Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya

1. Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria;

2. Mhe. William Vangimembe Lukuvi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu);

Naona makaka wa mama wamerudi...

Hapo kwa Kabudi, je mama anataka kufufua mchakato wa katiba mpya au anataka kupambana na ombwe la mikataba mibovu inayotafuna nchi?
 
Hamza Johari nilimfahamu kwenye mazishi last two weeks. Zaidi ya hapo sikuwa namjua kwa sura zaidi ya kumsoma kwenye mikataba ya kimataifa tunayoingia hasa DP World alikuwa analivalia njuga kuwaunga mkono kama ana shares vile.
 
Mjia
Wanachadema mjiandae kwa vijembe vya chura kiziwi akiwa anawaapisha hao jamaa zake
 
Hamza Johari umepambana sana kwenye mikataba mingi nyeti na simu yako muda mwingi haipokelewi kumbe ni masuala nyeti yanayokupa cheo kikubwa cha mwanasheria mkuu wa serikali.

Kwa umahiri mkubwa uliuandaa mkataba wa DP World na sasa hivi matunda yake yanaonekana kwa kuweza kurahisisha biashara pale TPA.

Mungu aendelee kukutunza na kukupatia afya njema, mwana-ukraine wa jiji la Kiev kabla halijapigwa na Putin.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…