Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya

Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya

Palikuwepo Three The Hardway Makamba, Ummy na Awesu

Mwamba aliyebaki ni Awesu na Wadogo zake akina MwanaFA

Tanga kunani paleee 😂
 
Hii ya mwanasheria mkuu wa serikali na CP Hamduni aliyekuwa boss wa Takukuru unahitaji moyo wa ziada kuendelea kufanya kazi.
 
Rais wetu chonde chonde, tunakuomba urudishe Dr Dorothy Gwajima wizara ya afya. Huyo ndiye mtu sahihi kuinyoosha wizara hiyo. Na anajua vilio vya Watanzania kwani tukitoa maoni au kero kwenye mtandao ya kijamii hapo hapo Dt anachukua hatua. Please mom, return this humble, genius Dr Gwajima.
 
Wazee naona wameshajirekebisha, sasa wafanye kazi yao katika Serikali pia kukiunganisha chama upya.

Naona timu Jiwe inarudi mdogo mdogo baada ya ile Msoga nyingine timu Msoga kujeruhiwa.

Yajayo yanafutahishandani ya chama chetu.
 
Majina ni haya haya sijawahi kuona majina mapya Mimi yaani hakunaga ingizo Jipya ni hao hao tu wana-rotate akitoka hapa anaingia pale akitoka pale anaingia pale hakuna watu wapya wapya wenye utendaji mpya mpya yaan watendaji ni wale wale tu na majina ni yale yale tu labda mpaka wafe leo Naibu katibu kesho kawa mkurugenzi kesho kutwa huyo huyo kawa katibu mkuu yaan anazunguka hapo hapo
 
Yaani mtu anatolewa chumba hiki anawekwa koridoni kesho anapelekwa chumba hiki yule anawekwa sebuleni na yeye kesho atapelekwa dining keshokutwa atarudishwa chumba kile. HAKUNA KIPYA WATU WALEWALE TU WANAZUNGUKA UJINGA MTUPU
 
Hivi Lucas Mwashambwa Chawa mtiifu wa mama kwanini hawamkumbuki jamani kumpa hata ukuu wa wilaya?
 
Sasa ni rasmi Samia amekiri alidanganya sana Kuhusu JPM. Wale wote JPM aliwatafuta wamerudishwa. Kabudi, Makonda, Lukuvi, Hapi Asante mama kwa kukataa Fitna za akina Nape na Makamba
Kinachowasumbua utendaji wao au Chadema? Mbona mnateseka sana?
 
HATA WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA ALISEMA,MKIAMBIWA MSIFANYE FUJO,MKAWA MNA KAIDI MTAPIGWA TUH...KWAHIYO SUALA LA CHADEMA KUPIGWA KWANI JIPYA??FANYA FUJO UONE...
 
Back
Top Bottom