Uteuzi Juni 15, 2024: Mobhare Matinyi, aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali apangiwa majukumu mengine, nafasi yake yachukuliwa na Thobias Makoba

Uteuzi Juni 15, 2024: Mobhare Matinyi, aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali apangiwa majukumu mengine, nafasi yake yachukuliwa na Thobias Makoba

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
1718479712217.png

Rais Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

i Amemteua Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi, Balozi Dkt. Simbachawene alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.

ii. Amemteua Bw. Nkoba Eliezer Mabula kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia utalii. Kabla ya uteuzi, Bw. Mabula alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.

Aidha, CP. Benedict Wakulyamba atakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia maliasili.

iii. Amemteua Dkt. Habib Gallus Kambanga kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi, Dkt. Kambanga alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.

iv. Amemteua Bw. Thobias Makoba kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi, Bw. Makoba alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Bw. Makoba anachukua nafasi ya Bw. Mabhare Matinyi ambaye amepangiwa majukumu mengine.

V. Amemteua Bw. Ally Rajab Mketo kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe. Kabla ya uteuzi, Bw. Mketo alikuwa Afisa Tawala Mwandamizi, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukombe. Bw. Mketo anachukua nafasi ya Bw. Onesmo Kisoka ambaye amestaafu.

vi. Amemteua Jaji Dkt. Mary Caroline Levira kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. Jaji Dkt. Levira ni Jaji wa Mahakama ya Rufani. Jaji Dkt. Levira anachukua nafasi ya Jaji Dkt. Gerald Ndika ambaye amemaliza muda wake.

vii. Amemteua Dkt. Leonard Douglas Akwilapo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Dkt. Akwilapo ni Katibu Mkuu Mstaafu na Mhadhiri Mwandamizi, Kikuu Kikuu cha Dodoma. Dkt. Akwilapo anachukua nafasi ya Prof. Maurice Mbago ambaye amemaliza muda wake. Amemteua Dkt. Noel Eusebius Mbonde kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala.

viii. ya Chuo cha Ufundi Arusha. Dkt. Mbonde ni Mkurugenzi Mstafu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.


20240615_201334.jpg

20240615_201332.jpg

============

THOBIAS MAKOBA NI NANI?

Kabla ya kujiunga na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Makoba alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Pamoja na kushiriki katika majukwaa mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo UN, African Union, SADC, EAC, World Economic Forum na mengineyo, kwa vipindi mbalimbali aliwahi kuwa Katibu wa Mawaziri wawili wa Mambo ya Nje Bernard Membe na baadae Balozi Dokta Augustine Mahiga kabla ya Kwenda kuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi katika Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar.

Bw. Makoba ana Masters Degree in Security and Strategic Studies kutoka National Defence College – Tanzania, Post-Graduate Diploma in Economic Diplomacy kutoka Chuo Cha Diplomasia Kurasini na Degree ya kwanza ya Political Science and Sociology with majors in International Relations.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Habari ndio hiyo wenye kupata wamepata na wenye kuhamishwa wamehamishwa.

Ila tu fahamu ya kuwa msemaji wa serikali wa sasa ameondolewa kwenye nafasi yake na atapangiwa kazi nyingine.

Kazi iendelee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti

Lucas Hebel Mwashambwa.mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili
IMG-20240615-WA0007.jpg
IMG-20240615-WA0008.jpg
 
Bado najiuliza BARUA Official inayotoka kwa UMMA na inayobeba MAMLAKA makubwa kiasi hichi inakuwa na DOSARI/KASORO ndogo ndogo za kiuandishi kiasi hichi na mtu anatia SAINI kabisa???

NAJIULIZA hili swali kila siku.
 
Back
Top Bottom