Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Unadhani kwanini amewataja kama anajua watamruka?
Utamzuiaje jambazi, kwani wanajua angeenda kuvamia duka saa ngapi? Kama alitumwa kwanini hakwenda na polisi hata moja? Mambo ya kuhusika na dolar black market hayana mamlaka husika hadi Mkuu wa Wilaya tena Wilaya ya Mkoa mwingine aingilie kati? Jambazi hajawahi kusafishika bwashe!
 
Yeye ndiyo akili zimemkaa sawa huko alikitangulia . Huwezi kujiona wewe ndiyo wewe dunia hii ya Mungu. Yako wapi sasa kawaachia watu wanatumbua .

Huwezi kupora mchakato wote as if umeongea na Mungu. Kwisha habari yake
Kifo ni haki ya kila mtu, hata ambao wameporwa ulaji 2020 kwa huzuni.

Kama ni Mungu alimuondoa JPM kwa ajili yenu, kisha akamleta Samia, basi huyu ni mungu wa mizuka.
 
soma hii rafiki

Kama prove ipo Mzee usifikili angefanya yale Bila ruhusa ya wakubwa wake
Burden of Proof...c&p

On which party has the burden to prove allegations in a complaint before the Office of the Ombudsman, the Court has ruled:​
The basic rule is that mere allegation is not evidence and is not equivalent to proof. Charges based on mere suspicion and speculation likewise cannot be given credence. When the complainant relies on mere conjectures and suppositions, and fails to substantiate his allegations, the complaint must be dismissed for lack of merit
 
Kwa maana nyingine amekiri kuhusika na hivyo asubiri kungininizwa tu. Hakuna mahakamanya kipumbavu ya kusikia mere stories za kuwasingizia rais au wengineo bila written proofs.

Angekuwa na akiri angejiuzuru baada ya kutumwa kinyume na scope yake
 
Sabaya anaeleza kuwa katika zoezi hilo alikuwa msimamizi mkuu ambapo Hata Gavana wa Fedha Prof Florian Luoga pamoja na aliye kuwa waziri wa Fedha hapa Nchini Dkt Philp Mpango ambaye kwasasa ndiye Makamu wa Rais wanalijua.
Wanaelewa kuwa alikwenda na mabunduki na majambazi yasiyo polisi kufanya "uhalifu"? Walimuingiza mkenge.... is no defence
 
Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad.

Akiongozwa na wakili Mosses Mahuna wakati akitoa utetezi wake mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Sabaya alidai yeye bado ni mtumishi wa Serikali ila alisikia tangazo la kusimamishwa kazi kutoka Kwa Rais Samia Suluhu.

Alidai kuwa siku ya tukio Februari 9 mwaka huu majira ya saa 9 kasoro alasiri alipigiwa simu na Mamlaka iliyomteua na kumpatia maelekezo ya kwenda kufanya kazi maalumu Arusha na kumtaka aongozane na watu wanne waliokuwa wakimsubiri uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro KIA.

Sabaya alidai kuwa walipofika Arusha wakiwa na wale watu wanne ambao ndio wenye taarifa zote walielekea eneo husika waliokuwa wameelekezwa na Mamlaka husika katika eneo la duka la Shaahid store lililopo mtaa wa Soko kuu jijini Arusha.

Akihojiwa na Wakili Mahuna kuhusu kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya tarehe 9.2.2021 ,Sabaya alidai alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani kilimanjaro na aliteuliwa na Rais Hayati Dkt John Pombe Magufuli tarehe 29.7.2018.

Lengai Ole Sabaya anaeleza mahakama kuwa alitumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 2 na miezi 10 na alikoma kuhudumu wadhifa huo tarehe 13.5.2021 baada ya Rais Samia Suluhu kutengua nafasi yake kupisha uchuguzi .

Sabaya ameieleza Mahakama kwamba baada ya kufikia katika duka hilo walimkosa Mmiliki wa duka na ndipo alipowasiliana na mamlaka iliyomtuma kazi hiyo, ambayo ilimjibu kwamba imeshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongozi na imeelekeza watu waliokutwa eneo la tukio wapelekwe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi ili kusaidia kupatikana Kwa mhusika wa duka aliyekuwa akitafutwa.

Anaeleza kuwa suala la yeye kupatiwa maelekezo na Mamlaka ya uteuzi ni Jambo la kawaida kwani miezi mitatu kabla ya siku ya tukio 9.2.2021 alipewa maelekezo ya kufanyakazi maalum na kubaini mtambo wa kutengeneza fedha bandia na kukamata fedha bandia sh,milioni 800 jijini Dar es salaam.

