Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:
(i) Dkt. Leonard Douglas Akwilapo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Dkt. Akwilapo ni Katibu Mkuu Mstaafu, anachukua nafasi ya Prof. Penina Mlama ambaye amemaliza muda wake;
(ii) Prof. Zacharia Babubu Mganilwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. Prof. Mganilwa ni Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), anachukua nafasi ya Dkt. Naomi Katunzi ambaye amemaliza muda wake;
(iii) Dkt. Mwamini Madhebehi Tulli ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA). Dkt. Tulli ameteuliwa kwa kipindi cha pili;
(iv) Mhandisi Dkt. Richard Joseph Masika ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. Mhandisi Dkt. Masika anachukua nafasi ya Prof. Henry Mahoo ambaye amemaliza muda wake;
(v) Balozi Salome Thaddaus Sijaona ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU). Balozi Sijaona ameteuliwa kwa kipindi cha pili;
(vi) Prof. Joseph Nicolao Otieno ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala. Prof Otieno ni Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), anachukua nafasi ya Prof. Hamisi Malebo ambaye amemaliza muda wake;
Pia soma: Uteuzi Septemba 16, 2024: Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi akiwemo Katibu wa Bunge
(vii) Bi. Janet Reuben Lekashingo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini. Bi Lekashingo alikuwa Kamishna wa Tume ya Madini, anachukua nafasi ya Prof. Idris Kikula ambaye amemaliza muda wake;
(viii) Bi. Asha Dachi Mbaruk ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Magazeti Tanzania (TSN). Kabla ya uteuzi huu, Bi Mbaruk alikuwa akikaimu nafasi hiyo; na
(ix) Bi. Mariam Salehe Mgaya ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji kwenye Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI). Kabla ya uteuzi huu, Bi. Mgaya alikuwa akikaimu nafasi hiyo.