Uteuzi majaji Mahakama ya Rufani utaharakisha mlundikano wa kesi?

Uteuzi majaji Mahakama ya Rufani utaharakisha mlundikano wa kesi?

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Judicial-Conflict-ResolutionJudicial-Conflict-Resolution.jpg

Mei 20, Rais Samia Suluhu Hassan aliteua majaji tisa wa Majaji wa Mahakama ya Rufani na hivyo kuongeza idadi yao kufikia 49. Uteuzi huo umeibua matumaini utatuzi wa ucheleweshwaji wa kesi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ni pamoja na Abdi Shaaban Kagomba Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Yohane Bokobora Masara Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha, Immaculata Kajetan Banzi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kagera, Rabia Hussein Mohamed ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Wengine ni Cyprian Phocas Mkeha Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Dar es Salaam, Yose Joseph Mlyambina Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dar es Salaam, Imani Daud Aboud - Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mzee Ibrahim Ibrahim - Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar na Juliana Laurent Masabo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Akizungumzia uteuzi huo, Wakili Peter Madeleka amesema uteuzi huo ni wa muhimu kwa sababu ya upungufu wa majaji kulingana na idadi ya Watanzania.

“Kwa ongezeko la idadi ya watu, uteuzi wa majaji 9 wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania ni wa muhimu, kwani sasa watafikia 49. Hata hivyo, bado hawatoshi, kwani siku hizi, mahakama za rufani zipo kila mkoa, tofauti na zamani ambapo Mahakama za rufani zilikuwa kwa kanda,” amesema.

Amesema kutokana na idadi ya Watanzania bado kuna haja ya kuteua majaji wengi Zaidi ili kuharakisha usikilizwaji wa kesi.

“Idadi ya majaji 49, bado haitoshi, kwani kuna kesi nyingi hazijasikilizwa na nyingine zinaendelea kufunguliwa. Kwa mfano kesi ya Lissu (Tundu Lissu- Mwenyekito wa CHADEMA), mpaka sasa ina miezi miwili na haijulikani itasikilizwa nini, hiyo ni kwa sababu ya uchache wa majaji,” amesema.

Maelezo yake yameungwa mkono na Wakili John Seka akisema majaji waliopo bado ni wachache.

“Kwa hali ilivyo sasa ni lazima mahakama iwe sehemu ya kupaki kesi, kwa sababu mpaka sasa hivuo majaji wanasikiliza kesi za mwaka 2023 na kwa kuwa kukata rufaa ni haki ya mtu, basi kesi zinaendelea kufunguliwa,” amesema.

Akieleza utaratibu wa mahakama hiyo, Seka amesema hufanya kazi kwa session na wanatembelea mikoani.

“Tofauti na Kenya au India ambako Mahakama ya Rufani zinafanya kazi kila siku, hapa kwetu, majaji wakitoa mkoa mmoja unaweza kupita mwaka mzima ndiyo wakarudi tena,” amesema.

Ameongeza: “Kwa hiyo uteuzi ni wa muhimu na bado wanatakiwa waongezwe.”
 
Back
Top Bottom