- Kwa kawaida huwa ninasikiliza maneno ya mwanzo tu basi katika hizi interviews za hawa wanasiasa wa bongo, lakini this one nimeisikiliza mpaka mwisho kwa sababu nilitaka kusikia anything new kuliko ninavyomfahamu waziri mwenyewe, na what she had to say kuhusu wagombea wengine wawili aliogombea nao, na the rest of the political story
- To my shock, waziri mzima wa jamhuri na mwenye elimu kubwa kama alivyodai kuwa nayo, ametumia muda karibu wote kumzungumzia mgombea mmoja tu, yaani Mama Janet, kwa nini sio the other candidate? Huyu mbona hatajwi na wala hakutajwa kabisa? WHY?
- Anaponda elimu ya mgombea mwingine kwa misingi ipi hiyo? Kwani katiba ya UWT haikutimilika kwa kiwango cha elimu ya wagombea wengine wawili? Na kama elimu kubwa ni kigezo cha uchaguzi wake kwa mawazo ya huyu waziri kwa nini hakuulizwa kuwa ni kwa nini Mwandosya na Salim wenye elimu kubwa sana, walishindwa urais na Kikwete mwenye elimu ndogo sana kulinganisha na hao wawili? Sasa kwa huu muono wake wa elimu ndogo kuwa ni sawa na kuongoza in the 60s na 70s, anapowaangalia Salim na Mwandosya, huku Kikwete akiwa ndiye rais aliyeshinda ina maana anaongoza like in the 60s na 70s?
- Sophia ameshinda uchaguzi tayari na sasa yeye ni mwenyekiti, then why worry na taarabu zote alizozitoa kwenye ile interview? I mean sijawahi kusikia mshindi wa uchaguzi akipoteza muda mrefu kuimba taarabu over mgombea aliyemshinda badala ya kutumia muda ule kuweka muongozo wa nini anategemea kukifanya, na kujaribu kuwa-win wananchi wasiomfahamu kiuongozi, lakini huyu ameongea taarabu weeee for what hasa? Hajiamini nini? Na kwa nini hajiamini hasa? Mbona interview za Obama baada ya hatujaona akiimba taarabu?
We can go on and on, kuhusu what was right na what was wrong na her ugly personal conduct kwa sababu ndio hasa sababu ya kuwepo kwetu hapa JF, na ninaomba kusema wazi kwamba hata mimi nimesikitishwa sana na the arrogance ya huyu waziri kwenye hii interview, sisi wananchi wa hili taifa sio wajinga kama hawa viongozi wanavyofikiri na ukweli ni kwamba huyu waziri aambiwe wazi kuwa anahitaji kufanya interview nyingine ili aombe radhi wananchi wote waliomsikiliza kwenye hii ya kwanza, kwa sababu imemshusha sana hadhi kuliko kumjenga na pia imetushusha hadhi wote tuliomsikiliza, kama this is all she could offer as far as kujitambulisha who she is kwa wananchi tusiomfahamu kabisa!
Sijui kilichopita huko nyuma na comments za wananchi hapa kuhusu ile interview, lakini Damn! majibu ya huyu waziri yalikuwa ni kinyume kabisa na elimu anayodai kua nayo, infact kwangu mimi inaleta maswali mazito sana kama kweli anayo hiyo elimu kwa sababu nimewahi kusikia sana kutoka kwa wanaofanya naye kazi kwa karibu kuwa huwa ana tabia za kutojiamini, as the results huwa anakuwa na ukali flani una-amount to arrogance hivi wa kujikinga asisogelewe karibu na maswali mazito, na baada ya kusikiliza hii interview ni clear kuwa critics wake wako right tena kwa 100%.
Amejaribu sana ku-raise ishus ambazo ukweli ni kwamba sio za wanawake wetu wa bongo, labda wa majuu huku akijaribu ku-promote ideas ambazo sijui ni wananchi wangapi wa Tanzania tumewahi kuzisikia zikifanyiwa kazi na UWT. What is UWT anyways? Wamewahi kufanya nini hasa kwa taifa au kwa maendeleo ya kina mama wetu? Mimi nijuavyo huu siku zote umekua umoja wa ku-hang out tu kwa kina mama wake wa viongozi na wanawake wanasiasa wa ngazi za juu tu, na sasa kuingia bungeni kwa mwenyekiti na katibu wake, pamoja na CC, lakini kwamba umewahi kumsaidia mwanamke wa kijijini? Labda zitolewe dataz tuzione kwanza.
Otherwise, tunamtakia kila na kheri Auntie Sophia, na ushindi huu ila tu cha msingi ni kwamba ni haki yetu wananchi kuuliza maswali, tena ya kila aina maana sisi wote hatuna akili moja na hatutoki kwenye njia moja ya maisha, ninaamini zipo interview zilizofanyika na viongozi wengi sana hapa ambazo Sophia anaweza akapewa kama muongozo on how to behave hapa JF, lakini never before nimewahi kusikia this kind of interview, where kiongozi ametumia muda karibu wote kuzungumzia mshindani wake badala ya UWT, tena kwa lugha chafu na dharau, kwa hili ustaarabu ni kwa huyu waziri kurudi hapa na atuombe radhi wananchi, na there is nothing personal about it ila ni kuelimishana tu! Apunguze jeuri na dharau hivi hamuoni bingwa wa dharau Mkapa alipo sasa? Hawa ndio mimi huwa ninasema wanaishia kumharibia Kikwete, maana unaishia kujiuliza anakuwaje na ukaribu na viongozi wenye this kind of Sophia's behavior?
Anajigamba amesoma, sasa kina Mwandosya watasema nini?
Sauti ya umeme, wazee wa FMES!