Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad.

Akiongozwa na wakili Mosses Mahuna wakati akitoa utetezi wake mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Sabaya alidai yeye bado ni mtumishi wa Serikali ila alisikia tangazo la kusimamishwa kazi kutoka Kwa Rais Samia Suluhu.

Alidai kuwa siku ya tukio Februari 9 mwaka huu majira ya saa 9 kasoro alasiri alipigiwa simu na Mamlaka iliyomteua na kumpatia maelekezo ya kwenda kufanya kazi maalumu Arusha na kumtaka aongozane na watu wanne waliokuwa wakimsubiri uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro KIA.

Sabaya alidai kuwa walipofika Arusha wakiwa na wale watu wanne ambao ndio wenye taarifa zote walielekea eneo husika waliokuwa wameelekezwa na Mamlaka husika katika eneo la duka la Shaahid store lililopo mtaa wa Soko kuu jijini Arusha.

Akihojiwa na Wakili Mahuna kuhusu kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya tarehe 9.2.2021 ,Sabaya alidai alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani kilimanjaro na aliteuliwa na Rais Hayati Dkt John Pombe Magufuli tarehe 29.7.2018.

Lengai Ole Sabaya anaeleza mahakama kuwa alitumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 2 na miezi 10 na alikoma kuhudumu wadhifa huo tarehe 13.5.2021 baada ya Rais Samia Suluhu kutengua nafasi yake kupisha uchuguzi .

Sabaya ameieleza Mahakama kwamba baada ya kufikia katika duka hilo walimkosa Mmiliki wa duka na ndipo alipowasiliana na mamlaka iliyomtuma kazi hiyo, ambayo ilimjibu kwamba imeshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongozi na imeelekeza watu waliokutwa eneo la tukio wapelekwe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi ili kusaidia kupatikana Kwa mhusika wa duka aliyekuwa akitafutwa.

Anaeleza kuwa suala la yeye kupatiwa maelekezo na Mamlaka ya uteuzi ni Jambo la kawaida kwani miezi mitatu kabla ya siku ya tukio 9.2.2021 alipewa maelekezo ya kufanyakazi maalum na kubaini mtambo wa kutengeneza fedha bandia na kukamata fedha bandia sh,milioni 800 jijini Dar es salaam.

Sabaya anaeleza kuwa katika zoezi hilo alikuwa msimamizi mkuu ambapo Hata Gavana wa Fedha Prof Florian Luoga pamoja na aliye kuwa waziri wa Fedha hapa Nchini Dkt Philp Mpango ambaye kwasasa ndiye Makamu wa Rais wanalijua.

Sabaya amedai kuwa hajawahi kufikia katika duka la Shaahid Store na kupora kiasi cha sh, milioni 2,769,000 na kisha kumpiga human Jasim , Bakari Msangi, Salim hasani na Ally shabani na kuwatisha Kwa silaha na kwamba hamfahamu mshtakiwa mwenzake anayetajwa Kwa jina la Daniel Mbura na pia Silvester Nyegu hakuwa naye siku ya tukio.

Sabaya anaendelea kujitetea....

View attachment 1890858
Ingekua China huko kaburi la mwendazake lingefukuliwa leo leo
 
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya leo Ijumaa Agosti 13, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha amewataja Hayati John Magufuli, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na Gavana wa Benki Kuu kuwa walikuwa wanajua operesheni aliyokuwa akiifanya Arusha.

Chanzo: mwananchi_official
Ukitumwa ndiyo uwatishe watu kwa bunduki ilhali we siyo askari ?!.

Mungu ni fundi amewanusuru WaTz na utawala wa mkono wa chuma.

Odhis *
 
Wakili anae endesha kesi ya sabaya ana uwezo mdogo sanaa kisheria, yaan mpaka hapo kamtia hatiani mteja wake. Rasmi sabaya hachomoki sababu wakili uwezo mdogo. Hoja ilitakiwa Sabaya kuwapiga wale au kuiba vitu pale na uwezekano wa kutokuwepo kwenye eneo husika.
 
hii kesi haina tofauti na ya Prof. Mahalu naye wakati alipo shitakiwa alidai alitumwa na aliye kuwa Rais wa awamu ya 3 Mkapa, kweli Mkapa walikuja na kumtetea Mahalau na Mahalu aliachiwa huru.
Sabaya hana makosa kama alikuwa anatekeleza maelekezo ya aliye mteua, naamini kama Magufuli angekuwa hai angemtetea Sabaya bila kigugumizi, lkn pia kama Mama Anna Mgwira ange kuwa hai ange mtetea Sabaya bila kigugumizi.

