UTEUZI: Jaffar Haniu ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu); amrithi Gerson Msigwa

UTEUZI: Jaffar Haniu ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu); amrithi Gerson Msigwa

Kwa nini msemaji mkuu wa serikali awe tofauti na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu?
Ikulu ni idara ndani ya Serikali. Msemaji wa Ikulu hawezi kuwa msemaji wa serikali. Msemaji Mkuu wa serikali huratibu pia usemaji ndani ya wizara, taasisi, mashirika na wakala za serikali.
 
Msigwa ni msemaji mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa habari MAELEZO.Hiyo kazi maalumu Ni ipi.
Ninachomaanisha cheo cha msemaji mkuu wa serikali akina tija kama kilivyo cha waziri katika ofisi ya rais kazi maalum. Vingefutwa ili kupunguza mzigo kwa walipaji kodi.

Kwa mtazamo wangu, msemaji Mkuu wa serikali hawezi kufanya kazi bila kugombana na viongozi wa wizara au hatapewa ushirikiano!!
 
Ikulu ni idara ndani ya Serikali. Msemaji wa Ikulu hawezi kuwa msemaji wa serikali. Msemaji Mkuu wa serikali huratibu pia usemaji ndani ya wizara, taasisi, mashirika na wakala za serikali.
Msemaji wa Ikulu anaweza kabisa kuwa ndo msemaji wa serikali maana ikulu ndo ofisi ya mkuu wa serikali.

Binafsi sioni tofauti kubwa ya hivyo vyeo.
 
Mmoja anahusika zaidi na mambo ya ofisi ya rais kama teuzi na tenguzi za rais, mwingine anahusika mambo ya serikali nzima kama kujibu habari za Tanzania kujihusisha kuuzia silaha waasi Burundi.
Haniu alikuwaga ikulu. ndiye aliyeandika barua ya taarifa ya uteuzi wa msigwa. Leo yeye ndio anayeandikiwa na msigwa
je inamaana hakuna mtu mwingine anayefit kwenye iyo nafasi? kwann nafasi hizi mama anazunguka mumo mumo?
 
Hongera Haniu.
hakika anastahili.
sasa chapa kazi, tunategemea ubunifu na umahiri.
 
Watu wa mtandao wa Awamu ya nne wanarudishwa kwa kasi kubwa.

Jamaa zake Hayati JPM macho yamewatoka kama mafundi saa wamepigwa butwaa nzito.
 
Back
Top Bottom