Sabaya anaeleza kuwa katika zoezi hilo alikuwa msimamizi mkuu ambapo Hata Gavana wa Fedha Prof Florian Luoga pamoja na aliye kuwa waziri wa Fedha hapa Nchini Dkt Philp Mpango ambaye kwasasa ndiye Makamu wa Rais wanalijua.

Sabaya amedai kuwa hajawahi kufikia katika duka la Shaahid Store na kupora kiasi cha sh, milioni 2,769,000 na kisha kumpiga human Jasim , Bakari Msangi, Salim hasani na Ally shabani na kuwatisha Kwa silaha na kwamba hamfahamu mshtakiwa mwenzake anayetajwa Kwa jina la Daniel Mbura na pia Silvester Nyegu hakuwa naye siku ya tukio.

Sabaya anaendelea kujitetea....

*Lengai Ole Sabaya-'LOS' must be the best, intelligent and bright government servant who confidently complied instructions from the appointing authority with consistency. He always was successful in all assignments. At this stage and witness defense statements assessment, the then Arusha DC, governor of the central bank, and the then finance and planning minister must be summoned in the court of law to complement the substance of facts.
 
mere stories za kuwasingizia rais au wengineo bila written proofs.
Umeongea vema in line with the law

Burden of Proof

On which party has the burden to prove allegations in a complaint before the Office of the Ombudsman, the Court has ruled:

The basic rule is that mere allegation is not evidence and is not equivalent to proof. Charges based on mere suspicion and speculation likewise cannot be given credence. When the complainant relies on mere conjectures and suppositions, and fails to substantiate his allegations, the complaint must be dismissed for lack of merit​
 
Anasafishwa tu hapo...

Mama anatimiza tu kilichoachwa na ..kiumbe...

Kesi ishazimuliwa na kuwa nyepesi....
Wepesi kisa kamtaja marehemu?
Hivi mpango na gavana walikosa njia ya kumfikia huyo mwenye duka wakaona mtu pekee ni Sabaya?

Ingalikua hivyo Mpango kwa wadhifa wake wa sasa asingalishindwa kuzuia hii kashfa dhidi yake
 
Mkuu wa wilaya ya Ya Hai anatumwa na Raisi akafanye operation wilaya isio yake ya Arusha? Raisi Hana operative wakuu wa wilaya ya Arusha au mkuu wa mkoa wa Arusha hidden operative wa kufanya hiyo Operation?

Sabaya zigo lako Hilo uliwezaje kwenda kufanya military operation nje ya your judistriction? Hiyo Operation alitakiwa afanye Mama Mgwira au mkuu wa wilaya ya Arusha au polisi wilaya ya Arusha au mkoa etc etc but from Arusha.Raisi hawezi ishiwa operatives wa any mission Hana haja ya kutafuta mtu wa Hai kwenda Arusha!!!

Sabaya jambazi wewe kesi Hilo lako usisingizie Marehemu wewe hukujua kuwa Arusha sio eneo lako la judistriction? Kuwa wewe ni
mkuu wa wilaya ya hai? Ungekuwa huna area ya uteuzi utetezi wako unge matter. Lakini mmmmmm .una kesi ya kujibu
Ni JURISDICTION wewe mwehu. Waambie Lumumba wawapeleke hata kwa ras simba.
 
I
hahah huyu jambazi anajidanganya kuwa akimtaja marehemu Pombe ndiyo atapata unafuu.
H
Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad.

Akiongozwa na wakili Mosses Mahuna wakati akitoa utetezi wake mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Sabaya alidai yeye bado ni mtumishi wa Serikali ila alisikia tangazo la kusimamishwa kazi kutoka Kwa Rais Samia Suluhu.

Alidai kuwa siku ya tukio Februari 9 mwaka huu majira ya saa 9 kasoro alasiri alipigiwa simu na Mamlaka iliyomteua na kumpatia maelekezo ya kwenda kufanya kazi maalumu Arusha na kumtaka aongozane na watu wanne waliokuwa wakimsubiri uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro KIA.

Sabaya alidai kuwa walipofika Arusha wakiwa na wale watu wanne ambao ndio wenye taarifa zote walielekea eneo husika waliokuwa wameelekezwa na Mamlaka husika katika eneo la duka la Shaahid store lililopo mtaa wa Soko kuu jijini Arusha.

Akihojiwa na Wakili Mahuna kuhusu kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya tarehe 9.2.2021 ,Sabaya alidai alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani kilimanjaro na aliteuliwa na Rais Hayati Dkt John Pombe Magufuli tarehe 29.7.2018.

