Mimi kwa kweli I don't subscribe na illusion kwamba leo wabunge wa CCM wamepata nuru ya kupigania utatuzi wa upungufu wa umeme. I really don't buy that.
Nilishangaa juzi Mh Sitta aliposema suala la RicmMond ni lazima wahusika wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria. Ni Sitta huyu ambaye alitumia rungu la CCM kuzima hoja ya Richmond na kuifunga akisema itajadiliwa na kamati husika hadi leo ni kimya. Ni wabunge wa CCM waliokaa kimya kuhusu Dowans n.k. Hata pale wapinzani walipotaka kumsulubu Ngeleja mapema kabisa CCM walitumia wingi wao na nguvu ya Spika kuzima hoja. Kama sitakosea kuna hoja ya mbunge wa upinzani kuhusu umeme ilizimwa na Spika wa CCM. Dhati ya kushughulikia umeme ipo wapi.
Bajeti ya Ngeleja ilipita katika kamati licha ya tuhuma za bahasha, kwa maneno mengine ilikubalika na kamati inayoongozwa na January Makamba.
Ni jambo la kushangaza January huyo huyo anapomhoji ngeleja wakati alishampa
go ahead. Dhati ipo wapi!
Bajeti hiyo ilipita baraza la mawaziri, sijui hawakuona mapungufu! dhati ya kushughulikia umeme ni ya kuhoji.
Kwa mtazamo wangu kilichotokea ni zao la makundi ndani ya chama ambayo yamezaa kitu kingine.
Pesa za Jairo hazikufikia walengwa wote bali kuzima midomo ya vinara.
Ukizingatia Ngeleja ni kijana wa mzee RA kundi hasimu halikunufaika na mgao. Ndipo wakaamua kumwaga maharage. Ndani ya bunge wapo wasiofaidika na mgao na wanaoamini uwepo wao bungeni ni kutokana na kuwa ndani ya CCM. Hawa wakabaini kuwa kama ilivyo Richmond ndivyo
Jairo gate itakavyopeleka chama pabaya zaidi. Wanajua ubunge ni sehemu ya kazi na maisha yao na kwa kutofaidika na mgao huenda wakaenda na maji. Ndicho kinachoonekana kuleta sintofahamu ndani ya bunge.
Ukweli unabaki pale pale, ni masilahi na si umeme kama wanavyotaka tuamini.
Kama wabunge wa CCM wangetaka suluhu ya tatizo hili tusingefika hapa tulipo. Wakati akina AL Adawi wanakuja, Ngeleja anaendeleza porojo, Symbion inabadilishwa jina kutoka Punda kuwa farasi, Songas wanazua ya kuzua n.k hakuna mbunge wa CCM aliyekuwa tayari ku-
intervene. Leo ujasiri wameupata wapi? Wote wanasema Ngeleja na Jairo wajiuzulu lakini hawasemi washtakiwe.
Umeme aongelee mwingine sio CCM.