Squidward
JF-Expert Member
- Jul 21, 2014
- 7,828
- 9,546
Hii nchi kuendelea sio Leo , kila Siku teuzi lini watafanya kazi !
Mbaya zaidi teuzi zao ni za watu wale wale as if tuliobaki ni mazombi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii nchi kuendelea sio Leo , kila Siku teuzi lini watafanya kazi !
Hapana anatoa circle ya wajinga ambao wamemcost sana Hasa wale aliowatoa kipindi cha jpmNi mwendo wa mikeka tu.
Toa huyu weka yule.
anatengeneza circle ya wajinga tu.
Me too!.Naanza kumpenda huyu bibi mdogo mdogo
Labda alienda kumpigia Hangaya magoti baada ya kuona taarifa humu.Mwigulu Nchemba amesalimikaje , au britanicca alitudanganya
Masikini alivyokuwa anampamba samia, leo kamtoa kweli?Ummy Mwalimu out!
britanicca hongera, uliandika wiki 2 zilizopita kuwa huyu atamwagwa.
Bado Mwigulu Nchemba yumo
Watu walisha mwambia wenzake wanafanya uchawa wenye akili wanapata shavu yeye anatumika kama kopo la chooniLukasi mshamba hayumo ??????
Watajua wenyewe na teua na Tenguzi zao , hatutoki kwenye mstari safari hii, kwa ukatili waliofanyiwa chademaTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa na kuhamishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo:
A: Uteuzi wa Mawaziri
1. Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria;
2. Mhe. William Vangimembe Lukuvi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu);
3. Mhe. Jenista Joackim Mhagama (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Mhagama alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu); na
4. Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Chana alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, anachukua nafasi ya Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais.
B: Uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Jaji wa Mahakama ya Rufani
1. Bw. Hamza Johari ameteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Johari alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), anachukua nafasi ya Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani;
2. Bw. Samwel Maneno ameteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Maneno alikuwa Msaidizi wa Rais, Sheria. Bw. Maneno anachukua nafasi ya Balozi Prof. Kennedy Gastorn ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, Sheria na Mikataba; na
3. Dkt. Ally Saleh Possi ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Possi alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi.
C: Uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa na Naibu Makatibu Wakuu
1. CP. Salum Hamduni ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga. Kabla ya uteuzi huu, CP. Hamduni alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), anachukua nafasi ya Prof. Siza Tumbo ambaye amerejea Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA);
2. Bw. Ismail Rumatila ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Afya. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Rumatila alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA);
3. Bw. Atupele Webster Mwambene ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya elimu. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mwambene alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia;
4. Bw. Abdul Rajab Mhinte ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia mifugo. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mhinte alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu; na
5. Bw. Methusela Stephen Ntonda ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Ntonda alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.
D: Uhamisho wa Naibu Makatibu Wakuu
1. Dkt. Grace Elias Magembe amehamishwa kutoka Wizara ya Afya kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya afya;
2. Dkt. Charles Enock Msonde amehamishwa kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi;
3. Dkt. Wilson Mahera Charles amehamishwa kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia masuala ya elimu ya msingi na sekondari;
4. Prof. Daniel Elius Mushi amehamishwa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia masuala ya sayansi na elimu ya juu;
5. Dkt. Franklin Jasson Rwezimula amehamishwa kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria;
6. Dkt. Khatibu Malimi Kazungu amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya umeme na nishati jadidifu.
Aidha, Dkt. James Peter Mataragio atakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya petroli na gesi;
7. Bw. Ludovick James Nduhiye amehamishwa kutoka Wizara ya Ujenzi kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi;
8. Dkt. Suleiman Hassan Serera amehamishwa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya ushirika na umwagiliaji.
Aidha, Dkt. Hussein Mohamed Omar atakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya maendeleo ya mazao na usalama wa chakula.
E: Uhamisho wa Wakuu wa Wilaya
1. Kanali Maulid Hassan Surumbu amehamishwa kutoka Wilaya ya Tarime kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali. Kanali Sulumbu anachukua nafasi ya Brigedia Jenerali Denis Filangali Mwila ambaye amepangiwa majukumu mengine;
2. Meja Edward Flowin Gowele amehamishwa kutoka Wilaya ya Rufiji kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime;
3. Bw. James Wilbert Kaji amehamishwa kutoka Wilaya ya Tanga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi;
4. Bw. Zephania Stephan Sumaye amehamishwa kutoka Wilaya ya Moshi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto;
5. Bw. Japhari Kubecha Mghamba amehamishwa kutoka Wilaya ya Lushoto kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga;
6. Bi. Rebecca Sanga Msemwa amehamishwa kutoka Wilaya ya Morogoro kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi;
7. Bi. Gift Isaya Msuya amehamishwa kutoka Wilaya ya Bahi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani; na
8. Bw. Mussa Ramadhani Kilakala amehamishwa kutoka Wilaya Pangani kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.
F: Uteuzi wa Katibu Tawala wa Wilaya
1. Bi. Proscovia Jaka Mwambi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukoba.
G: Uhamisho wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri
1. Bw. John Lipes Kayombo amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha;
2. Bw. Juma Hamsini Seph amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga;
3. Bw. Fredrick Damas Sagamiko amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma;
4. Bw. Elihuruma Mabelya amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam;
5. Bw. Jomary Mrisho Satura amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke;
6. Bi. Joanfaith John Kataraia amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida;
7. Bw. Jeshi Godfrey Lupembe amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro;
8. Bw. Khamis Jaaphar Katimba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi;
9. Bi. Rose Robert Manumba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala;
10. Bw. Stephen Edward Katemba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali;
11. Bw. Missana Kalela Kwangura amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga;
12. Bi. Happines Joachim Msanga amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe; na
13. Dkt. Amon David Mkoga amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
H: Uteuzi wa Wakuu wa Taasisi
1. Bw. Crispin Chalamila ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Kabla ya uteuzi huu, Bw. Chalamila alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu;
2. CPA. Moremi Andrea Marwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Kabla ya uteuzi huu, CPA. Marwa alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Magereza (SHIMA); na
3. Dkt. Irene Isaka ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Aidha, uapisho wa Mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Katibu Tawala wa Mkoa na Naibu Makatibu Wakuu wateule utafanyika Ikulu - Dar es Salaam kesho tarehe 15 Agosti, 2024 saa 8.00 mchana.
PIA SOMA
- Uteuzi Agosti 6, 2024: Rais Samia afanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali
View attachment 3070207
View attachment 3070209
View attachment 3070210
View attachment 3070211
View attachment 3070247
Safari hii ni kulamba Asali kwa zamu.
Na kumpa check disability kuwa maanasheria mkuuKipindi hiki tutaona mengi😂😂 Hadi maji yatapanda mlima.
Huyu mama alikurupukaga kumtoa kabudi na lukuvi ona sasa.
Alidanganywa na kuwatoa watu wema na kuwarudisha wezi lipuyanga kutoa watu wa kazi Takukuru, Ofisi Dpp na ofisi ya Mwanasheria mkuu hizi ndizo Taasisi zina pambana na wezi na wahujumu uchumi, sasa yeye alidanganywa na Msoga akaweka watu ili wawatoe mafisadi, huyu Mkurungenzi wa Takukuru tokea angle Madarakani hajawai kumstaki mtuumiwa yoyote wa ufisadi nchi hii na mafisafi wapo wanatamba tu, kazi yake ilikuwa kutangaza wameokoa billion Mia ukimwambia azionyeshe zilipo hajui zilipo.Sasa kwa nini aliwatoa? Mbona anarudi kule kule kwa timu Magufuli