Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Ole Sabaaya ameshapotoshwa na wanasheria wake,

1) Amri Kutoka Kwa Wakuu Wake (Order From Higher Personnel) sio utetezi wa jinai (Sio Criminal Defence). Ni Heri hata angejitetea alikua amelewa kupita kiasi kwasababu Ulevi (Intoxication) inaweza kutumika kama Criminal Defence.

2) Ushahidi wa kumtaja mtu kwamba amekupa maagizo fulani kisheria unahitaji "CORROBORATION" ya ushahidi wa ziada kutoka kwa huyo mtu alietajwa. Magufuli hawezi kupatikana kwaajili ya kutoa ushahidi wa ziada ku-support na ku-confirm ushahidi wa Ole Sabaaya.
Exactly.....

Serikali inafanya kazi kwa nyaraka...
Ukipigiwa simu kwenda kufanya ushenzi, ujue mambo yakiharibika you are on your own, serikali haihusiki hapo.

Pia kwenda kumtaja Luoga na Mpango ni kujimaliza kabisa, yaani anategemea Gavana na Vice President waseme tulikuwa tunajua "ujambazi" wa Sabaya.

Very stupid defense
 
JELA MWAKA MMOJA KWA KOSA LA KUFANYA KAZI NJE YA KITUO CHA KAZI BAADA YA HAPO ANAKUWA HURU MWAKA MMOJA NI SAWA NA MIEZI SITA TU
Hahahaa, naona mshaanza kubadili gia angani! Huyu lazima ale mvua
 
Mkuu wa wilaya ya Ya Hai anatumwa na Raisi akafanye operation wilaya isio yake ya Arusha? Raisi Hana operative wakuu wa wilaya ya Arusha au mkuu wa mkoa wa Arusha hidden operative wa kufanya hiyo Operation?...
Msimfanye mataga mwenzenu mbuzi wa kafara, enzi za utawala wa jiwe neno lake lilikuwa sheria na sheria ilikuwa neno lake.
 
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya leo Ijumaa Agosti 13, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha amewataja Hayati John Magufuli, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na Gavana wa Benki Kuu kuwa walikuwa wanajua operesheni aliyokuwa akiifanya Arusha.

Sabaya amesema hayo wakati akitoa utetezi mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi Odira Amworo kuwa alichokuwa anakifanya Arusha Februari 9, 2021 haikuwa operesheni yake ya kwanza kuagizwa na hayati Rais Magufuli.

Akiongozwa na wakili anayemtetea Mosses Mahuna, wakati alipoanza kujitetea mahakamani hapo amesema kesi hiyo ni ya kutengeneza na yeye hajaiba wala kumtishia mtu yoyote kwa silaha.

Sabaya alisema siku ya tukio Februari 9, 2021 alipomaliza kuongoza kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Hai, alipokea simu ya Dk Magufuli aliyemwelekeza kazi ya kufanya katika mkoa wa Arusha ambapo pia alipaswa kuwapitia watu wengine wanne katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo watu hao walikuwa na maelekezo juu ya kazi hiyo wanayoenda kufanya.

"Hiyo haikuwa kazi ya kwanza kwa sababu miezi michache iliyopita tulipewa zoezi la kukamata mitambo inayotengeneza noti bandia na tulifanikiwa kukamata mitambo na fedha Sh 800 Milioni bandia eneo la Chanika wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam ,Gavana wa BoT anajua na aliyekuwa Waziri wa Fedha kwa wakati huo Dk Philip Mpango, Makamu wa Rais wa sasa pia anafahamu," alisema Sabaya.

Chanzo: Mwananchi
 
Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad...

"Like son like father."

IMG_20210513_200524_882.jpg


Yote yalikuwa majambawazi tu!
 
Kwamba saa hii mnajula bata[emoji1][emoji1]

Kamanda umesahau masiha wenu yuko nyavu!!!!
Hata kama . Yule dhalimu ameleta mambo ya Kishamba sana. Tz tulishavuka hayo mambo . Ghafla tumekuwa wa kunyoshewa mikono !!

Odhis *
 
Je, wana CHADEMA Wenzangu hapa Mitandaoni JamiiForums kwa jinsi huyu aliyekuwa Adui yetu Ole Sabaya sasa anavyoupiga mwingi Kiutetezi kwa Kuwataja Hayati Rais Dkt. Magufuli, Makamu wa Rais Dkt. Mpango na Gavana wa BOT tutabadilika na kuanza Kumpenda na Kumpamba Mitandaoni au tutaendelea tu Kumkazia na watajuana wenyewe kwa wenyewe?
 
Exactly.....

Serikali inafanya kazi kwa nyaraka...
Ukipigiwa simu kwenda kufanya ushenzi, ujue mambo yakiharibika you are on your own, serikali haihusiki hapo.

Pia kwenda kumtaja Luoga na Mpango ni kujimaliza kabisa, yaani anategemea Gavana na Vice President waseme tulikuwa tunajua "ujambazi" wa Sabaya.

Very stupid defense
Bwashee tofautisha Kazi maalumu na Ujambazi!

Usipanic.......hii kesi tangu mwanzo ilionyesha Sabaya anachomoka!
 
Hata kama . Yule dhalimu ameleta mambo ya Kishamba sana. Tz tulishavuka hayo mambo . Ghafla tumekuwa wa kunyoshewa mikono !!

Odhis *
Ushamba hufanya kazi kwa washamba.

Alijua mma ushamba fulani,akawaletea mwingine ili akili ziwakae sawa.
 
Back
Top Bottom