UTEUZI: Jaffar Haniu ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu); amrithi Gerson Msigwa

UTEUZI: Jaffar Haniu ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu); amrithi Gerson Msigwa

Haniu alikuwaga ikulu. ndiye aliyeandika barua ya taarifa ya uteuzi wa msigwa. Leo yeye ndio anayeandikiwa na msigwa
je inamaana hakuna mtu mwingine anayefit kwenye iyo nafasi? kwann nafasi hizi mama anazunguka mumo mumo?
Kanuni za usalama zinasema kwamba, unavyozidisha watu kwnye kazi za siri nyeti, ndivyo unazidisha uwezekano wa usiri na usalama kubomolewa.

Hivyo, labda wanaona badala ya kuweka watu wapya ambao hawajahakikiwa, waendelee na hawa hawa wakongwe.
 
Kiranga una vituko, nadhani na kuhusu corona imefika wapi, au?
Corona huku Marekani ni aina ya bia watu wanakunywa.

Asilimia 70 ya watu wazima Mqrekqni wamechanjwa dhidi ya Covid-19.

Binafsi nimechanjwa sindano mbili za Pfizer.

Sasa hivi tunachanja watoto wa kuanzia miaka 12 mpaka 17.

Maambukizi yamwpungua sana kutokana na chanjo kusaidia.

Ila bado kuna vichwangumu hawataki chanjo.
 
Hahaha!

Jen Psaki ni White House spokeswoman.

Ila kila wizara ina msemaji wake mkuu.

Nadhani hivyo ndivyo inafaa iwe.

But I digress. Nisije kuambiwa nahoji kisa simpendi huyo Mama.

Manake sasa hivi hatupaswi kuhoji chochote kile.
Hata hapo nyuma kidogo tulikua hatuhoji chochote [emoji40][emoji40][emoji40]
 
Kwanini unashangaa kwa sasa wakati sio mara ya kwanza? Hujioni kama mnafiki!
Nashangaa kwa sababu nilitegemea hayo mambo yasingeendelea na utawala huu mpya!

Mabaya yanaachwa. Mazuri yanaendelezwa.

Sioni unafiki unaingiaje kwenye mlinganyo!

Boresha msamiati wako wa Kiswahili ujifunze fasili za maneno utumiayo.
 
Kanuni za usalama zinasema kwamba, unavyozidisha watu kwnye kazi za siri nyeti, ndivyo unazidisha uwezekano wa usiri na usalama kubomolewa.

Hivyo, labda wanaona badala ya kuweka watu wapya ambao hawajahakikiwa, waendelee na hawa hawa wakongwe.
Myopic,

Kufanya hivyo ni kutengeneza gap kubwa sana kiutendaji, itafika mahali hao wakongwe nature itafanya selection hawataweza kudeliver na hakutakuwa na replacement.

Hakuna mbadala wa kutoleta watu wapya.
 
Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi katika kazi yake
 
Nishafanya hivyo mara nyingi sana.

Sina sababu ya kurudia.

Hutaki, unaacha.
Sa unalalamika nini wakati mambo hayo hata mungu wako alifanya na ukaona ni halali. Leo anafanya Rais wetu mwenye utu unaona ajabu!🤔
 
alaaa,, Leo kifutwe!!!!!

Wakati wa dikteta hamkusema ivyo
Kama si kusema jambo fulani wakati wa Kikwete nilikuwa sina haki ya kulisema wakati wa Magufuli!

Na kama si kuhoji wakati wa Mkapa nilikuwa sina haki ya kuhoji wakati Kikwete.

Mnashangaza!!
 
Sa unalalamika nini wakati mambo hayo hata mungu wako alifanya na ukaona ni halali. Leo anafanya Rais wetu mwenye utu unaona ajabu!🤔
1. Sina mungu. Kama Samia wewe ni mungu wako, usidhani na wengine wanaabudu kama wewe.

2. Hata Magufuli nilimkosoa sana tu. Na huo ni ukweli usiopingika. Huwezi kabisa kuupinga ukweli huo.

3. No one is above criticism and no one is below praise.

4. Anybody can get it. Including you.
 
Back
Top Bottom