezo na Mamlaka ya uteuzi ni Jambo la kawaida kwani miezi mitatu kabla ya siku ya tukio 9.2.2021 alipewa maelekezo ya kufanyakazi maalum na kubaini mtambo wa kutengeneza fedha bandia na kukamata fedha bandia sh,milioni 800 jijini Dar es salaam.

Sabaya anaeleza kuwa katika zoezi hilo alikuwa msimamizi mkuu ambapo Hata Gavana wa Fedha Prof Florian Luoga pamoja na aliye kuwa waziri wa Fedha hapa Nchini Dkt Philp Mpango ambaye kwasasa ndiye Makamu wa Rais wanalijua.

Sabaya amedai kuwa hajawahi kufikia katika duka la Shaahid Store na kupora kiasi cha sh, milioni 2,769,000 na kisha kumpiga human Jasim , Bakari Msangi, Salim hasani na Ally shabani na kuwatisha Kwa silaha na kwamba hamfahamu mshtakiwa mwenzake anayetajwa Kwa jina la Daniel Mbura na pia Silvester Nyegu hakuwa naye siku ya tukio.

Sabaya anaendelea kujitetea....

Utetezi wa kijanga sana. Hivi aliapa kwa katiba au aliapa kuwa chawa!
 
Duh!! Mungu anamuona lakini!

Amejitetea kiume sana

Makamu wa Rais Dr Mpango na DC mstaafu Dr Kihongosi watakuwa mashahidi wake muhimu kama katiba inaruhusu.

Rais mstaafu Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kumtetea Prof Mahalu pale Kisutu!
Kiume gani?. Ni vile tu ni kwa nchi kama hii sheria zinapindishwa tu kwa maslahi ya watu fulani fulani. Lakini kiuhalisia ukiwa na akili timamu huwezi kutumwa tu hata iwe na mkuu wako wa kazi kufanya kazi ya kupora watu,kunyang'anya na kupiga na kutishia siraha au kufanya vitendo vyovyote vya uharifu na wewe ukakubali. Vinginevyo ukatae na ujiuzuru. Ona kama sasa hata kama umetumwa lakini mahakamani unasimama na kujibu wewe kama wewe ulietenda
 
Kuweka kumbukumbu sawa Marehemu Mzee Pombe hakumpigia simu Sabaya na kumuambia eti aende Dar kufanya kazi maalum ya kusaka mtambo wa kuchapisha pesa feki, ni polisi wa Hai walikamata pesa feki hapo Hai wakamtaarifu Sabaya wakawabana watuhumiwa na kusafiri nao kwenda Dar mpaka wakaonyesha mtambo wao wa kuchapisha pesa bandia.

In short Sabaya jambo lolote linalohusu PESA liwe la halali au haramu ilikua lazima atahakikisha anashiriki kwenda phisical eneo husika hata kama sio eneo lake la kazi au hata kama ni jukumu la taasisi nyingine.
 
Ukipitia hukumu ya Zombe ( RPC mstaafu) kwenye ile kesi ya wale jamaa wa madini utagundua Sabaya ana nafasi kubwa ya kuachiwa huru!
 
Kuweka kumbukumbu sawa Marehemu Mzee Pombe hakumpigia simu Sabaya na kumuambia eti aende Dar kufanya kazi maalum ya kusaka mtambo wa kuchapisha pesa feki, ni polisi wa Hai walikamata pesa feki hapo Hai wakamtaarifu Sabaya wakawabana watuhumiwa na kusafiri nao kwenda Dar mpaka wakaonyesha mtambo wao wa kuchapisha pesa bandia.

In short Sabaya jambo lolote linalohusu PESA liwe la halali au haramu ilikua lazima atahakikisha anashiriki kwenda phisical eneo husika hata kama sio eneo lake la kazi au hata kama ni jukumu la taasisi nyingine.
Kwanini alikuwa hakamatwi?
 
Ngoja gavana wa Bot Luoga apande kizimbani kumtetea!
Kumbuka utetezi wa Luoga na Philip Mpango ambao anautaja Sabaya ni kuhusu yeye kushiriki kusaka na kukamata mtambo wa kuchapisha pesa bandai baada ya kuwakamata wahalifu waliokua wakiuza pesa bandia huko Hai.

Amewataja hao kina Luoga na Mpango akiamini anatengeneza uhalali kuwa yeye ni kawaida kufanya kazi za kipolisi nje ya wilaya yake 🤣

Haihusiani na hii ya kuvamia duka la muarabu, Sabaya anawachanganyia maneno.
 
Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad.

Akiongozwa na wakili Mosses Mahuna wakati akitoa utetezi wake mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Sabaya alidai yeye bado ni mtumishi wa Serikali ila alisikia tangazo la kusimamishwa kazi kutoka Kwa Rais Samia Suluhu.