Lengai Ole Sabaya anaeleza mahakama kuwa alitumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 2 na miezi 10 na alikoma kuhudumu wadhifa huo tarehe 13.5.2021 baada ya Rais Samia Suluhu kutengua nafasi yake kupisha uchuguzi .

Sabaya ameieleza Mahakama kwamba baada ya kufikia katika duka hilo walimkosa Mmiliki wa duka na ndipo alipowasiliana na mamlaka iliyomtuma kazi hiyo, ambayo ilimjibu kwamba imeshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongozi na imeelekeza watu waliokutwa eneo la tukio wapelekwe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi ili kusaidia kupatikana Kwa mhusika wa duka aliyekuwa akitafutwa.

Anaeleza kuwa suala la yeye kupatiwa maelekezo na Mamlaka ya uteuzi ni Jambo la kawaida kwani miezi mitatu kabla ya siku ya tukio 9.2.2021 alipewa maelekezo ya kufanyakazi maalum na kubaini mtambo wa kutengeneza fedha bandia na kukamata fedha bandia sh,milioni 800 jijini Dar es salaam.

Sabaya anaeleza kuwa katika zoezi hilo alikuwa msimamizi mkuu ambapo Hata Gavana wa Fedha Prof Florian Luoga pamoja na aliye kuwa waziri wa Fedha hapa Nchini Dkt Philp Mpango ambaye kwasasa ndiye Makamu wa Rais wanalijua.

Sabaya amedai kuwa hajawahi kufikia katika duka la Shaahid Store na kupora kiasi cha sh, milioni 2,769,000 na kisha kumpiga human Jasim , Bakari Msangi, Salim hasani na Ally shabani na kuwatisha Kwa silaha na kwamba hamfahamu mshtakiwa mwenzake anayetajwa Kwa jina la Daniel Mbura na pia Silvester Nyegu hakuwa naye siku ya tukio.

Sabaya anaendelea kujitetea....

Hahaha zakuambiwa changanya nazako sabay unafanya kosa unasingizia fulani alikutuma hakuna sheria ya hivyo hapa dunian pambana na hali yako
 
Duh!! Mungu anamuona lakini!

Amejitetea kiume sana

Makamu wa Rais Dr Mpango na DC mstaafu Dr Kihongosi watakuwa mashahidi wake muhimu kama katiba inaruhusu.

Rais mstaafu Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kumtetea Prof Mahalu pale Kisutu!
Magufuli was a big problem in this country!
 
*Lengai Ole Sabaya-'LOS' must be the best, intelligent and bright government servant who confidently complied instructions from the appointing authority with consistency. He always was successful in all assignments. At this stage and witness defense statements assessment, the then Arusha DC, governor of the central bank, and the then finance and planning minister must be summoned in the court of law to complement the substance of facts.
Nani atakubali kuja?
 
hii kesi haina tofauti na ya Prof. Mahalu naye wakati alipo shitakiwa alidai alitumwa na aliye kuwa Rais wa awamu ya 3 Mkapa, kweli Mkapa walikuja na kumtetea Mahalau na Mahalu aliachiwa huru.
Sabaya hana makosa kama alikuwa anatekeleza maelekezo ya aliye mteua, naamini kama Magufuli angekuwa hai angemtetea Sabaya bila kigugumizi, lkn pia kama Mama Anna Mgwira ange kuwa hai ange mtetea Sabaya bila kigugumizi.
sijaona unyang'anyi uliotendwa!
mnyang'anyi angechukua receipts machine ya nn?!!
mnyang'anyi angepiga simu kituo cha polisi?!
huo ni unyang'anyi wa wapi?!
Wewe kweli akili yako umeshikiwa. Yani sabaya hana kosa? Na hapo ni kesi ya Shahid Stores tu bado hizo kesi za ubakaji, bado kesi za huko Kilimanjaro. .

Huyo mtu ana kesi nyingi na uovu mwingi sana mpaka shetani mwenyewe analaani.
 
Du hii hatari ndomaana alikuwa anajiamini kupita kiasi? Kumbe alikuwa mkuu wa operation maalumu alikuwa na majukumu zaidi ya ukuu wa wilaya tuliodhani ndo kazi yake.
Sasa hivi tuko katika hatari kubwa kwa sababu serikali haiwezi kutulinda tena kwani uharamia unafanywa na yenyewe!
 
Wewe kweli akili yako umeshikiwa. Yani sabaya hana kosa? Na hapo ni kesi ya Shahid Stores tu bado hizo kesi za ubakaji, bado kesi za huko Kilimanjaro. .

Huyo mtu ana kesi nyingi na uovu mwingi sana mpaka shetani mwenyewe analaani.
Duh!
ana lingana na Gaidi namba 1?!
 
Back
Top Bottom