UTEUZI CCM JUMUIYA: Chama cha Mapinduzi chateua wagombea nafasi ya Taifa katika Jumuiya zake zote, hawa hapa walioteuliwa

UTEUZI CCM JUMUIYA: Chama cha Mapinduzi chateua wagombea nafasi ya Taifa katika Jumuiya zake zote, hawa hapa walioteuliwa

Nimeangalia 90% ya wagombea ni waislam!! Samia anataka kurudisha ile nchi ya enzi za mwembeyanga?
Hatafutwi paroko au sista pale, anatafutwa kiongozi ambaye anaweza kuwa muislamu au mkiristo.

Kama hutaki muislamu sema awekwe wa dini gani!
 
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC) imekutana kikao cha kawaida Jumapili 13 Novemba, 2022 chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan, Makao Makuu ya Chama, Dodoma.



Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imefanya uteuzi wa majina ya wanachama watakaogombea nafasi za uongozi ndani ya CCM na Jumuiya zake katika ngazi ya Mkoa na Taifa kwa mujibu wa katiba ya CCM ya mwaka 1977 Toleo la mwaka 2022 Ibara ya 82(1). Kwa upande wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya za CCM ngazi ya Taifa walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-





NAFASI: MWENYEKITI UVCCM TAIFA

1. Farid Mohamed HAJI

2. Kassim Haji KASSU

3. Mohamed Ali MOHAMED (KAWAIDA)

4. Abdallah Ibrahim NATEPE





NAFASI: MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA

1. Khadija Khalid ISMAIL

2. Dorice John MGETTA

3. Victoria Charles MWANZIVA

4. Rehema Sombi OMARY



NAFASI: MWENYEKITI UWT TAIFA

1. Gaudentia Mugosi KABAKA

2. Kate Sylvia KAMBA

3. Dkt. Wemael Allen CHAMSHAMA

4. Mariam Mohamed LULIDA

5. Mary Pius CHATANDA



NAFASI: MAKAMU MWENYEKITI UWT TAIFA

1. Latifa Nasser AHMED

2. Thuwaybah Edington KISSASI

3. Hafsa Said KHAMIS

4. Zainab Khamis SHOMARI



NAFASI: MWENYEKITI WAZAZI TAIFA

1. Dkt. CPA. Edmund Bernard MNDOLWA

2. Fadhili Rajabu MAGANYA

3. Bakari Nampenya KALEMBO

4. Said Mohamed MOHAMED (DIMWA)

5. Mwanamanga Juma MWADUGA

6. Ally Maulid OTHMAN

7. Ali Khamis MASUDI

8. Hassan Haji ZAHARA







NAFASI: MAKAMU MWENYEKITI WAZAZI TAIFA

1. Haidar Haji ABDALLA

2. Dkt. Wemael Allen CHAMSHANA

3. Fatma Abeid HAJI

4. Rachel Ntiganyigwa KABUNDA

5. Neema George MTURO

6. Zahoro Salehe MOHAMED

7. Dogo Idd MABROUK



Uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya hizo kwa ngazi ya Taifa utafanyika tarehe 24-29 Novemba, 2022. Wagombea wote wanakumbushwa kuheshimu Kanuni za uchaguzi za CCM na misingi ya chama kwa kufanya siasa safi na kuzingatia maadili ya Chama wakati wote.



Aidha Orodha ya majina ya wagombea uongozi Chama na Jumuiya zake ngazi ya Mkoa yatatumwa katika mikoa husika.



KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI



Shaka Hamdu Shaka

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa

Itikadi na Uenezi.

13 Novemba, 2022
NAONA WAISLAMU WAMEPITISHWA WENGI SANA
 
hamna kitu hapo, ccm nawadharau sana ni kama walivaa taulo ghafla likadonkoka wanajaribu kujificha uchi usionekane...raia wamekomaa kuangalia uchi tu
 
Hatafutwi paroko au sista pale, anatafutwa kiongozi ambaye anaweza kuwa muislamu au mkiristo.

Kama hutaki muislamu sema awekwe wa dini gani!
Sijasema sitaki mi nimeongea kilichopo kwamba kateua 90% waislam basi!! Kwani nimekataa au kupinga?
 
Huyu Dr.wemael chamshana atatumikiaje mabwana wawili....

Anawania nafasi mbili KWA wakati mmoja!? Hakuna wenngine wenye sifa stahiki!? Zaidi yake!?....

Ama kweli Ccm ina wenyewe...
 
Najua vijana mliahidiwa kupita na kihongosi mnavyojificha kwenye kichaka cha naona wengi ni waislamu.

Binafsi nina furaha kubwa sana ,nilikuwa ni moja ya watia nia na sio kwamba nina furaha jina langu kutokuwepo ila kwa sababu uteuzi huu wa wajina umemshangaza kila mtu
 
Back
Top Bottom