Uteuzi: Diwani wa Kata ya Mbagala, Michael Makwega ateua wasaidizi watatu kushika nyadhifa kwenye ofisi yake

Ulikuwa unawatetea TRA, Jana Mpango kawatumbua Madanga wako ukamuunga mkono. Tumewazoea serikali isiyofuata sheria za nchi.
Umeandika nini sasa๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Oooiiiii
 
Mods watu wenye stress kama huyu dada mleta mada muwa mnawapiga ban angalau kwa wiki tu ili akili ziwakae sawa.

Ni utopolo gani sasa huu umeuleta hapa.?
Taarifa kuwafikia walaji ni moja ya namna ya kutoa hamasa katika maendeleo,labda aina na nanna ya utoaji taarifa nyenyewe.
 
Wewe ndo utopolo zaidi yake, tuambie hizo ajira alizotoa Diwani ni Kwa mujibu wa sheria ipi? Cheo cha Katibu wa Diwani kimeanza lini nchi hii? Msemaji wa Diwani analipwa toka fungu gani na majukumu yake yameandikwa kwenye mwongozo gani?
Fadhila,mpango wa ushindi ulijumuisha wengi.
 
Hii ndio awamu ya sasa nchini Tanzania ambapo kila kiongozi anayo mamlaka ya Uteuzi kwenye eneo lake, kama ambavyo Mh Diwani amefanya.

Bado haijafahamika kama wateule hawa wataapishwa lini ili waanze kulitumikia rasmi Taifa.

Amesahau tu kuandika kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya.... kifungu cha ......., Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wawamu hii tutaona mengi!
 
Halafu kila siku wako busy kuhide posts zetu zilizoshiba kisa tu zinapiga penye ukweli.

All in all huu Uzi ni wa kinafiki na kuendelea kuujadili hapa nikuendekeza unafiki na chuki binfsi.
Nalog off! Maana siyo kuwa pumba hizi.
Mnesema basi unafiki wake umekaaje..!!! kuendelea kuusema hivi sisi wengine hatujui.. TUNOANA NA NYIE WANAFIKI TU..!!! WENGINE HUWAITA HATERS...!!! Otherwise tupeni sababu ya kuona hivyo..
 
Hii ndio awamu ya sasa nchini Tanzania ambapo kila kiongozi anayo mamlaka ya Uteuzi kwenye eneo lake, kama ambavyo Mh Diwani amefanya.

Bado haijafahamika kama wateule hawa wataapishwa lini ili waanze kulitumikia rasmi Taifa.

Haya ndo Maccm๐Ÿ˜€

Hayataki kupitwa na Mwenyekiti wao mvivu wa kazi kwenye promo za kuteua na kutengua
 
Mods watu wenye stress kama huyu dada mleta mada muwa mnawapiga ban angalau kwa wiki tu ili akili ziwakae sawa.

Ni utopolo gani sasa huu umeuleta hapa.?
hahahhahha mkuu @cremia ,huyu dada yetu anazaidi ya matatizo,kama vp niunge katka juhudi zang za kumrudisha kwenye msingi..Nipo nampa ushauri pm mara kwa mara๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Hii ndio awamu ya sasa nchini Tanzania ambapo kila kiongozi anayo mamlaka ya Uteuzi kwenye eneo lake, kama ambavyo Mh Diwani amefanya.

Bado haijafahamika kama wateule hawa wataapishwa lini ili waanze kulitumikia rasmi Taifa.

Kimsingi teuzi alizofanya Mh Diwani ni batili kisheria maana Diwani hana mamlaka kisheria ya teuzi.

Ukisoma rejea za sheria hizi;
1.Katiba ya Jamhuri ya MuunganoTanzania ya mwaka 1977
2.Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya),
Sura ya 287
3.Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288
4. Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292, na 5. Kanuni za Maadili na Mwenendo wa Madiwani (Tangazo la Serikali Na. 280 la mwaka 2000).

Madiwani wanao makatibu wao ambao ni Watendandaji wa Kata, hutekeleza majukumu hayo ya kikatibu kupitia vikao vya kila robo mwaka ambavyo hukaa kila baada ya miezi mitatu ya mwaka wa serikali unaoanza julai mosi kila mwaka. Hii inamaanisha kuwa July-septemba ni robo ya kwanza, octoba-disemba ni robo ya pili, januari-march robo ya tatu na februari-juni ni robo ya nne. Vikao hivi kwa mujibu wa sheria Diwani anakuwa mwenyekiti na katibu wake anakuwa Afisa mtendaji wa Kata husika. Pia katika vikao vyote vya hadhara ambavyo watakaa na wananchi kwenye zoezi la uhamasishaji wa maendeleo. Katika kutekeleza majukumu ya kilasiku kunakuwa na mahusiano ya ukaribu ambayo hufanyika bila kuwepo na ombwe la katibu maana maelekezo yote kutoka Halmashauri na barua zote za Mheshimiwa Diwani zinapitia kwa Afisa mtendaji Kata na Mtendaji Kata humjulisha Mheshimiwa Diwani taarifa hizo pia kuwepo kwa barua zake.

Katika utendaji kazi huo Mheshimiwa Diwani hawezi kukosa mtu wa kumsaidia majukumu ya kila siku maana kila kinachofanyika kwenye Kata kinafanywa na Afisa mtendaji Kata kwa ushirikiano na Mheshimiwa Diwani kwa ukaribu.

Mfumo wa uendeshaji wa ofisi hauruhusu raia yeyote kuwa na access na mafaili ya ofisi na taarifa na vikao na barua za ofisi na hiyo ni kwasababu kwa utaratibu taarifa hizi zinapaswa kuwafikia wananchi baada ya vikao kukaa na maafikiano kufanyika. Unapomuweka mtu asiyejua taratibu na basi ofisi inakosa usiri na taratibu hukosa kufuatwa.

Ninapozungumzia usiri simaanishi jambo baya bali jambo lolote lile ambalo kwa wakati ule linakuwa bado halijawa public

Kwahiyo kwa mujibu wa barua ya Diwani huyo hakuna uhalali wowote wa kisheria labda kama anaofisi yake binafsi nje ya ile anayowajibikanayo kisheria.
 
Uzi huu uliwekwa makusudi ili kutoa fundisho , tunakushukuru
 
Back
Top Bottom