Alidai kuwa siku ya tukio Februari 9 mwaka huu majira ya saa 9 kasoro alasiri alipigiwa simu na Mamlaka iliyomteua na kumpatia maelekezo ya kwenda kufanya kazi maalumu Arusha na kumtaka aongozane na watu wanne waliokuwa wakimsubiri uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro KIA.

Sabaya alidai kuwa walipofika Arusha wakiwa na wale watu wanne ambao ndio wenye taarifa zote walielekea eneo husika waliokuwa wameelekezwa na Mamlaka husika katika eneo la duka la Shaahid store lililopo mtaa wa Soko kuu jijini Arusha.

Akihojiwa na Wakili Mahuna kuhusu kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya tarehe 9.2.2021 ,Sabaya alidai alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani kilimanjaro na aliteuliwa na Rais Hayati Dkt John Pombe Magufuli tarehe 29.7.2018.

Lengai Ole Sabaya anaeleza mahakama kuwa alitumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 2 na miezi 10 na alikoma kuhudumu wadhifa huo tarehe 13.5.2021 baada ya Rais Samia Suluhu kutengua nafasi yake kupisha uchuguzi .

Sabaya ameieleza Mahakama kwamba baada ya kufikia katika duka hilo walimkosa Mmiliki wa duka na ndipo alipowasiliana na mamlaka iliyomtuma kazi hiyo, ambayo ilimjibu kwamba imeshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongozi na imeelekeza watu waliokutwa eneo la tukio wapelekwe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi ili kusaidia kupatikana Kwa mhusika wa duka aliyekuwa akitafutwa.

Anaeleza kuwa suala la yeye kupatiwa maelekezo na Mamlaka ya uteuzi ni Jambo la kawaida kwani miezi mitatu kabla ya siku ya tukio 9.2.2021 alipewa maelekezo ya kufanyakazi maalum na kubaini mtambo wa kutengeneza fedha bandia na kukamata fedha bandia sh,milioni 800 jijini Dar es salaam.

Sabaya anaeleza kuwa katika zoezi hilo alikuwa msimamizi mkuu ambapo Hata Gavana wa Fedha Prof Florian Luoga pamoja na aliye kuwa waziri wa Fedha hapa Nchini Dkt Philp Mpango ambaye kwasasa ndiye Makamu wa Rais wanalijua.

Sabaya amedai kuwa hajawahi kufikia katika duka la Shaahid Store na kupora kiasi cha sh, milioni 2,769,000 na kisha kumpiga human Jasim , Bakari Msangi, Salim hasani na Ally shabani na kuwatisha Kwa silaha na kwamba hamfahamu mshtakiwa mwenzake anayetajwa Kwa jina la Daniel Mbura na pia Silvester Nyegu hakuwa naye siku ya tukio.

Sabaya anaendelea kujitetea....

Kwani Yeye ni robot, si alifanya akiwa na akili timamu, au alikua kichaa ,sabaya ACHA utetezi wa Kishamba, ilikua wazi kuamua au kuachia kazi ,uzuri ulishafutwa, na wengine watafuta kufutwa
 
Katika uliokuwa utawala wa Magufuli, hili la kumwagiza DC wa Hai - Kilimanjaro kwenda kufanya special operation nje ya eneo lake la utawala kwa maana ya wilaya na mkoa mwingine bila kiongozi wa eneo hilo la kiutawala kwa maana ya DC au RC kujua, inawezekana lilifanyika maana Tanzania ya wakati huo na ya sasa ni kama Banana Republic....

Mimi nadhani kwa kutoa utetezi huo, basi awe na ushahidi wa vielelezo vya kutosha kuufanya ukubalike. Na pia aweje kujibu cross examination questions kwa ufasaha toka kwa mawakili wa upande wa mashtaka...

Hata hivyo, kwa kutumia common sense tu, mtu anaweza kugundua kuwa huyu bwana kuna uwezekano mkubwa anadanganya tu kwa kumtumia marehemu kama ngao yake. Na ni wazi kuwa aliupata u - DC kimakosa...!!
 
Duh!! Mungu anamuona lakini!

Amejitetea kiume sana

Makamu wa Rais Dr Mpango na DC mstaafu Dr Kihongosi watakuwa mashahidi wake muhimu kama katiba inaruhusu.

Rais mstaafu Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kumtetea Prof Mahalu pale Kisutu!
Kihongosi naye ni dr.?
Au ili mradi awe mwanaccm?!!
 
Nani atathibitisha kama alitumwa na Magufuli , halafu ukitumwa kufanya ujambazi ndio hufungwi jela ?

Huyu kijana tulimuonya mara nyingi mno ! lakini akatupuuza akidhani kwamba jiwe litaishi milele , Kiko wapi sasa ?
Huu muda utumie vizuri kumtetea mwenyekiti wenu bado yupo nyuma ya nondo kwa kesi ya ugaidi
 
Back
Top Bottom