Utetezi wa Simbachawene unaeleweka ukiwa ni mtu wa umri fulani

Awamu ya sita ina changamoto ya ongezeko la watu. Hesabu nyepesi tu, nyumba yenye watoto wawili na ile yenye watoto kumi ipi ina majukumu mazito zaidi?.
 
Tangu tupate uhuru haijawahi kutokea tukawa na mipango mizuri. Tunaona shida kulipa hizi tozo lakini ndio uhalisia wenyewe wa maisha.

..I disagree.

..Mipango yetu mingi ilikuwa mizuri.

..Tatizo ni Tanu na Ccm kutekeleza mipango yetu vibaya.

..Mara nyingi tumetumbukiza SIASA ktk mambo yanayohitaji utaalamu.

..Viongozi wetu wanaendekeza PROPAGANDA badala ya kufanya kazi na kutatua changamoto.
 
Awamu ya sita ina changamoto ya ongezeko la watu. Hesabu nyepesi tu, nyumba yenye watoto wawili na ile yenye watoto kumi ipi ina majukumu mazito zaidi?.

..Serikali ya awamu ya 6 ina uwezo mkubwa zaidi ya serikali ya awamu ya 1,2,na 3.

..Ccm na serikali wamekosa ubunifu tu, pia hawajitumi.

..Kudai kwamba tuna idadi kubwa ya watu ni kuficha uzembe tu wa serikali.
 
Zamani Landlover zilinunuliwa mpaka zinachakaa ndio zinakuja zingine. Siku hizi kila mwaka Waziri anabadilisha gari V8 MAX new edition. Wangeacha ubinafsi na ulafi nchi ilikuwa na uwezo wa kulea raia bila tatizo. Huyo LIONCHAMWENE ni bepari hatari. Aache uongo.
 
..Serikali ya awamu ya 6 ina uwezo mkubwa zaidi ya serikali ya awamu ya 1,2,na 3.

..Ccm na serikali wamekosa ubunifu tu, pia hawajitumi.

..Kudai kwamba tuna idadi kubwa ya watu ni kuficha uzembe tu wa serikali.
Ongezeko la watu linakwenda sambamba na uboreshaji wa hali zao za maisha. Kina Nyerere hawakukutana na mazingira kama haya ya sasa.
 
Ongezeko la watu linakwenda sambamba na uboreshaji wa hali zao za maisha. Kina Nyerere hawakukutana na mazingira kama haya ya sasa.

..hoja yangu ni kwamba Mwalimu Nyerere alikuwa na nyenzo duni za kuboresha maisha ya wananchi ukilinganisha na Samia Suluhu.

..Enzi za Mwalimu Nyerere kipindi cha masika mikoa ya kusini ilikuwa haifikiki kutokana na ubovu wa barabara ya kwenda kusini.

..Serikali ya awamu ya 6 ina mahusiano mazuri na nchi zote majirani zetu, wakati wa Mwalimu Nyerere tulikuwa na mahusiano mabaya na Uganda, Kenya, Malawi, Zaire, na Msumbiji chini ya Wareno.

..Mwalimu kuna wakati alikatiwa fedha za misaada na mikopo, wakati Samia anapata misaada na anaweza kukopa popote.

..Natofautiana na wewe kwamba awamu ya 6 watawala wana changamoto kuzidi wa aeamu ya 1 2 au 3.
 
Awamu ya sita ina changamoto ya ongezeko la watu. Hesabu nyepesi tu, nyumba yenye watoto wawili na ile yenye watoto kumi ipi ina majukumu mazito zaidi?.
Kama wewe ni mwananchi wa kawaida basi nakupa pole maana siku ukiujua ukweli utajutia utetezi wako huu kwa serikali. Na kama ni kiongozi basi endelea kulamba asali kimya kimya maana ipo siku itageuka shubiri.

Wingi wa watu ungekuwa chanzo cha umaskini kwa taifa, basi china wangeshika nafasi ya kwanza kwa umaskini!

Maskini Watanzania, sijui ni nani aliyewaroga? Mnalishwa matango pori na bado mnaamini ni ukweli!

Kilicholiathiri hili taifa ni ufisadi, ubadhilifu, rushwa na ubinafsi! Viongozi wengi wanamiliki mali nyingi zisizoendana na vipato vyao halisi!
Wauze mali walizonazo tujenge viwanda! Waache kutulundikia kodi na tozo kwa kipato hicho hicho.
Tozo na kodi zaidi ya mara moja kwa kipato hicho hicho, ni wizi!
 
Tatizo siyo ongezeko la watu, tatizo ni mfumo mbovu wa Ujamaa tunaoung'ang'ania. India ina watu bilioni 1.3 lakini uchumi wao unakua. Wanawezaje? Hawana sera mbovu za Ujamaa zinazoharibu uchumi na kufanya maisha yawe magumu sana.
 
Tupo watu milioni 60 na zaidi kidogo, kawaulize watawala wa Nigeria ugumu wa kuongoza taifa lenye watu karibu milioni 200 utapata majibu mazuri.
 
  • JE NCHI INA RASILIMALI? JE ZINATUMIKIA WANANCHI AU WANANCHI NDIO WANAZITUMIKIA?
  • Ni sawa na kusema changamoto zinatokana na ukubwa wa nchi.
 
Ni mantiki gani ya mshahara wangu uliokatwa paye ukaingizwa kwenye akaunti niliyoambiwa nifungue kwa ajili ya mshahara, akaunti ambayo nakatwa bank charges zote halafu mshahara huo huo uje ukatwe tozo! Mshahara huo huo nikimtumia mama yangu mpesa ukatwe tena tozo, mshahara huo huo nikimlipa mwenye nyumba kodi nikatwe wakala wa TRA 10%, ninalipwa sh ngapi kuwa wakala wa TRA! Mwigulu maarifa yamemuishia, inahitajika damu mpya.
 
Kwamba Nan alaumiwe???

Ni wazi waliozaa watoto wengi?

Au ilaumiwe Serikali iloshindwa kutumia wingi wa watu kupiga hatua kimaendeleo kama china???

Kama hawana majibu ya matatizo ya wananchi waachie Ngazi, ije Serikali ya chama lingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…