..Magufuli angekuwepo Sabaya asingeshtakiwa.

..Sidhani kama Mama Mghwira angekuwepo angemtetea Sabaya.

..Na hata angemtetea ushahidi wake ungekuwa hauna nguvu.

..Wanaotakiwa kumtetea Sabaya, na utetezi wao ukawa na nguvu, ni viongozi wa serikali na polisi wa mkoa wa Arusha.

..Tatizo lipo hapa: mtu anaweza kuwa ametumwa na mamlaka halali, ila ktk utekelezaji akavunja sheria. Kwa mfano, utetezi wa Sabaya kupiga watu ni nini?

..Pia wakati Sabaya anahojiwa hakusema kwamba alikuwa ametumwa na Raisi Magufuli? Kwanini polisi na DPP wamepuuza utetezi huo na kuamua kumshtaki Sabaya?

NB:

..Mramba na Yona walikuwa na ushahidi wa nyaraka za serikali kuonyesha kwamba maamuzi yao yalikuwa na baraka za Raisi. Pamoja na utetezi huo mahakama iliwakuta na hatia.
 
kijana sabaya anatuponza vijana tusipewe mamlaka kwa nchi yetu pendwa malawi ya kaskazini. 😆😆
 
Ukitumwa ndiyo uwatishe watu kwa bunduki ilhali we siyo askari ?!.

Mungu ni fundi amewanusuru WaTz na utawala wa mkono wa chuma.

Odhis *
Kwamba saa hii mnajula bata[emoji1][emoji1]

Kamanda umesahau masiha wenu yuko nyavu!!!!
 
Sabaya ameona ngoja atumie mlango wa dharura ( Emergency exit) kujinasua. Jamaa anaakili sana. Kunakoendelea hana kesi . Hapo suluhisho ni Katiba mpya amasivyo hata mpango hatoweza kuitwa kutoa utetezi wake mahakamini kisa katiba na sheria zilizopo haziruhusu Raisi wala makamu wala spika wala Jaji mkuu kushitakiwa
Sabaya amethibitisha bila chenga kuwa Magufuli alikuwa jambazi aliyekubuhu!
 
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya leo Ijumaa Agosti 13, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha amewataja Hayati John Magufuli, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na Gavana wa Benki Kuu kuwa walikuwa wanajua operesheni aliyokuwa akiifanya Arusha.

Chanzo: mwananchi_official
Basi mpango nae afanyiwe mpango

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sabaya anataka kuchoma nyumba

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
Tungekuwa tupo nchi zilizo very serious kwa Kutajwa tu huku tena kwa Kesi kama zinazomkabili Ole Sabaya hivi sasa Makamu wa Rais na Gavana walitakiwa wawe wameshajiuzuru.

Ole Sabaya tulimtuhumu, tulimcheka, tulimdharau na hadi kumuombea apatwe na mabaya ila sasa naona anaenda kuwa Shujaa na katika Basketball anaitwa MVP.

Kuna Hatari naiona au Habari mbaya inakuja tena Siku si nyingi katika Masikio yetu. Ole Sabaya ametimiza Ahadi yake alipokuwa Mahakamani kuwa atakuja Kupasua Ukweli wote na asitishwe na Mtu.
 
Kwamba saa hii mnajula bata[emoji1][emoji1]

Kamanda umesahau masiha wenu yuko nyavu!!!!
Kwani kuwa nyavu ni kifo?
Au kuwa nyavu ndio hakuna kutoka?
Mnafurahia udhalimu, ipo siku yenu ya kufi..rwa subirini
 
Kwani kuwa nyavu ni kifo?
Au kuwa nyavu ndio hakuna kutoka?
Mnafurahia udhalimu, ipo siku yenu ya kufi..rwa subirini
Kufi.rwa kuna wapa watu faida,si unaona mpaka umenunua simu??
 
Sabaya amethibitisha bila chenga kuwa Magufuli alikuwa jambazi aliyekubuhu!
Du hii hatari ndomaana alikuwa anajiamini kupita kiasi? Kumbe alikuwa mkuu wa operation maalumu alikuwa na majukumu zaidi ya ukuu wa wilaya tuliodhani ndo kazi yake.
 
Duh.....Mungu anamuona lakini!

Amejitetea kiume sana

Makamu wa Rais Dr Mpango na DC mstaafu Dr Kihongosi watakuwa mashahidi wake muhimu kama katiba inaruhusu.

Rais mstaafu Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kumtetea Prof Mahalu pale Kisutu!
Itabidi sauti ya jiwe ipelekwe mahakamani pia
 
Back
Top Bottom