Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Wepesi kisa kamtaja marehemu?
Hivi mpango na gavana walikosa njia ya kumfikia huyo mwenye duka wakaona mtu pekee ni Sabaya?

Ingalikua hivyo Mpango kwa wadhifa wake wa sasa asingalishindwa kuzuia hii kashfa dhidi yake
Haya mambo yako wazi Ipo video Gavana Akimsifia Kijana kwa kazi nzuri ya pesa bandia Tafuta utaipata
 
Huyu ndio mtu alitaka kazi ya undercover? Undercover gani ana blow mission???[emoji23][emoji23][emoji23]
 
*Lengai Ole Sabaya-'LOS' must be the best, intelligent and bright government servant who confidently complied instructions from the appointing authority with consistency. He always was successful in all assignments. At this stage and witness defense statements assessment, the then Arusha DC, governor of the central bank, and the then finance and planning minister must be summoned in the court of law to complement the substance of facts.

c&p​

What to do when your boss asks you to do something unethical or illegal​

"It can feel like a lose-lose — but you should never comply with an illegal request."

"Most of all, know that your self-protection is paramount," Taylor explains. "Misdeeds, ....., illegal hiring and .... can plague you for a lifetime if you decide to engage — professionally, morally, and in extreme cases, legally."

Again, if you think (or know) the request is illegal, do not comply.
 
Hamna kesi hapo ni watu wanaenda mahakaman kusubiria siku ya mashtaka kufutwa
 
Serikali iliyopo madarakani inaundwa na wale wale wa enzi ya JPM, hao nao wana la kujibu, hasa Samia na Mpango waitwe mahakamani wakakanushe ama wakili tuhuma hizo
 
Majukumu ya polisi ni yapi!.na majukumu ya mkuu wa wilaya ni yapi!

Hapa kimeumana tunataka katiba mpya
JamiiForums2011088224.jpg
 
*Lengai Ole Sabaya-'LOS' must be the best, intelligent and bright government servant who confidently complied instructions from the appointing authority with consistency. He always was successful in all assignments. At this stage and witness defense statements assessment, the then Arusha DC, governor of the central bank, and the then finance and planning minister must be summoned in the court of law to complement the substance of facts.

c&p​

What to do when your boss asks you to do something unethical or illegal​

"It can feel like a lose-lose — but you should never comply with an illegal request."

"Most of all, know that your self-protection is paramount," Taylor explains. "Misdeeds, ....., illegal hiring and .... can plague you for a lifetime if you decide to engage — professionally, morally, and in extreme cases, legally."

Again, if you think (or know) the request is illegal, do not comply.
 
I
H
Hahaha zakuambiwa changanya nazako sabay unafanya kosa unasingizia fulani alikutuma hakuna sheria ya hivyo hapa dunian pambana na hali yako

What to do when your boss asks you to do something unethical or illegal​

"It can feel like a lose-lose — but you should never comply with an illegal request."

"Most of all, know that your self-protection is paramount," Taylor explains. "Misdeeds, ....., illegal hiring and .... can plague you for a lifetime if you decide to engage — professionally, morally, and in extreme cases, legally."

Again, if you think (or know) the request is illegal, do not comply.
 
Sabaya ameona ngoja atumie mlango wa dharura ( Emergency exit) kujinasua. Jamaa anaakili sana. Kunakoendelea hana kesi . Hapo suluhisho ni Katiba mpya amasivyo hata mpango hatoweza kuitwa kutoa utetezi wake mahakamini kisa katiba na sheria zilizopo haziruhusu Raisi wala makamu wala spika wala Jaji mkuu kushitakiwa
Kwa jicho la mtaani, utaona hivyo lakini kwa jicho la kisheria hakuna kichaka kama hicho!!yaani kiongozi wako akupe maelekezo ya kutenda jinai, utende eti badaye uje useme nilikuwa natekeleza maagizo?!!waulize polisi, wanajeshi huwa kinawakuta nini pale wanapokengeuka eti kwa kutii maaelekezo, ya wakuu wao!!!bora hata ingekuwa ni kwenye matumizi mabaya ya pesa ya umma, akawa na ushahidi wa mkubwa wake?!!
Kwa hiyo leo hii IGP, akimwambia askari wa chini piga risasi huyo, na kweli akampiga, huyo askari hatakuwa na kesi??
 
Kama haijatajwa hii kwenye post zilizopita naomba nitaje:
Kwa mtu wa serikali kucommit crime na baadaye kujitetea kwamba walikuwa wanafuata orders za wakubwa zake haukubaliki kisheria.
Refer to Nuremberg trials of NAZI war criminals (majenerali wa Hitler) after WW2.
Utetezi wao kwamba walifuata orders za Hitler ulikataliwa na wakanyongwa.
 
