Gamba la Nyoka... unafikiri Rais anajua uzito wa tatizo la upungufu wa nishati au anahitaji kupewa ushauri na watu wengine juu ya uzito huo?
Raisi pamoja na ufahamu wake anafanya kazi na watu, "correct information" zitakazo mfanya afikie uamuzi hazipati kwa mganga wa kienyeji, bali anzipata kutoka kwa timu yake aliyoiteua imsaidie kazi wakiwemo mawaziri.
Mathalani, Raisi anaweza akawa anfikiri option X kwa ajili ya tatizo Y, lakini wataalamu na washauri wake wakampa ushauri kwamba option X inaweza kuleta matatizo mengine huko mbeleni au isiwe effective n.k na hivyo basi wakapendekeza solution Z, lakini iwapo washauri na wataalamu hawatampa raisi option yoyote ya kutatua tatizo na raisi akaendelea kutumia option X basi mambo yakija kuharibika huko mbeleni Washauri watakuwa hawakutimiza wajibu wao ipasavyo wa kumshauri presidaa na hivyo wanapaswa kuwajibika. au kama washauri wamempa raisi ushauri Z na mambo bado yakaharibika basi Washauri hawana budi kuwajibika.
Ninachotaka kusema ni hiki, Raisi anaweza kuwa anajua kabisa uzito wa Tatizo, lakini akawa hana majibu yote ya hayo matatizo, hapo ndipo atakapotegema Wasaidizi wake waje na majibu ya hayo matatizo, sasa unaweza kuniuliza salama ya Wasaidizi ni nini basi?, Salama ya Wasaidizi iwapo wanampa raisi option za kufuata kuondoa tatizo lakini Raisi hazifuati ni kwa Wao kujiuzulu tu. Mtei alijiudhuru alipompa Mwalimu ushauri ule maarufu lakini mwalimu hakuufuata.
Na pia hatutegemei Mshauri akawa anampa raisi ushauri halafu anageuka geuka, mara aukane ushauri huo, mara amshauri tena raisi ushauri wa namna hiyo hiyo then baadae aukane tena, ikitokea hali ya namna hii basi ni jukumu la raisi kumfuta kazi mshauri huyo na kutafuta mwingine.
So far Ngeleja hana jibu lolote la Tatizo la Umeme nchini, Siwezi kumhukumu Raisi kwanza kabla ya Waziri mwenye dhamana kwa maana tukifanya hivyo, udhaifu wa Waziri mmoja mmoja utakuwa associated na Raisi kwa kusema eti "kwani raisi hajaliona mbona hajafanya chochote?", kila waziri ni lazima awajibike kwa wizara anayoiongoza!.
Na kwa kweli iwapo tatizo lingekuwa ni Raisi na si ngeleja, tayari tungeshaona Ngeleja ameshajiuzulu toka zamani!, mtu makini utafanyaje kazi na mtu ambaye unadhani ni kikwazo?. kama Ngeleja anadhani ameshafanya homework yake vizuri lakini kikwazo ni raisi, anasubiri nini kujiuzulu? kwa maana hata akikaa hapo wizarani hawezi kufanya chochote kwa kuwa raisi hamsikilizi, si ndivyo ingetakiwa kuwa?
Ngeleja should Go