Kwa hi
hii kesi haina tofauti na ya Prof. Mahalu naye wakati alipo shitakiwa alidai alitumwa na aliye kuwa Rais wa awamu ya 3 Mkapa, kweli Mkapa walikuja na kumtetea Mahalau na Mahalu aliachiwa huru.
Sabaya hana makosa kama alikuwa anatekeleza maelekezo ya aliye mteua, naamini kama Magufuli angekuwa hai angemtetea Sabaya bila kigugumizi, lkn pia kama Mama Anna Mgwira ange kuwa hai ange mtetea Sabaya bila kigugumizi.
Mbona anamdhalilisha mwendazake, Luoga na Mpango aisee hii nchi tunahitaji katiba mpya tu
Ana ushahidi wa maandishi kuwa aliagizwa au mfa maji tu
 
Kwanini wasimfunge tu kwanza miaka 10 halafu kesi ndio ianze kusikilizwa
 
Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad.

Akiongozwa na wakili Mosses Mahuna wakati akitoa utetezi wake mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Sabaya alidai yeye bado ni mtumishi wa Serikali ila alisikia tangazo la kusimamishwa kazi kutoka Kwa Rais Samia Suluhu.

Alidai kuwa siku ya tukio Februari 9 mwaka huu majira ya saa 9 kasoro alasiri alipigiwa simu na Mamlaka iliyomteua na kumpatia maelekezo ya kwenda kufanya kazi maalumu Arusha na kumtaka aongozane na watu wanne waliokuwa wakimsubiri uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro KIA.

Sabaya alidai kuwa walipofika Arusha wakiwa na wale watu wanne ambao ndio wenye taarifa zote walielekea eneo husika waliokuwa wameelekezwa na Mamlaka husika katika eneo la duka la Shaahid store lililopo mtaa wa Soko kuu jijini Arusha.

Akihojiwa na Wakili Mahuna kuhusu kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya tarehe 9.2.2021 ,Sabaya alidai alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani kilimanjaro na aliteuliwa na Rais Hayati Dkt John Pombe Magufuli tarehe 29.7.2018.

Lengai Ole Sabaya anaeleza mahakama kuwa alitumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 2 na miezi 10 na alikoma kuhudumu wadhifa huo tarehe 13.5.2021 baada ya Rais Samia Suluhu kutengua nafasi yake kupisha uchuguzi .

Sabaya ameieleza Mahakama kwamba baada ya kufikia katika duka hilo walimkosa Mmiliki wa duka na ndipo alipowasiliana na mamlaka iliyomtuma kazi hiyo, ambayo ilimjibu kwamba imeshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongozi na imeelekeza watu waliokutwa eneo la tukio wapelekwe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi ili kusaidia kupatikana Kwa mhusika wa duka aliyekuwa akitafutwa.

Anaeleza kuwa suala la yeye kupatiwa maelekezo na Mamlaka ya uteuzi ni Jambo la kawaida kwani miezi mitatu kabla ya siku ya tukio 9.2.2021 alipewa maelekezo ya kufanyakazi maalum na kubaini mtambo wa kutengeneza fedha bandia na kukamata fedha bandia sh,milioni 800 jijini Dar es salaam.

Sabaya anaeleza kuwa katika zoezi hilo alikuwa msimamizi mkuu ambapo Hata Gavana wa Fedha Prof Florian Luoga pamoja na aliye kuwa waziri wa Fedha hapa Nchini Dkt Philp Mpango ambaye kwasasa ndiye Makamu wa Rais wanalijua.

Sabaya amedai kuwa hajawahi kufikia katika duka la Shaahid Store na kupora kiasi cha sh, milioni 2,769,000 na kisha kumpiga human Jasim , Bakari Msangi, Salim hasani na Ally shabani na kuwatisha Kwa silaha na kwamba hamfahamu mshtakiwa mwenzake anayetajwa Kwa jina la Daniel Mbura na pia Silvester Nyegu hakuwa naye siku ya tukio.

Sabaya anaendelea kujitetea....

Mpaka hapo Lengai amekiri kuwa alivamia dukani kwa watu nje ya eneo lake la utawala, kuhusu utetezi wake kuwa katumwa na mamlaka ya uteuzi ni wajibu hao waliotajwa kukanusha au kukiri ili nao wajifunue hadharani
 
Back
Top Bottom